Tafuta

2021.04.18: Kardinali Parolin ameathimisha Misa katika Chuo Kikuu Katoliki cha Milano katika fursa ya Jubilei ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwake 2021.04.18: Kardinali Parolin ameathimisha Misa katika Chuo Kikuu Katoliki cha Milano katika fursa ya Jubilei ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwake 

Papa kwa Chuo Kikuu Katoliki:Vijana wajifunze na matumaini endelevu!

Mara bada ya sala ya Malkia wa Mbingu,Papa Francisko amekumbuka Siku ya 97 ya Chuo Kikuu cha Moyo Mtakatifu cha Milano,akiwatakia waendeleze utume wa kielimu na kuibariki Jumuiya nzima.Katika fursa hiyo ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa,Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican ameadhimisha Misa Takatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, akiwa  katika dirisha wa Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa waamini, Dominika tarehe 18 Aprili 2021, amesema: “Leo nchini Italia inaadhimishwa Siku ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, ambacho kwa miaka mia moja kimekuwa kikifanya huduma msingi kwa ajili ya mafunzo na uundaji wa vizazi vipya.” Papa Francisko amesema kwamba “hawa wanaweza kuendelea kutekeleza lengo lake la  kielimu ili kusaidia vijana kuwa wahusika wakuu wa siku zijazo zilizo na matumaini. Kwa maana hiyo amewabariki, wafanyakazi, maprofesa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki.

Salamu kwa waroma na mahujaji

Na hatimaye Papa Francisko akiwageukia umati  katika uwanja wa Mtakatifu Petro amesema:“Na sasa salamu  ni kwenu nyinyi nyote, Waroma na mahujaji..., Wabrazil, Wapoland, Wahispania ..., na ninaona bendera nyingine hapo... Asante Mungu tunaweza kukutana tena katika uwanja huu katika  sherehe ya Jumapili na likizo. Ninawambia jambo moja: Ninakosa uwanja huu wakati lazima nifanye Sala ya Malaika kwenye Maktaba. Nina furahi, asante Mungu! Na asante kwa uwepo wanu ... Na kwa watoto wa Parokia ya Mkingiwa  ni wazuri... Na kwa wote  ninawatakia Jumapili njema. Tafadhali msisahau kuniombea. Mlo Mwema, mchana mwena na kwaheri ya kuonana!”

Kardinali Parolin aongoza Misa ya Jubilei ya miaka 100

Katika misa iliyofanyika katika Kikanisa cha Chuo Kikuu Katoliki Milano nchini Italia , Dominika tarehe 18 Aprili 2021 imeongoza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican. Katika mahubiri yake amenukuu Ujumbe wa Baraza la Maaskofu  nchini Italia katika fursa ya tukio la kuadhiisha Miaka 100 ya Chuo Kikuu hicho. Kardinali amesema kwamba chuo hicho kinaitwa kukabiliana na changamoto ambazo siyo rahisi kama zile za mwanzo, kuhusiana na shughuli ya kitaaluma na ulazima wa ubunifu kwa ajili ya mafunzo na utafiti, badala yake  ni kutoa maendeleo kamili ambayo ni utume wa tatu na ambao tangu mwanzo umekuwa ukiongoza chuo hicho.  Kwa kufanya kumbu kumbu ya shukrani ya karne iliyopita, ambayo iliona maendeleo ya kila wakati ya Taasisi Katoliki, Kardinali Parolin amewaalika watazame mbele, wakikumbuka kazi yake ya kufungua akili ya vijana na si tu katika ufahamu, lakini pia katika hekima ya Mungu iliyooneshwa na Yesu.

Mungu anajua na kuondoa hofu zetu

Kardinali Pietro Parolin, akijikita kufafanua Injili ya Liturujia ya Dominika ya Tatu ya Pasaka ambapo Yesu alifungu mitume wake akili kwa ajili ya kutambua Maandiko, wakati walikuwa bado wamekumbwa na hofu, Yesu Mfufuka alisimama katikati yao na wao wakafikiria wanaona kivuli na kutetemeka wakidhani amekuja kulipiza kisasi kutokana na kumkana na kumwacha peke yake.  Kardinali ameongeza kusema “Inajionesha wazi hasa woga wa kina ambao ni wa kidini. Kwa sababu Mwenyezi anajua, na anaondoa hofu ambayo imeambukizwa hata kwetu sisi wenyewe”. Mara nyingi Kadinali ametoa mfano kuwa picha ya Mungu inayojionesha kwetu ni ya kuheshimu, lakini pia ya kumwogopa. Mawazo ni mengi hasa ya kufikiria kwamba : Je Mungu atanifanya nini ikiwa mwenendo wangu ni mbaya? Je atanitaka nini ikiwa mimi nitajikabidhi kwake? Je atanitumia labda jaribiofulani? Woga huu umekita ndani mwetu ni kama muhuri mweusi wenye kizingiti hadi  kufikia kuanguka kwetu; ni picha ya uongo au iliyopindishwa kuhusu  Mungu, lakini inatokana na tunda ya kudhani kwetu na hofu zetu. Inakita ndani ya moyo wa mawazo tanayosongwa na kukandamizwa, ya Mungu ambaye ni Bwana badala ya kuwa Baba, ambaye hutuelekeza kama mwingiliano wenye mguso, mdhibiti mwema na hakimu mkali.

Yesu aliwaonesha mitume uso wa kweli wa Mungu

Kardinali Parolin amesema kuwa, Yesu kwa njia ya ishara na maneno yake aliwaonesha mitume wake uso wa kweli wa Mungu. Yeye aliomba aguswe, alikula na wao, alawaalika watazame majereha kutokana na misumari kwenye mikono na miguu yake akifuta kabisa umbali kati ya Mungu na mwanadamu. Kwa mujibu wa Kardinali, Yesu anaonesha ishara za udhaifu wa kweli wa mwanadamu ambazo alizibeba. Madonda yake,  mikondo iliyofunguliwa ya huruma, inatualika kwa namna ya kujifunulia kwake, na Yeye anabeba udhaifu wetu, unyonge wetu kwa sababu Mungu anatupenda hata pale penye umaskini ambao tunapata aibu. Madonda ya Mfufuka, alama zisizofutika katika upendo wake kwa ajili yetu, yanatuonesha kuwa hakuna misumari ya dhambi, hakuna jeraha la maisha, hakuna majuto ya wakati uliopita yanaweza kuwakilisha kizingiti cha kutofanya huruma kuelekea kwetu.

WAKATI WA IBADA YA MISA ILIYOONGOZWA NA KARD. PAROLINI
WAKATI WA IBADA YA MISA ILIYOONGOZWA NA KARD. PAROLINI

Mugu hakuepusha mateso kwa mwanae

Kardinali Parolin akiendelea na mahubiri hayo amesema kuwa “Lakini wafuasi wa Yesu katika Injili hawana hofu tu japokuwa hata wasi wasi na kujaa mashaka. Kilichowafanya kuwa hivyo ni msalaba, na kifo cha Yesu wakati wao walikuwa wanafikiria ni Masiha ambaye alipaswa kuwa na nguvu na kushinda, lakini hata hivyo Kardinali ameongeza kusisitiza kuwa hilo “Lazima kutimizwa kama maandiko yalivyo andikwa kuhusu mimi” , alisema Yesu. Neno” lazima ambalo Yesu anaelezea kuwa Mungu ni kitenzi hiki  ambacho Yesu alielezea kwamba Mungu hakuepusha tendo la mateso makali, lakini alimkomboa, akamchukua mwenyewe. Na haya yote yanatuelezea kuwa uovu unaweza kushindwa tu kwa njia hii: sio kwa kukimbia, si kwa nguvu, lakini ni kwa upendo. Hivi ndivyo Mungu alifanya na huu ni ukuu wake ambao haujawahi kutokea wa kujua jinsi ya kubadilisha kila kitu kuwa kizuri kupitia upendo. Kila kitu, hata mateso na kifo. Hii pia ni maana yetu ya Pasaka kwamba ni kufanya kila kitu kinachopita katika maisha yetu kupitia katika upendo wa Mungu.

MISA YA JIBILEI YA MIAKA 100 YA CHUO KIKUU KATOLIKI CHA MILANO
MISA YA JIBILEI YA MIAKA 100 YA CHUO KIKUU KATOLIKI CHA MILANO

Kufundisha watu waliokomaa ili kusaidia vijana wawe mstari wa mbele katika njia mpya

Katibu wa Vatican kwa njia hiyo amesema hatua ya kutimiza ni ile ya kumkaribisha Bwana katika pembe za ndani  zaidi ya maisha yetu, mahali ambapo hofu, woga, mashaka na kujifunga kwetu vinaishi. Mwaliko wa Yesu wa kutokuwa na hofu, ndiyo ameuelekeza kwa wale wote wanaojifunza na kufanya kazi katika Chuo Kikuu Katoliki kwamba: “ Msiogope mbele ya wakati ambao hauna uhakika na umejaa mabadiliko ya wakati. Msiogope kwa kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko, anasisitiza kwa nguvu, kuhusiana janga lakini  Kardinali akiamini ni kweli, yaani janga la kielimu, huku  akitualika kujitoa, familia, jumuiya, shule, vyuo vikuu, taasisi, dini, watawala, wanadamu wote kufundisha watu walikomaa na kusaidia vijana kuwa wahusika wakuu wa njia mpya”. Amehitimisha.

18 April 2021, 13:59