Tafuta

Papa:Fedha ziwe za watu na maskini wasilipe gharama za madhara ya mfumo huo!

Katika Ujumbe kwa njia ta video wa Mtandao wa kimataifa wa sala kwa nia za mwezi Mei 2021,Papa Francisko anaomba wasali ili wahusika wa ulimwengu wa kifedha washirikiane na serikali kwa ajili ya kithibiti masoko ya kifedha na kulinda raia wao wadhaifu dhidi ya hatari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Nia za Baba Mtakatifu kwa Mwezi Mei 2021 zinahusu ulimwegu wa kifedha ambapo katika ujumbe kwa njia ya video ulioandaliwa na Mtandao wa Kimataifa kwa ajili ya nia za kila mwezi, Papa anasema:

“Wakati uchumi wa kweli ambao unatengeneza ajira upo katikati ya kipeo cha mgogoro, ni watu wangapi wasiokuwa na ajira! Lakini masoko ya fedha hayajawahi kuongezeka zaidi kama yalivyo sasa.

Jinsi gani ulimwengu wa fedha ulivyo mbali na sehemu kubwa ya maisha ya watu wa kawaida! Ikiwa fedha haijasimamiwa, inakuwa uvumi ulio safi unaoongozwa na sera za kifedha. Hali hii si endelevu. Ni hatari.

Ili kuzuia maskini wasirudi kulipa gharama za madhara ya mfumo huo, ni lazima kudhibiti kwa uangalifu ubahatishaji wa kifedha.Ninataka kulitilia mkazo neno hili: Kubahatisha.

Fedha iwe chombo cha kuhudumia watu na kuwatunza

Papa anakazia zaidi na kusesema: "Fedha iwe chombo cha huduma, chombo kwa ajili ya kuwahudumia watu na kuwatunza katika nyumba yetu ya pamoja! Bado tunao muda wa kuanza mchakato huu wa kuleta mabadiliko ya ulimwenguni ili kujikita kwenye matendo ya dhati ya kufanya uchumi tofauti, ambao ni wa haki, jumuishi na ambao hauachi mtu yoyote nyuma.

Tunaweza kulifanya hili! Na tuombe ili wale walio na jukumu la kifedha ulimwenguni washirikiane na serikali kudhibiti eneo la fedha na kuwalinda raia wadhaifu dhidi ya hatari zake".

 

04 May 2021, 16:22