Tafuta

2021.04.03:Kitabu: maisha ya Roho, Papa Francisko na Padre Franco Nardin 2021.04.03:Kitabu: maisha ya Roho, Papa Francisko na Padre Franco Nardin 

Papa Francisko,Maisha ya Roho.Mungu anazungumza katika moyo wa mtu

“Papa Francisko Maisha ya Kiroho.Mungu anazungumza katika moyo wa mtu” ni kichwa cha kitabu kipya chenye mkusanyo wa tafakari za Papa zilizoandaliwa na Padre Nardini.Utangulizi wa kitabu hicho umeandikwa na Kardinali Angelo De Donatis,Makamu wa Papa,Jimbo la Roma.Kitabu hicho kinapatikana katika Duka la vitabu toleo la Paulinus tangu tarehe 6 Aprili 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kitabu kipya chenye mkusanyiko wa tafakari za Papa Francisko kilichopewa jina la Papa Francisko Maisha ya Roho. Mungu anazungumza katika moyo wa mtu, kimeandaliwa na Padre Franco Nardin kikiwa na utangulizi wa Kardinali Angelo De Donatis Makamu wa Papa, kinapatikana tayari kwenye maduka ya vitabu tangu tarehe 6 Aprili 2021. Katika utangulizi wake Kardinali De Donatis kuhusu kitabu hicho anandika kuwa  “maneno muhimu ya kiroho katika Hati ya Mwisho ya Mafundisho ya Kipapa, yamejikita kwa kina na daima katika wazo la kitaalimungu naAnthropolojia yaani sayansi ya jamii ambayo imejitolea kusoma kwa nyanja zote za Asili ya mwanadamu) ambayo Papa mweywea anafafanua  kama Maisha ya Kiroho. Ni tasaufi ya kwelu ya moyo ambayo inafungamanisha tamaduni kubwa za Kanisa na Tasaudi ya Mtakatifu Ignaius wa Loyola. Jina la kitubu Maisha ya Roho. Mungu anazungumza katika Moyo wa mtu kinataka kuonesha wazi wzo kuu la Papa Francisko ambacho si tu mkusanyiko rahi wa nukuu zake na tafakari za kiroho, lakini ni ukweli wa mafunz a Kitaalimungu kiroho, katika maisha ya utatu uliosimikwa ndani ya mtu, aliye mfano na sura ya Mungu.

Ni Roho kwa hakika ambaye anatufanya kuwa watoto kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu., ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba (Rm 8,15). Ndiyo hapo Yeye anatushauri kuanzia na upyaisho wa shauku katika kutangaza Neno la Mungu na uzuri wa Ukweli Kristo. Anaandika Kardinali De Donatis. Wazo ya Taalimungu ya kiekuemeana kwa maana hiyo ni kama mchango wa nguvu katika maisha ya kiroho kwa waamini wengi, watawa, na makuhanii ili waweze kuongozwa na kufunguka si tu kutokana na sauti ya Roho , kwa ajili ya kuponesha dhidi ya ugumu wa moyo, lakini pia hata kuwa na moyo daima wenye uwezo wa kufanya mang’amuzi yawe binafsi na hata ya kichungaji, ili kuweza kutambua ishara ambazo Mungu mpaji anatupatia kila siku, na kwa ajili ya kuwa na mazungumzo yenye kuzaa matunda na Makanisa, Tamaduni na dini, anaandika katika utangulizi Kardinali.

Ikumbukwe Jorge Mario Bergoglio, yaani Papa Francisko alizaliwa huko Buenos Aires nchini Argentina mnamo tarehe  17 Desemba 1936. Ni mtoto wa muhamiaji kutoka Mkoa wa Piemonte nchini Italia. Yeye ni mtaalam wa somo la Kemia. Akiwa na umri wa miaka 21 alijiunga  unovizi katika Shirika la Yesu yaani Kijesuit. Baada ya shahada ya Falsafa, mnamo tarehe 13 Desemba 1969 alipewa daraja la Kikuhani. Aliendelea na maandalizi ya kiroho kati ya mwaka 1970 na 1991 nchini Uhisipania na tarehe 22 Aprili 1973 alifunga nadhiri za milele. Alirudi nchini Argentina na tarehe 31 Julai 1973 akachaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Kijesuit huko Aregentina. Mnamo tarehe 20 Mei 1992 akachaguliwa kuwa Askofu wa Auca na Msaidizi wa Jimbo Kuu la Buenos Aires, Argentina. Tarehe 3 Juni 1997 alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Buenos Aires.

Haikupita hata miezi tisa, baada ya kifo cha Kardinali Quarracino wa jimbo Kuu akachukua jukumu la jimbo kuu, mnamo tarehe 28 Februari 1998, kama Askofu Mkuu na mkuu wa Kanisa la Argentina, kwa maadhimisho na ibada ya kuingia katika Jimbo Kuu hilo. Katika uteuzi wa makardinali wapya mnamo tarehe 21 Februari 2001, akachaguliwa kuwa Kardinali na Mtakatifu Yohane Paulo II. Na tarehe 13 Machi 2013 akachaguliwa kuwa Papa na kuchagua jina la Francisko.

07 April 2021, 15:28