Tafuta

2021.04.15 Rosario Livatino 2021.04.15 Rosario Livatino 

Papa:Ushuhuda wa Livatino ufanye kuhisi wote ni ndugu

Ifuatayo ni dibaji ya Papa Francisko katika kitabu kilichoandikwa na Vincenzo Bertolone kuhusu hakimu mwathirika wa kikundi cha kihalifu kiitwacho mafia.

PAPA FRANCISKO

Rosario Angelo Livatino (3 Oktoba 1952-21 Septemba 1990) [...] Hakimu wa Canicattì aliyeuwawa kwa sababu ya uthabiti wa kikristo na kitaaluma, mikononi mwa kikundi cha wahalifu ambao walikuwa wanadhibiti eneo la Sicilia kwenye miaka ya Themanini katika karne iliyopita na aliondolewa katika janga la kusikitisha na wauaji vijana  waliolipwa na viongozi wa Stidde na wa Cosa Nostra.

"Wadogo ni kitu gani nimewafanyia?"  Ndivyo aliweza kuwauliza kabla ya uso wake kama wa Mtoto Yesu haujaharibiwa na risasi, kama vile alivyoeleza rafiki yake. Yalikuwa ni maneno ya nabii anayekufa akitoa sauti ya kulalamika, ya mwenye haki ambaye alitambua kuwa hakustahili kifo hicho kisicho cha haki. Maneno ambayo yalikuwa yanapaza sauti dhidi ya maherodi wa wakati wetu, ambao hawatazami uso wa yoyote hasiye na hatia, hata kufikia kuwaadaa vijana wasio na huruma kuingia utume wa kifo. Kilio cha maumivu na wakati huo huo  cha ukweli, ambacho kwa nguvu zake huangamiza majeshi na kila mtindo unaojihusisha kukanusha undani wa Injili, lakini licha ya wao kuwa na onesho la karne nyingi za kuwa na picha takatifu, za sanamu takatifu na kwa kulazimishwa kupiga magoti yasiyo na heshima, za upeperushwaji wa udini uliokanushwa.

“Kwa sababu hii, nikifikiria sura ya hakimu wa Sicilia, ninarudia kile nilichosema katika Ukumbi wa  Clementina mnamo tarehe 29, Novemba 2019 kwamba:  “Livatino ni mfano, sio tu kwa sababu alikuwa hakimu, bali kwa wale wote wanaofanya kazi katika uwanja wa sheria: imani na kujitoa kwake kufanya kazi, na kwa umuhimu wa tafakari zake” []. Mada juu ya Rosario Livatino inashangaza, kwa sababu inajikita katika ishara za kile ambacho kingeibuka na ushahidi mkubwa katika miongo iliyofuata, na  sio tu nchini Italia, ambayo ni, haki ya kuingiliwa kwa jaji katika maeneo ambayo sio yake mwenyewe, lakini hasa katika masuala ya kile kinachoitwa “haki mpya”, na hukumu ambazo zinaonekana kuhusika na kutimiza matamanio mapya kila wakati, zilizojitengwa na upungufu wowote wa malengo”

Papa Francisko anaendela kuandika kuwa: Kwa kutembelea Agrigento na maeneo mengine huko Sicilia mnamo 1993, mtangulizi wangu Mtakatifu Yohane  Paulo II  mwishoni mwa maadhimisho ya  Ekaristi iliyoadhimishwa katika Bonde la Mahekalu, alisema “ Kuwe na maelewano katika nchi yenu hii! Maelewano bila vifo, bila kuuawa, bila woga, bila vitisho, bila waathiriwa! Utangamano huu, amani hii ambayo kila mtu na kila utu wa kibinadamu na kila familia anatamani! Baada ya kuteseka mara nyingi, mwishowe kuna haki ya kuishi kwa amani”. Na wale ambao wana hatia ya kuvuruga amani hii, wale ambao husababisha waathirika wengi wa kibinadamu kwa dhamiri zao, lazima waelewe,  kwamba watu wasio na hatia hawaruhusiwi kuuawa! Mungu siku moja alisema: “Usiue”: mtu, yeyote, mkusanyiko wowote wa kibinadamu, mafia, hawezi kubadilika na kukanyaga haki hii takatifu ya Mungu!”.

Harufu nzuri ya Kristo ambayo huenea kutoka katika mwili uliouawa wa jaji kijana basi uwe mbegu ya kuzaliwa kwa upya kama ilivyotokea tayari kwa wote wauaji na wakuu wengine ambao  leo hii wako kwenye njia ya toba na uongofu  kwa sisi sote, hasa kwa wale ambao bado wanapata hali za vurugu, vita, mashambulio, mateso kwa sababu za kikabila au kidini, na ukiukwaji dhidi ya utu wa binadamu. Kwa Rosario Angelo Livatino, leo hii pia kupitia kutangazwa kuwa mwenyeheri tunatoa shukrani kwa mfano aliotuachia, ya kwamba kila siku tumepambana vita vizuri vya imani kwa unyenyekevu, upole na huruma. Ni  kwa jina la Kristo, daima bila kuacha kabisa imani na haki, hata katika hatari ya kifo ndiyo inakuwa mbegu iliyopandwa, na hii  ndio matunda yatakayokuja.

04 May 2021, 17:49