Tafuta

Vatican News
2021.05.23 Misa ya Siku Kuu ya Pentekoste 2021.05.23 Misa ya Siku Kuu ya Pentekoste  (Vatican Media)

Papa Francisko Kanisa sio shirika la kibinadamu ni hekalu la Roho Mtakatifu

Papa katika Misa ya Siku kuu ya Pentekoste,ametoa ushauri wa aina tatu:Roho Mtakatifu anaishi katika wakati uliopo:Roho msaidizi ni kutafuta kwa pamoja na kumweka Mungu mbele kabla ya umimi.Kanisa sio shirika la kibinadamu,ni hekalu la Roho Mtakatifu.Yesu alileta moto wa Roho duniani na Kanisa linabadilishwa na upako wa neema,kwa nguvu ya maombi,furaha ya utume, na uzuri wa umaskini usio na ulinzi.Tumuweke Mungu mbele.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika siku kuu ya Pentekoste, ambayo imefanyika Jumapili tarehe 23 Mei 2021, Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Misa Takakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akianza mahubiri baada ya Injili iliyosomwa amesema kuwa “Atakuja huyo Msaidizi, nitakaye wapelekea kutoka kwa Baba, (Yh 15,26). Kwa maneno hayo Yesu alitoa ahadi  ya Roho Mtakatifu kwa Mitume zawadi ya mwisho, yaani zawadi ya zawadi. Alizungumza kwa kutumia kielelezo maalum na fumbo yaani Msaidizi. Tupokee maneno hayo yasiyo rahisi kutafsiri kutokana na yalivyo maana kuu. Msaidizi kimsingi ina maana ya kusema mambo mawili mfariji na mwakiri. Papa Francisko amefafanua kuwa, Msaidizi ni Mfariji.  Sisi sote hasa wakati mgumu kama ule ambao tunaoishi, tunajaribu kutafuta faraja. Lakini mara nyingi tunaishia kwenye faraja za kidunia ambazo zinapotea haraka. Yesu leo hii anatupatia faraja kutoka mbinguni, Roho, mfariji kamili.  Je kuna utofauti gani? Faraja za ulimwengu ni kama ganzi. Inakupatia faraja ya muda tu, lakini haiponeshi ugonjwa wa ndani ambao tunaubeba ndani mwetu. Inakuondolea, inafadhaisha, lakini haikuponeshi. Inafanya kazi kiujuu juu tu kwa ngazi za hisia na siyo katika moyo. Kwa sababu ni yule tu anayetufanya tuhisi tumependwa namna tulivyo na  anatoa amani ya moyo. Roho Mtakatifu, roho wa upendo anatufanya hivyo, kwani anashuka ndani kama roho na kutenda katika roho zetu. Anatembea ndani ya moyo kama mgeni mtamu wa Roho. Ni huruma nyenyewe ya Mungu  ambaye hatuachi peke yetu kwa sababu kukaa na yule aliye na upweke tayari ni kufariji. Papa Francisko ameshuri kuwa ikiwa unahisi giza la upweke, ikiwa unabeba ndani mzigo mzito unasonga matumaini, ikiwa unao moyo uliojeruhiwa ambao unachoma, ikiwa hupati njia ya kutoka,  basi jifungulie Roho Mtakatifu. Mtakatifu Bonaventura alisema kuwa mahali palipo na mahangaiko analeta faraja na siyo jinsi ambavyo Dunia inafanya kwamba katika matarajio inafariji  lakini wakati mgumu inakucheka na kukuhukumu. Ndivyo Dunia inafanya, hivyo hasa adui wa roho, shetani. Kwanza anakudanganya na kukufanya kama mshindi na  anakutupa chini na kukufanya ukosee. Anafanya kila njia ili akuangushe chini, wakati Roho Mfufuka anataka kukuinua.

Papa wakati wa kuhubiri
Papa wakati wa kuhubiri

Papa Francisko kwa kutoa mfano amesema tuwatazame mitume. Wao walikuwa peke yao na wanahaangaika, na milango yao ikiwa imefungwa, walikuwa na wasi wasi na mbele ya macho yao walikuwa na udhaifu na kushindwa kwao. Miaka iliyopita wakiwa na Yesu, haikuwabadilisha, Baadaye wakapokea Roho na yote hayo yakabadilika. Matatizo,sirika zenyewe hazikubalika, lakini hawakuogopa tena na wala hawakuogopa hata kutendewa mabaya. Walisikia kufarijika ndani na waltaka sasa kwenda kutafuta faraja ya Mungu. Kwanza walikuwa wanaogopa na sasa hawaogopi tena kushuhudia upendo walioupokea. Yesu alikuwa ametabiri kwao kuwa Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami. (Yh 15, 26-27). Hata sisi tumealikwa kushuhudia katika roho Mtakatifu, kageuka kuwa wasaidizi na wafariji. Ndio, Roho anatuomba kutoa mwili katika faraja. Je kwa namna gani? Si kwa kutoa hotuba ndefu, lakini kwa kujifanya kuwa karibu; si kwa maneno makali, bali kwa sala na ukaribu. Msaidizi anasema kwa Kanisa ambalo leo hii la wakati wa kufariji. Ni kipindi cha kutangaza Injili zaidi ya kupambana upagani. Ni wakati wa kupeleka furaha ya Mfufuka. Si wakati wa kulalamika juu ya balaa za ulimwengu. Ni kipindi cha kutoa upendo katika ulimwengu, bila kuolewa na malimwengu. Ni kipindi ambacho nicha kutoa shuhuda za huruma zaidi kuliko kutunga sheria kubwa, ni kipindi cha Msaidizi.

Msaidizi na baadaye mwakiri. Papa Francisko akifafanua kuhusu mwakiri kwamba katika mantiki ya historia ya Yesu, mwakiri hakuwa anafanya kazi kama anavyofanya leo hii. Badala ya kuzungumza kwa niaba ya mtuhumiwa, Yeye alikuwa kawaida karibu naye, akimpa ushauri kupitia sikioni nini aweze kusema kwa kujitetea. Na ndivyo anafanya hivyo msaidizi, Roho wa kweli ambaye hajiweki nafasi yake bali anatulinda dhidi ya ubaya na kutuongoza katika mawazo na hisia. Anafanya hivyo kwa utaratibu na kujali, bila kutulazimisha; anapendekeza lakini halazimishi. Roho mbaya, anafanya kinyume; anatafuta kutubamiza, anataka kutufanya tuamini  kuwa tunalazimishwa kuamini maelekezo mabaya na hata mazoea mabaya. Tujaribu kwa maana hiyo kupokea ushauri wa aina tatu wa msaidizi na mwakiri wetu. Ni njia tatu msingi dhidi ya vishawishi ambavyo leo hii vimeenea, Papa amebainisha. Ushauri wa kwanza wa Roho Mtakatifu ni kwamba Roho anaishi katika wakati uliopo. Wakati uliopo sio wakati uliopita au wakati ujao. Msaidizi anathibitisha msingi leo hii dhidi ya vishawishi vya kutufanya kugandamana na machungu ya wakati uliopita, au kusimamia juu ya ukosefu wa uhakika wa kesho na kutuacha tukiwa na hofu za  ndani mwetu za wakati ujao.  Roho mwakiri anatukukumbusha neema ya wakati uliopo.

Waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro

Hakuna muda ulio bora  zaidi kwa ajili yetu wa sasa, mahali tulipo, ni wakati muafaka usiorudiwa ili kutenda mema, ili kufanya maisha yawe zawadi. Tuishi wakati uliopo. Papa Francisko amesema ushauri wa pili wa Roho ya msaidizi, ni kutafuta kwa pamoja. Kutafuta pamoja si katika upande. Roho haumbi mtu aliyefungwa, lakini anatufanya kama Kanisa katika karama zilizo nyingi, umoja ambao siyo unaofafanana. Msaidizi anathibitisha ule ukuu wa kuwa pamoja. Kwa kuwa pamoja kwenye jumuiya ya Roho ambaye inaendelea na kutuumba na kuleta mapya.  Bustani ya Mitume.  Walikuwa ni tofauti, kati yao kwa mfano kulikuwa na Mateo mtoza ushuru ambaye alikuwa anashirikiana na Warumi, Simoni Zeloti ambaye alikuwa anapinga. Kulikuwa na mawazo ya kisiasa tofauti, maono ya ulimwengu tofauti.  Lakini walipopokea Roho walijifunza wasitoe umuhimu wa mtazamo wao wa kibinadami, bali upamoja wa Mungu. Leo, ikiwa tunamsikiliza Roho, hatutazingatia wenye misimamo mikali, wanajadi na wazushi, kulia na kushoto na ikiwa hivi ndivyo vigezo, basi inamaanisha kuwa Roho amesahauliwa Kanisani. Msaidizi anatia msukumo wa umoja na maelewano katika utofauti. Anatuonesha sehemu za Mwili uleule, wa kuwa kaka na dada kati yetu. Tutafute umoja.

Mwonekano wa ndani
Mwonekano wa ndani

Na hatimaye Papa Francisko ametoa ushauri wa tatu mkubwa na kusema ni kumweka Mungu mbele kabla ya umimi.  Ni hatua yenye msimamo wa maisha ya kiroho, ambayo siyo mkusanyiko wa mastahili au wa matendo yetu, lakini ni unyenyekevu wa ukarimu wa Mungu. Msaidizi athibitisha ukuu wa neema. Ni pale ambao tunajikung’uka kuondokana na mimi wetu na kumwachia Bwana; ni pale tu ambapo tutakapomwamini  Yeye ndipo tutajipata sisi wenyewe; ni pale tu tukiwa maskini wa Roho tutakuwa matajiri wa Roho Mtakatifu. Inastahili hata kwa Kanisa.  Hatuwezi kuokoa yoyote na wala sisi wenyewe kwa nguvu zetu binafsi. Ikiwa nafasi ya kwanza tunaweka mipango yetu: “ mipango yetu ya mageuzi itaishia kwa utendaji tu, kwa ufanisi, katika usawa na hatutazaa matunda. Kanisa sio shirika la kibinadamu, ni hekalu la Roho Mtakatifu. Yesu alileta moto wa Roho duniani na Kanisa linabadilishwa na upako wa neema, kwa nguvu ya maombi na furaha ya utume, na uzuri wa umaskini usio na silaha. Tumtangulize Mungu mbele! Kwa kuhitimisha Papa amesema, Roho Mtakatifu, faraja ya mioyo yetu.Tufanye wamisionari wa “faraja yako, wasaidizi wa huruma katika ulimwengu. Wakiri wetu, mshauri mwema wa  roho, utufanye kuwa mashuhuda wa Mungu wa leo, manabii wa umoja kwa Kanisa na ubinadamu, mitume wanaojengwa juu ya neema yako, ambayo huunda kila kitu na inasasisha kila kitu kuwa kipya”.

23 May 2021, 11:50