Tafuta

Papa Francisko:Matukio ya Misa ya Huruma ya Mungu katika picha

Misa imeudhuriwa na uwakilishi wa wauguzi kutoka Hospitali ya Roho Mtakatifu,Sassia, Wamisionari mbali mbali wa Huruma,walemavu,wafungwa wa kike na viongozi wengine.wakiwakilisha makuhani zaidi ya elfu moja,wa taasisi zilizoanzishwa wakati wa Jubilei ya Maalum ambao Papa aliwakabidhi utume wa maadhimisho ya sakramenti ya kitubio.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Katika Misa aliyoongoka katika Kanisa la Roho Mtakatifu, Papa Francisko katika Dominika ya Huruma ya Mungu  tarehe 11 Aprili 2021 amesema "kwa kuabudu, na kwa kubusu majeraha yake tunagundua kuwa kila udhaifu wetu umepokelewa katika huruma yake. Hii inatokea kwa kila Misa, mahali ambapo Yesu anatoa mwili wake uliojaa majeraha na mfufuka. Tunamgusa na Yeye anagusa maisha yetu. Na anafanya kushuka kwetu Mbingu. Majereha yake angavu yalipasua giza ambalo tunalibeba ndani mwetu. Na sisi kama Tomasi, tunampata Mungu, tunamgundua ndani na karibu kwa hisia nzito tunasema “Bwana wangu, Mungu wangu” (Yh 20,28). Yote hayo yanazaliwa hapa, na neema ya kuwa tumehurumiwa. Kutoka hapa tunaanza safari ya kikristo. Ikiwa tunahesabu uwezo wetu, kujitosheleza na miundo yetu na mipango yetu, hatutakwenda mbali. Ni pale ambapo tutapokea upendo wa Mungu tu tutaweza kutoa chochote kipya katika ulimwengu.

WAAMINI WAKATI WA MISA
WAAMINI WAKATI WA MISA

Kwa maana hii walifanya utume waliohurumiwa, waligeuka kuwa wenye huruma. Tunawaona katika somo la kwanza. Katika kitabu cha Matendo ya mitume kinasimulia kuwa “wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. (Mdo 4,32. Hii siyo ukomusiti ni ukristo ulio safi. Na inashangaza sana ikiwa tunafikiria kwamba mitume hao hao kabla walikuwa wamegombania juu ya zawadi na nafasi muhimu kwamba ni nani angeweza kuwa mkuu kati yao (taz Mk 10,37; Lk 22,24). Na sasa wanashirikishana kila kitu, walikuwa na moyo mmoja na roho moja (Mdo 4,32). Je walifanyaje kubadilika hivi? Waliona katika mwingine huruma ile ile ambayo iliyo wabadilisha maisha yao. Waligundia kuwa na utume mmoja, msamaha na Mwili wa Yesu. Kushirikisha mali za nchi zikawa matokeo ya kawada.

MAADHIMISHO YA MISA
MAADHIMISHO YA MISA

Papa Francisko ameuliza swali: Je unataka kuhakikisha kuwa Mungu amegusa maisha yako. Hakikisha ikiwa unainamia madonda ya wengine. Leo hii ni siku ya kujiuliza. “Mimi ambaye nimepokea mara nyingi amani ya Mungu, msamaha wake, huruma yake, ninayo huruma kwa wengine? Mimi ambaye mara nyingi nimemwilishwa Mwili wake, ninafanya chochote kushibisha ambaye ni maskini? Tusibaki na sintofahamu. Tusiishi imani nusu ya anayepokea lakini hatoi, anayepokea zawadi lakini hajifanyi zawadi. Tulihurumiwa, tugeuke kuwa wenye huruma. Kwa sababu ikiwa upendo unaishia ndani mwetu tu, imani inakauka ndani bila kuzaa matunda, bila wengine haiwezi kuwa mwili. Bila kazi ya huruma inakufa (Yk 2,17). Tuuishe amani, kutoka na msamaha na majeraha ya Yesu wa huruma. Na tuombe neema ya kugeuka kuwa mashuhuda wa huruma. Ni kwa njia hiiyo tu imani itakuwa hai. Na maisha yanaunganika. Ni kwa njia hiyo tu tutatangaza Injili ya Mungu kwamba ni Injili ya huruma. Papa Francisko amehihitimisha na kukaa kimya kabla ya sala ya Nasadiki.

MAKUHANI WALIOSHIRIKI MISA NA PAPA
MAKUHANI WALIOSHIRIKI MISA NA PAPA
11 April 2021, 17:41