Tafuta

Papa azindua kwa upya wito wa kusali Rosari

Mara baada ya Katekesi ya Jumatano,Papa Francisko amekumbusha sala kwa Mama Maria tarehe 8 Mei katika Madhabahu ya Pompei na kwa upya amewaalika waamini wote kuungana pamoja katika mpango wa sala kila siku kwa ajili ya mwezi wa Mei ambao unajumuisha madhabahu 30 ya Mama Maria Ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko mara baada ya katekesi, yake Jumatato tarehe 5 Mei 2021 amerudia kwa upya kutoa mwaliko wa kuungana pamoja katika sala ya Rosari ambapo  kila siku katika madhabahu ya ulimwengu wanasali Rosari Takatikafu.

“Kwa kuongozwa na madhabahu yaliyoko umwelinguni katika mwezi Mei, tusali Rosari kwa ajili ya kuomba kuisha janga, na kuanza kwa upya shughuli za kijamii na kazi”. Aidha amesema Papa “ Leo madhabahu ya Bikira mwenyeheri wa Rosari wa Namyang, nchini Korea Kusini yanaongaza sala ya Maria. Tuungane na wale ambao wamekusanyika katka madhagai hio wakusali hasa kwa ajili ya watoto na vijana barubaru.

Papa Francisko amewasalimu waamini wa lugha ya kiitaliano ambao amekumbusha sala kwa mwezi wa Mei. Amewashauri kusali Rosari na kwamba  Bikira Maria anaheshimiwa sana. Kufuatia na hiyo amewakumbusha kuungana kiroho katika maombi kwa Mama wa Rosari itakayofanyika Jumamosi tarehe 8 Mei saa sita kamili katika madhabahu ya Pompei, Italia.

Kama kawaida Papa wazo lake limewaendeea wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Wasali kwa Maria mfano wa imani na ushuhuda wa kazi katika Neno la Kristo ili kupata nguvu ya kikristo katika chaguzi na katika matatizo ya maisha.

05 May 2021, 16:18