Tafuta

Vatican News
 Papa ametuma ujumbe kwa njia ya video katika Mkutano wa 5 wa kimataifa kuhusu Kuchunguza Akili, Mwili na Roho. Papa ametuma ujumbe kwa njia ya video katika Mkutano wa 5 wa kimataifa kuhusu Kuchunguza Akili, Mwili na Roho. 

Papa:Mwili,akili na roho havitengani&mifumo ya afya bila ubaguzi!

Katika ujumbe kwa njia ya video kwa washiriki wa mkutano wa kimtaifa kwa njia ya mtandao ukiongozwa na mada ya “Kuchunguza Akili,Mwili na Roho”,Papa anashukuru sayansi ya matibabu,utafiti wa hali ya juu zaidi na matibabu ya kutosha,lakini kuna maswali ya kimaadili ya kujiuliza kama suala la udanganyifu wa jenomu ya kibinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa ametoa ujumbe kwa njia ya video uliofunga mkutano wa V wa kimataifa kwa njia ya mtandao ulikuwa unaongozwa na kauli mbiu: “Kuchunguza Akili, Mwili na Roho”, ambao umeandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni, Taasisi ya Huduma na Mfuko wa Sayansi na Imani na Shina la Maisha.  Papa Francisko ameshukuru awali ya yote aliyechagua kama jitihada binafsi, kitaaluma kutubu wagonjwa na kuwasiaidia wahitaji zaidi kwa namna ya pekee wanaojikita bila kuchoka kupambana na janga, ambalo haliishi kuongeza wathiwa wengi na wakati huo huo kuweka majaribu katika maana yetu ya mshikamano na udugu.

Mkutano huo ulianza yarehe 6 na ambao kwa siku tatu umeweza kuwaona madaktari, wanasayansi, wasomi wa maadili, viongozi wa dini, watunga sera, wafadhili ili kujadili uvumbuzi wa hivi karibuni katika dawa, huduma ya afya na kinga, pamoja na athari za kiutamaduni wa maendeleo ya kiteknolojia, pia wakichunguza uhusiano kati ya akili, mwili na roho. Papa Francisko amesema ni hasa kutoka akili, mwili na roho, dhana ya utatu inayodhaniwa na Mababa wengi wa Kanisa na baadaye wanafikra mbali mbali wa kisasa, ambao Papa katika tafakari yake amejikita  kwa kutazama hali ya sasa na kwamba: Kufikiria na kuweka mtu katikati pia inahitaji kutafakari juu ya mifano ya mifumo ya afya iliyopaswa kufunguliwa kwa wagonjwa wote, bila tofauti yoyote”.

Maendeleo ya maarifa na maswali ya kimaadili

Katika hotuba yake kwa njia ya video, Papa pia anapongeza sayansi ya kisasa ya matibabu ambayo, bila shaka imefungua mbele yetu upeo wa maarifa na maingiliano ambayo karne chache zilizopita hata hayakuweza kufikiria. Haya ni maendeleo katika maarifa ya kweli ambayo yametafsiriwa na na kuanzishwa katika utafiti wa kisasa zaidi na matibabu ya kutosha na sahihi zaidi. Mfano juu ya yote ni uwanja mkubwa wa utafiti katika uwanja wa maumbile, unaolenga kushinda magonjwa mbali mbali. Utafiti huu, hata hivyo, amebainisha Papa, huibua pia maswali msingi ya anthropolojia na maadili, kwa mfano, suala la kudanganywa kwa jenomu ya kibinadamu ili kudhibiti au hata kushinda mchakato wa kuzeeka, au kufikia kuboreshwa binadamu.

Mwili, akili, roho” vinaunganishwa kwa kina kutoweza kutenganishwa

Binadamu ambaye, hatupaswi kusahau, ameundwa na mwili, akili, roho. Ni makundi matatu, ambayo hayafanani na maono ya Kikristo ya kawaida, ambaye mfano wake ni ule wa mtu, anayeeleweka kama umoja usioweza kutenganishwa wa mwili na roho, ambaye pia, amepewa akili na utashi”, Papa amefafanua. Maono haya sio ya kipekee, ameelezea Papa,  kwa sababu, vipimo kadhaa vya uhai wetu, leo  hii mara nyingi hutenganishwa, na ambavyo kiukweli hufanya uhusiano mkubwa na usioweza kutenganishwa kati yao. Tafakari ya Papa imejikita kwenye misingi ya uwepo wa mwanadamu, kuanzia safu yake ya kibaolojia ambayo inajidhihirisha kupitia mwili wetu na hufanya mwelekeo wa haraka zaidi, lakini sio rahisi kuelewa. Sisi sio roho iliyo safi, Papa Francisko anasema,  kuwa  kwa kila mmoja wetu, kila kitu huanzia na mwili wetu, lakini sio tu hilo , kwani tangu kutungwa hadi kufa hatuna mwili tu, lakini sisi ni mwili na imani Kikristo inatuambia kwamba tutakuwa pia katika ufufuko ”.

Matukio ya kibinadamu zaidi ya mali ya mwili

Papa ameenfdelea kufafanua kuwa maana hii msingi ni mwelekeo wa akili ambao hufanya hali ya uwezekano wa kujielewa kwetu. Kwa sasa, Papa  amebainisha,  kuwa mara nyingi kuna tabia ya kutambua eneo hili muhimu na ubongo na michakato yake ya neva. Walakini, licha ya kusisitiza umuhimu wa sehemu ya kibaolojia na unaofanya kazi ya ubongo, na sio tu hata hivyo,  kiini kinachoweza kuelezea matukio yote yanayotufafanua kama wanadamu, ambayo mengi hayawezi 'kupimika' na, kwa hivyo, huenda zaidi ya mali ya mwili. Kwa hakika mwanadamu hawezi kumiliki akili bila jambo la ubongo; lakini, wakati huo huo, akili yake haiwezi kupunguzwa kwa utajiri tu wa ubongo wake. Huu ni mlingano wa kufuata.

Matumizi ya neno akili katika nyanja ya kisayansi huongeza shida nyingine, amesisitiza Papa Francisko. Katika neno akili kwa kawaida huoneshwa ugumu wa vitengo vya kibinadamu, hasa kuhusiana na malezi ya mawazo. Kwa maana hiyo swali kuhusu asili ya vitengo vya kibinadamu ni kama unyeti wa maadili ya mtu, huruma, upendo wa mshikamano ambao hutafsiri kuwa ishara za uhisani na kujitoa kwa wengine, na zaidi ni ya sasa, au hisia ya urembo, bila kuzungumzia utafutaji usio na  mwisho wa aliye juu.

Roho katika tamaduni na dini hutoka nje na kutazama mlango wa upeo.

Hivi ndivyo tafakari juu ya mwelekeo katika sehemu hizi tatu unafungua kuhusu  roho.  Hili pia ni neno ambalo limechukua maana tofauti katika tamaduni na dini mbali mbali. Biblia hasa, tafakari ya kifalsafa-kitaalimungu na dhana ya roho , kinyume chake  inafafanua upekee wa kibinadamu, ikiwa na maana wa mtu asiyeweza kupunguzwa kwa aina yoyote ya kiumbe hai, pamoja na ufunguzi wake kuelekea hali isiyo ya kawaida na kwa hiyo, kwa Mungu, Papa amefafanua.  Uwazi huu kwa aliye juu zaidi, kwa kitu kikubwa zaidi kuliko nafsi, kwa mujibu wa Papa Francisko ni ya kisheria na inashuhudia thamani isiyo na kikomo ya kila mtu. Kwa maana hiyo, roho inapaswa kueleweka kama dirisha, ambalo hutoka nje na kutazama mlango kuelekea upeo wa juu.

08 May 2021, 17:47