Tafuta

Vatican News
Msaada nchini India unahitajika dhidi ya maambukizi ya Covid-19 Msaada nchini India unahitajika dhidi ya maambukizi ya Covid-19  (AFP or licensors)

Papa Francisko anasali kwa jili ya India kwa sababu ya Covid

Papa Francisko ametuma ujumbe mrefu kwa Kardinali Oswald Gracias, Askofu Mkuu wa Bombay na Rais wa Maaskofu wa India akisali kwa ajili ya waathirika na kuombe wagonjwa,falimia zao,madaktati na watoa huduma wote ili wahifdhi nguvu na amani.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican.

Moto unaoneonekana kuwaka ambao unachoma maiti kwa machozi ya nchi ambayo imeshindwa kuendelea mbele kutokana na maambukizi mengi ya kasi ya virusi. Vifo elfu nne kila siku, na maambukizi elfu 380 katika masaa 24 yaliyopita ambayo, ndivyo hali inavyoendelea mbele ikimaanisha ni milioni ya kesi ya maambuki kwa mwezi. Ndivyo ilivyo India inayo shika rekodi mbaya za janga ambalo wanaendelea na mapambano  dhidi ya kuenea kwa Covid na idadi kubwa ya rasilimali za kiuchumi karibia dola bilioni 7 ambazo  zimetengwa kwa ajili ya  chanjo na huduma za afya.

Mshikamano wa Papa

Ni hali ambayo inaibuka kuptia vyombo vya  habari na ambavyo vimemsukama  Papa kuelezea hisia zake kwa kuandikia watu wa nchi kubwa ya bara la Asia na kwa Kanisa lake.  Papa ameandika: “ Wakati huu ambapo watu wengi nchini India wanakabiliwa na dharura ya sasa ya kiafya, ninaandika kuonesha mshikamano wangu wa dhati na ukaribu wa kiroho kwa watu wote”. Mpokeaji wa ujumbe huo mrefu ni Kardinali Oswald Gracias, askofu mkuu wa Bombay na rais wa Baraza la maaskofu wa eneo hilo.

Sala ya Papa

Papa Francisko ametaka kukumbuka mtu yeyote ambaye ameona njia yake ilipitiwa na virusi vya Corona: “Mawazo yangu yanwaendela zaidi ya yote kwa wagonjwa na familia zao, kwa wale wanaowasaidia, na hasa kwa wale ambao wanaomboleza kufiwa na wapendwa wao. Ninafikiria pia juu ya madaktari wengi, wauguzi, wafanyakazi wa hospitali, madereva wa magari ya wagonjwa na wale wanaofanya kazi bila kuchoka ili kujibu dharura za kaka na dada zao. Kwa shukrani kubwa ninaombea wote zawadi za Mungu ya uvumilivu, nguvu na amani”.

Kanisa liko mstari wa mbele

Kwa ajili ya Jumuiya Katoliki ya India, Papa Francisko ametoa maneno ya shukrani kwa kazi upendo na mshikamano uliofanywa kwa ajili ya huduma ya wote. Papa amesisitizia, juu ya ukarimu uliooneshwa na vijana wengi waliojitolea na amehitimisha ujumbe wake kwa kupendekeza kuwa na huruma ya kimungu kwa waamini wote ambao wamepoteza maisha yao, miongoni mwao wakiwemo hata makuhani, wanaume na watawa wa kike. Katika siku hizi za uchungu mkubwa Papa amesema  kwamba wote tunaweza kufarijiwa na tumaini linalotokana na Pasaka na imani yetu isiyotetereka katika ahadi ya ufufuko na ya maisha mapya ya Kristo.

06 May 2021, 19:32