Tafuta

Katika sala ya Rosari kwa mwezi wa tano ambayo kwa namna ya pekee Papa ameomba ili janga liisha anaomba pia  kusali kwa ajili ya Myanmar Katika sala ya Rosari kwa mwezi wa tano ambayo kwa namna ya pekee Papa ameomba ili janga liisha anaomba pia kusali kwa ajili ya Myanmar  

Papa:Tuombee nchi ya Myanmar kwa mwezi wa Maria

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa mbingu Dominika,pmoja na kusali ili jaga liishe ametoa wito pia kusali kwa ajili ya Myanmar katika mwezi wa Rozari.Amekumbusha kutangazwa kwa mwenye heri José Gregorio Hernández huko Caracas,Venezuela.Amewatakia heri ya Pasaka waorthodox na kuwaombea waathirika la janga lililotokea nchini Israeli.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, amekumbusha jinsi ambavyo tayari tumekwisha ingia kwenye mwezi wa tano ambao kwa watu walio wengi wanajieleza kwa namna mbali mbali ya ibada ya Bikira Maria. “Mwaka huu sala hiyo itakuwa na tabia Marathoni kupitia madhabahu muhimu ya Mama Maria, ili kuaomba janga liishe. Jana jioni ilikuwa ni hatua ya kwanza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro”, Papa amesema.

Kuombea Myanmar

Papa Francisko ameongeza: “Katika mantiki hii, kuna mpango ambao upo ndani ya moyo wangu. Ni kwa lile Kanisa la Birmania ambalo ninawaalika kusali kwa ajili ya amani nchini Myanmar kwa sala ya Salam Maria katika Rosari ya kila siku. Kila mmoja wetu, amwelekee mama anapokuwa katika mahitaji na shida; na sisi katika hili kwa mwezi, tuombe mama yetu wa Mbingu azungumze katika moyo wa wote wahusika wa Myanmar, ili wapate ujasiri wa kuanza  mchakato wa kukutana, kupatana na wa amani", Papa amehimiza

Mwenye heri mpya wa Venezuela

Papa Francisko amekumbusha kutangazwa kwa mwenyeheri José Gregorio Hernández Cisneros huko Caracas, nchini Venezuela, Ijumaa tarehe 30 Aprili 2021, aliyekuwa mwamini mlei. Papa amesema kwamba alikuwa ni daktari aliyebobea sayansi na wa imani. Aliweza kutambua kupitia wagonjwa uso wa Kristo na kama Msamaria Mwema, aliwahudumia kwa upendo wa kiinjili. Mfano wake utusaidie kuwa na utunzaji kwa wale ambao wanateseka katika mwili na kiroho. Papa ameomba kumpigia makofu kwa ajili ya Mwenyeheri mpya.

Pasaka ya Kiorthodox

Papa Fracisko amewatumia heri nyingi kwa ndugu, kaka na dada wa Makanisa ya Kiorthodox na makanisa Katoliki ya Mashariki na kilatini ambao leo hii kwa mujibu wa kalenda ya kijuliani wameadhimisha Siku Kuu ya Pasaka. "Bwana mfufuka awajalie mwanga, amani na kuwapa nguvu jumuiya ambazo wanaishi hali kwa namna fulani ngumu", ameeleza Papa.

Uchungu wa Papa kwa ajali ya Israeli

Papa Fracisko vile vile kwa uchungu ameelezea ukaribu wake kwa watu wa Israeli kufuatia na ajali iliyotokea Ijumaa tarehe 30 Aprili juu ya kilima cha Meron waktiti wanafanya sherehe zao za kiutamaduni, na kusababisha vifo vya watu 45 na majeruhi wengi. Amewakikisha kuwakumbuka katika sala kwa ajili ya waathiriwa wote wa janga hilo na kwa ajili ya familia zao.

Chama cha Meter:Kusaidia waathirika wa vurugu na unyonyaji

Papa Francisko akiendelea, wazo lake limewaendea hata Chama cha Meter ambacho amewatia moyo wa kuendeleza juhudi kwa ajili ya watoto waathirika kwenye vurugu na unyonyaji. Hatimaye amewasalimia kwa moyo wote waliokuwa wamekusanyika katika uwanja huo, warumi na mahujaji kutoka pande mbali mbali za nchi. Amewasalimia pia kwa namna ya pekee Wanaharakati wa kisiasa, wa Jumuiya wafokalari iliyoundwa na Chiara Lubich miaka 25 iliyopita. Amewatakia kazi njema ya huduma ya kufanya siasa iliyo njema. Amehitimisha akiwatakia Domika njema, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

02 May 2021, 13:21