Tafuta

Vatican News
 Bikira Maria wa Lujan nchini Argentina Bikira Maria wa Lujan nchini Argentina  

Papa Francisko ametuma ujumbe katika fursa ya sala ya Rosari kwa Mama wa Lujan

Katika ujumbe kwa njia ya Video Papa amewaelekeza maaskofu ambao watakutana katika Madhabahu ya Mama Yetu wa Lujan katika fursa ya sala ya Rosari na Misa ili kuombea afya ya watu wa Argentina.Ni fursa ambayo inakumbusha yote yaliyotendwa na Bikira katika nchi yao.Papa anawambie wafanye kumbukumbu inayohakikisha usalama wa wakati ujao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko tarehe 6 Mei 2021, ametuma ujumbe kwake kwa njia ya video katika fursa ya kusali Rosari kwa ajili ya afya ya watu wa Argentina. Katika ujumbe wake Papa anasema Mwezi wa Mei, Mwezi wa Maria, 8 Mei natazama Lujan kwa maana ya kutazama mama Mawa wa Lujan. Papa Francisko katika ujumbe huo anasema: “Ninatamani kuwa nanyi karibu tarehe 7 katika mkesha ambapo ninyi maaskofu mtaungana pamoja ili kusali Rosari kwa ajili ya afya ya watu wa Argentina. Kutoka hapa ninawasindikiza. Na hata Jumamosi tarehe 8 wakati mtakuwa mbashara ili kusali Rosari katika Madhabahu itakayofanyika huko saa 7.00 mchana na saa 1.00 jioni kwa ajili ya misa ya kubadili vazi.  Katika misa hiyo mtakuwa mmeunganika ili kuanza kuandaa pamoja mchakato wa miaka tisa ya kufikia 2030 ili kuweza kuadhimisha miaka 400 tangu tokeo muujiza”.

Kukumbuka mambo makuu yaliyotendwa na mama Maria, Argentina

Papa Francisko amesisitiza kuwa “Ni safari ndefu, lakini ambayo inapita kwa haraka, japokuwa inahitaji kuifanya. Ni safari ya kumbu kumbu, yaani  kumbu ya kile ambacho Bikira alifanya hapo na  anataka kubaki hapo. Safari ya kumbu kumbu ya miaka mingi na miaka ya hija, ya kutafuta, ya miujiza, ya wana na mabinti ambao wanatembea kwa ajili ya kumwona mama. Mkutano huo wa kumbu kumbu uweze kuwa kwenu kiongozi, kwa sababu kumbu kumbu ya nguvu iweze kuhakikisha wakati ujao salama. Mwachie yeye awasindikize na kumsindikiza katika safari yake. Bwana awabariki wote na Bikira awalindi. Na tafadhali msisahau kusali kwa ajili yangu. Asante”, amehitimisha ujumbe wake kwa njia ya video.

06 May 2021, 16:30