Tafuta

Vatican News
Kukaribisha maisha mapya Kukaribisha maisha mapya  

Papa Francisko atafungua Mkutano kuhusu upungufu wa watu Italia

Tarehe 14 Mei Papa atakuwa katika Ukumbi wa wa Conciliazione,Roma kuzindua mkutano unaojikita na masuala ya shida ya kupungua kwa idadi ya watu nchini Italia na ulimwenguni,ulioitishwa na rais wa Jukwaa la vyama vya familia Bwana Gigi De Palo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 3 Mei 2021, Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Bruni ametoa taarifa kwa waandishi wa habari kuwa tarehe 14 Mei ijayo, Baba Mtakatifu Francisko atazindua mkutano unaojikita na masuala ya shida ya kupungua kwa idadi ya watu nchini Italia na ulimwenguni, ambao sehemu ya watu watafuatilia  kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na Jukwaa la Vyama vya kifamilia. Baada ya hotuba yake, inayotarajiwa kufanyika  majara ya asubuhi saa 3.30 hivi katika Ukumbi mkubwa ulioko njia ya Conciliazione Roma, Papa atarudi nyumbani kwake Vatican.

Katika taarifa ya waandaaji Bwana Gigi De Palo Rais wa Jukwaa la vyama vya familia amesdema kuwa hili ni toleo la kwanza la Hali halisi kwa ujumla kuhusiana na kuzaliwa na kukuza wakati uliopo ili kufikiria juu ya siku zijazo, katika muktadha wa mgogoro wa upungufu wa watu nchini Italia. Ni mkutano wa aina yake ili kuangazia wakati ujao na kuzindua wito wa wajibikaji wa kuanza tena kuzaliwa kwa watoto nchini Italia.

Ni mada ambayo itahusu muktadha wa hali halisi zaidi na athari kubwa za janga, ambalo limepelekea familia zaidi ya milioni moja kuwa maskini zaidi nchini. Kwa zaidi ya muongo mmoja,  amesema rais huyo Italia imekuwa nchi inayozeeka zaidi na isiyo na watu wengi, ikikabiliwa na kasoro za kimuundo na sheria katika kiwango cha kifedha, kiuchumi na kijamii na ambapo sasa inapitiwa hadi kukosekana kwa watoto. Yote haya, ni mbele ya fursa isiyowezekana na ambayo imewakilishwa na Mpango wa Kitaifa wa Kurejesha na Kuhimili (PNRR), ulioyokabidhiwa hivi sasa  na serikali ya Italia, kwa agizo la Bunge, kwa Jumuiya ya Ulaya.

03 May 2021, 15:40