Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ameridhia Nyongeza Kwenye Litani ya Mtakatifu Yosefu kwa kutambua mchango wake katika ulinzi na huduma kwa Mtoto Yesu; Msaada kwa wenye shida na ulinzi kwa maskini. Baba Mtakatifu Francisko ameridhia Nyongeza Kwenye Litani ya Mtakatifu Yosefu kwa kutambua mchango wake katika ulinzi na huduma kwa Mtoto Yesu; Msaada kwa wenye shida na ulinzi kwa maskini. 

Mwaka wa Mtakatifu Yosefu: Nyongeza ya Litania ya Mt. Yosefu

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia mabadiliko ya Nyongeza Katika Litania ya Mtakatifu Yosefu, yaliyowasilishwa kwake na Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa! Mlinzi wa Mkombozi, Mhudumu wa Kristo, Mlinzi wa afya, Msaada wa wenye shida, Mlinzi wa wakimbizi, Mlinzi wa wenye shida na Mlinzi wa maskini. Marais wa Mabaraza ya Maaskofu wanafanya kazi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Maadhimisho ya Mwaka wa Mtakatifu Yosefu yalizinduliwa tarehe 8 Desemba 2020 na yanatarajiwa kufungwa rasmi kwa kudema hapo tarehe 8 Desemba 2021. Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa Kitume “Patris Corde” yaani “Kwa Moyo wa Kibaba”: “Mwaka wa Mtakatifu Yosefu, Kumbukumbu ya Miaka 150 Tangu Mtakatifu Yosefu alipotangazwa Kuwa Msimamizi wa Kanisa la kiulimwengu” anataja sifa kuu za Mtakatifu Yosefu akisema kwamba ni: “Baba mpendevu, mwenye huruma na mapendo; mtiifu na mwepesi kukubali. Ni Baba aliyebahatika kuwa na kipaji cha ugunduzi na ujasiri, lakini alibaki akiwa amefichwa kwenye vivuli, akawajibika na kuwa ni chanzo cha furaha na sadaka binafsi katika maisha.

Katika moyo wa unyenyekevu, Mtakatifu Yosefu aliyahifadhi mafumbo yote ya maisha yaliyomzunguka Mtoto Yesu na Mama yake Bikira Maria. Mtakatifu Yosefu mtu wa busara na haki, alijiaminisha mbele ya Mwenyezi Mungu na kuyatekeleza yale yote aliyoambiwa na Malaika katika ndoto. Lengo la maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu Yosefu anasema Baba Mtakatifu, ni kuwasaidia waamini kumfahamu na kumpenda Mtakatifu Yosefu aliyekuwa na mang’amuzi ya kibinadamu kama walivyo waamini wengi duniani. Ni Mtakatifu ambaye hakushtushwa sana na mambo, hakuwa na karama maalum wala kati ya watu wa nyakati zake, hakuwa mtu mashuhuri. Na wala Maandiko Matakatifu hayaoneshi maneno yaliyotoka kinywani mwake hata kidogo, lakini machoni pa Mwenyezi Mungu, aliweza kutenda matendo makuuu katika maisha na utume wake.

Mtakatifu Yohane Paulo II katika Waraka wake wa Kitume, “Redemptoris custos”, yaani “Mlinzi wa Mkombozi” uliochapishwa kunako tarehe 15 Agosti 1989 anamtaja Mtakatifu Yosefu kuwa ni Mlinzi wa Mkombozi na Familia Takatifu. Mtakatifu Yosefu alikuwa ni mtu mwenye imani thabiti, aliyejiaminisha mbele ya Mwenyezi Mungu. Mwanadamu anapomweka Mungu pembeni mwa mipango na vipaumbele vya maisha yake, matokeo ni kutumbukia katika majanga yanayodhalilisha utu, heshima na haki msingi za binadamu. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko ameiridhia mabadiliko ya Nyongeza Katika Litania ya Mtakatifu Yosefu, yaliyowasilishwa kwake na Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa!

Tayari mabadiliko haya yamekwisha kutumwa kwa Marais wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki sehemu mbalimbali za dunia, ili yaweze kuingizwa katika Litania ya Mtakatifu Yosefu kwa kuzingatia maana. Mlinzi wa Mkombozi, Mhudumu wa Kristo, Mlinzi wa afya, Msaada wa wenye shida, Mlinzi wa wakimbizi, Mlinzi wa wenye shida na Mlinzi wa maskini.

Litania ya Mtakatifu Yosefu

Bwana utuhurumie - Bwana utuhurumie

Kristo Utuhurumie - Kristo Utuhurumie

Bwana utuhurumie - Bwana utuhurumie

Kristo utusikie - Kristo utusikilize

Bwana wa Mbinguni, Mungu - utuhurumie

Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu - utuhurumie

Roho Mtakatifu, Mungu mmoja - utuhurumie

Utatu Mtakatifu - utuhurumie

Maria Mtakatifu - utuombee

Yosefu Mtakatifu - utuombee

Mzao bora wa Daudi - utuombee

Mwanga bora wa Mababu - utuombee

Mume wa Mzazi wa Mungu - utuombee

Mlinzi wa Mkombozi - utuombee

Mlinzi safi wa Bikira - utuombee

Mlishi wa Mwana wa Mungu - utuombee

Mkingaji mwaminifu wa Kristo - utuombee

Mhudumu wa Kristo - utuombee

Mlinzi wa afya - utuombee

Mkubwa wa jamaa takatifu - utuombee

Yosefu mwenye haki - utuombee

Yosefu mwenye usafi wa Moyo - utuombee

Yosefu mwenye utaratibu - utuombee

Yosefu hodari kabisa - utuombee

Yosefu mtiifu kabisa - utuombee

Yosefu mwaminifu kabisa - utuombee

Kioo cha uvumilivu - utuombee

Mpenda umaskini - utuombee

Mfano wa watu wa kazi - utuombee

Uzuri wa mwendo wa nyumbani - utuombee

Mlinzi wa Mabikira - utuombee

Tegemeo la jamaa - utuombee

Msaada wa wenye shida - utuombee

Kitulizo cha maskini - utuombee

Matumaini ya wagonjwa - utuombee

Mlinzi wa wakimbizi - utuombee

Mlinzi wa wenye shida - utuombee

Mlinzi wa maskini - utuombee

Mlinzi wa walio kufani - utuombee

Mlinzi wa wenye kuzimia - utuombee

Kitisho cha mashetani - utuombee

Mlinzi wa Kanisa Takatifu - utuombee

Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utusamehe Bwana

Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utuhurumie Bwana

Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utusikilize Bwana

K. Amewekwa Bwana wa nyumba yake

W. Na mkubwa wa mali yake yote.

Tuombee: Mungu uliyetaka kwa maongozi yasiyotajika, ulimteua Yosefu mwenye heri, kuwa mchumba wa mzazi wako Mtakatifu, fanyiza twakuomba, tustahili kumpata mwombezi mbinguni yeye mwenyewe tunayemheshimu kama msimamizi duniani unayeishi na kutawala milele na milele. Amina.

LITANIÆ IN HONOREM S. IOSEPH SPONSI B. MARIÆ V.

Kyrie, eléison.                                           

Christe, eléison.                                         

Kyrie, eléison.                                           

Christe, audi nos.                                      

Christe, exáudi nos.                                   

Pater de cælis, Deus,                                  miserére nobis.

Fili, Redémptor mundi, Deus,                     miserére nobis.

Spíritus sancte, Deus,                                 miserére nobis.

Sancta Trínitas, unus Deus,                         miserére nobis.

Sancta María,                                             ora pro nobis.

Sancte Ioseph,                                            ora pro nobis.

Proles David ínclyta,                                  ora pro nobis.      

Lumen Patriarchárum,                                ora pro nobis.

Dei Genitrícis sponse,                                ora pro nobis.

Custos Redemptóris,                                ora pro nobis.

Custos pudíce Vírginis,                              ora pro nobis.

Fílii Dei nutrítie,                                        ora pro nobis.

Christi defénsor sédule,                              ora pro nobis.

Serve Christi,                                            ora pro nobis.

Miníster salútis,                                        ora pro nobis.

Almæ Famíliæ præses,                               ora pro nobis.

Ioseph iustíssime,                                       ora pro nobis.

Ioseph castíssime,                                      ora pro nobis.

Ioseph prudentíssime,                                 ora pro nobis.

Ioseph fortíssime,                                       ora pro nobis.

Ioseph obedientíssime,                               ora pro nobis.

Ioseph fidelíssime,                                     ora pro nobis.

Spéculum patiéntiæ,                                   ora pro nobis.

Amátor paupertátis,                                    ora pro nobis.

Exémplar opíficum,                                    ora pro nobis.

Domésticæ vitæ decus,                               ora pro nobis.

Custos vírginum,                                        ora pro nobis.

Familiárum cólumen,                                 ora pro nobis.

Fúlcimen in difficultátibus,                      ora pro nobis.

Solátium miserórum,                                  ora pro nobis.

Spes ægrotántium,                                      ora pro nobis.

Patróne éxsulum                                       ora pro nobis.

Patróne afflictórum,                                 ora pro nobis.

Patróne páuperum,                                  ora pro nobis.

Patróne moriéntium,                                   ora pro nobis.

Terror dæmónum,                                      ora pro nobis.

Protéctor sanctæ Ecclésiæ,                          ora pro nobis.

Agnus Dei, qui tollis peccáta mundi, parce nobis, Dómine.

Agnus Dei, qui tollis peccáta mundi, exáudi nos, Dómine.

Agnus Dei, qui tollis peccáta mundi, miserére nobis.

℣. Constítuit eum dóminum domus suæ.

℞. Et príncipem omnis possessiónis suæ.

Orémus.

Deus, qui ineffábili providéntia beátum Ioseph, sanctíssimæ Genitrícis tuæ sponsum elígere dignátus es, prǽsta, quǽsumus, ut, quem protectórem venerámur in terris, intercessórem habére mereámur in cælis. Qui vivis et regnas in sǽcula sæculórum. ℞. Amen.

Litania ya Mt. Yosefu
03 May 2021, 14:29