Tafuta

Vatican News
Eneo la shambulizi huko Corinto nchini Colombia tarehe 26 Machi 2021 Eneo la shambulizi huko Corinto nchini Colombia tarehe 26 Machi 2021  (AFP or licensors)

Ukaribu wa Papa kwa watu waathirika wa vurugu Colombia Kusini

Katika telegram ya Papa Francisko iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican,Kardinali Pietro Parolin ambayo imeelekezwa kwa rais wa Baraza la Maaskofu nchini Colombia,Papa anakumbuka shambulizi na migogoro halisi katika eneo la Kusini mwa Colombia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko anaalaani matukio ya shambulizi na vurugu na anaonesha ukaribu wake kwa watu ambao wanaishi katikati ya mateso makubwa katika Mkoa wa Pasifiki ya Kusini Magharibi mwa Colombia. Hayo yameandikwa na Katibu wa Vatican, Kardinali Petro Parolin katika Telegram aliyoelekeza kwa Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Colombia, Askofu Mkuu Oscar Urbina Ortega, wa Jimbo Kuu Katoliki Villavicencio. Katika ujumbe huo anakumbusha hata jitihada za Maaskofu, makuhani, watawa kike na kiume na walei katika harakati za kutafuta bila kuchoka kujenga mahusiano ya amani katika kanda hiyo nzima.

Shambulio na vurugu

Katika kipindi cha mwisho yamerekodiwa matukio ya vurugu kwa upande wa Kusini mwa nchi. Tarehe 26 Machi, makumi ya watu walibaki wamejeruhiwa huko Corinto, kusini magharibi mwa Kolombia ya Cauca. Bomu lilipuka mbele ya manispaa, katika eneo ambalo ni kitovu cha Jumuiya ya watu Asilia nchini Colombia. Ni katika eneo ambalo kwa makumi ya miaka iliyopitia ilikuwa ni ngome ya vikundi cha upinzani (Farc). Kwa  maana hiyo linahusiana  na vikundi vyenye silaha na magenge yanayohusiana na wauzaji wa dawa za kulevya. Corinto, kama manispaa jirani, na Toribío, ni manispaa zinazoongozwa kihistoria na watu wa asili. Huko Toribio, Padre Álvaro Ulque, kuhani wa kiasilia wa huko Colombia, aliuawa mnamo 1984, na walioendeleza utume wake ni wamisionari wa Consolata. Ripoti, iliyowasilishwa hivi karibuni na ya meza ya Kiekumene kwa ajili ya Amani na mashirika mengine, inaandika kuwa hizo ni vurugu zilizotesa kwa miongo kadhaa na mashirika ya Kanisa ambayo yamekuwa yakipambana pamoja na vikundi maskini zaidi.

10 April 2021, 10:28