Tafuta

Vatican News
2021.04.30 Kanisa la Kiorthodox la Yerusalem 2021.04.30 Kanisa la Kiorthodox la Yerusalem 

Nchi Takatifu:Papa ameomba Kanisa zima kusali kwa ajili ya amani

Papa Francisko amewaalika wachungaji wote ulimwenguni kuunganisha sala zao katika Mkesha wa Pentekoste utakaodhimishwa katika Kanisa la Mtakatifu Stefano Yerusalemu.

VATICAN NEWS

Kanisa la ulimwengu linaunganika katika mkesha wa Petekoste huko Yerusalemu. Huo ndiyo wito wa Papa Francisko ambao Ijumaa tarehe 21 Mei 2021, amesema mara baada ya hotuba yake kwa mabalozi wapya wasio wakazi ambao wamewakilisha  barua zao za utambulisho kwa Papa jijini Vatican. Papa Francisko kwa maana hiyo amewaaalika makanisa yote ulimwenguni kusali na kuomba amani kwa ajili ya  nchi Takatifu, kwa kuungana katika madhimisho ambayo yameandaliwa na wakatoliki katika Nchi Takatifu.

Papa amesema kuwa: “Kila Jumuiya ifanye sala kuomba Roho Mtakafu ili Waisraeli na Wapalestina waweze kupata njia ya mazungumzo na msamaha, wavumilie na wawe wajenzi wa amani, na haki, kwa kujifunguali hatua kwa hatua ya matumaini ya pamoja na kuishi kama ndugu”. Haya ni maneno ambayo pia yanakumbusha wito wa amani katika nchi Takatifu ambao aliutoa mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, siku ya  Jumapili tarehe 16 Mei 2021.

 

21 May 2021, 16:21