Tafuta

Vatican News
2021.05.21 Wjumbe wa Chama cha "Lazare" 2021.05.21 Wjumbe wa Chama cha "Lazare"  (Vatican Media)

Papa kwa maskini&wasio kuwa na makazi:Ninyi ni tunu yenye thamani

Katika mkutano wa Papa na chama cha kifaransa kiitwacho Lazare ambacho kinasaidia maskini na wasio na makazi,katika kuadhimisha mwaka wa 10 tangu kuanizhswa kwake,ameshauri waendelea kuwa mashuhuda wa huruma ya Mungu katikati ya utamaduni wa ubinafsi,kutojali,na kudharau.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Chama cha ‘Lazare’, kinachojikita kusidia maskini na wasio kuwa na nyumba, ambapo mwaka huu wanaandimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Katika ujumbe wake alioukabidhi kwako anamshukuru Mungu kwa kufanya mkutano huo na ambao mwaka jana ulifutwa kutokana na mgogoro wa kiafya. Daima ni furaha kwake kuona hata watu wengi walio na imani, mapenzi mema na ujasiri wa kuishi uzoefu wa kutoa huduma na udugu. Amelezea juu ya chama chao ambacho kimejengwa juu ya misingi rahisi kwa mfano kuwa wenyewe kwa ajili ya kujitoa kusaidia wengine, kutafuta furaha, kuhisi wamependwa, kujifunza wema kama familia, kuishi pamoja kwa urahisi sana.

Misingi hii ina maana ya kupanua wigo katika utamaduni ni msimama ikiwa inabubujika na urafiki wa nguvu na Kristo, ambaye ni kisima cha utendaji wao wa wema. Papa amesema kuwa tendo la kwenda kukutana na wengine katika hali mbali mbali na kuunda familia, kunajenga maelewano na furaha ya kuishi kwa pamoja na wao wanashiriki katika utume wa Kanisa la kwenda katika pembezoni mwa maisha yetu. Kama alivyokuwa amewaeleza katika  ujumbe kwa njia ya video mwaka jana tarehe 29 Mei 202, amethibitisha kuwa pembezoni mwa maisha ndiyo kitovu cha moyo wa Mungu. Yesu alipenda kuja katika pembezoni mwa maisha yetu. Yeye mwenyewe alijifanya kuwa wa pembeni.

Chama hiki limependa kuwa kwa wwatu ambao wanahudumu kama, mkono, macho, masikio, tabasamu ya Mungu. Kama waoa wanaonesha ukaribu wa Bwana ambaye anatunza watu wake hasa wale ambao wamejeruhiwa, na kuelemewa kutokana na mizigo ya maisha ili upendo uweze kuwa kweli na pasipotee kitu ambacho ni cha lazima katika mabadiliko ya historia inayoelekeza wema wa walio wa mwisho ( Fratelli tutti165). Katika jitihada zao, wanatafuta kuwa wakristo ambao si kwa maneno tu bali kwa matendo. Na kwa maana hiyo wanazaa matunda mengi ambayo yanaonesha na kupanuka katika chama chao katika Nchi mahalia na mabara.

Papa amewaomba wasiwe na hofu ya kuwasha moto wa matumaini na upendo. Wao ni mashuhuda wa huruma ya Mungu katikati ya utamaduni wa ubinafsi, sintofahamu, kutojali, kutupa, kudharau maskini na wadhaifu. Kwa kuanzisha uzoefu hu wao wanaishi upendo na hatua nzuri ya historia yao iliyojaa wakati mwingine na uchungu, upweke , machoz, majaribu, kubaguguliwa na kukataliwa, wao ni zawadi yenye thamani ambavyo inafanya kuona upendo wa Bwana. Papa amesisitiza kuwa wao hawajabaguliwaau kuwa watu wa chini, watu walioshindwa, kama jamii inavyotaka kuwaaminisha. Machoni pa Mngu wao ni tunu, zawadi, maisha na hadhi.  Katika sura zao kunonekana matendo ya Kristo ambaye anatualika kuwa na upendo wa dharura na ufunguzi wa moyo.

Papa anawashauri chama hiki wabaki waaminifu katika malengo yao.  Leo hii kuliko hapo awali kunahitajika kujenga ulimwengu, jamii ya uhusiano wa kidugu na uliojaa maisha. Kwa sababu vitendo vinavyotokana na umoja ambao unainamia zaidi kuelekea mwingine kwa kumfikiria mwenye thamani,  hadhi, mpendwa na mzuri mbali na  mwili na maadili. Upendo wa mwingine kwa maana hiyo unatusukuma kutafuta upendo wa maisha yake. Ni kwa kukukuza namna hiyo tu uhusiano wa kuwezesha urafiki kijamii ambao haubagui yoyote na udugu unaufungulia wote. Papa amewaalika kwa maana hiyo kuwa mashuhuda  wa huruma, na wema wa Mungu. Katika ujumbe wake alioukabidhi kwao anahitimisha akiwakabidhi kwa Bikira Maria familia zao na kuwabariki wote na baraka takatifu.

21 May 2021, 16:28