Tafuta

2021.04.11 Santa Messa Chiesa di Santo Spirito in Sassia 2021.04.11 Santa Messa Chiesa di Santo Spirito in Sassia 

Papa Francisko:Toa huruma ya dhati,ukaribu,huduma na umakini kwa wahitaji!

Mara baada ya misa na kabla ya sala ya Malkia wa Mbingu Papa Francisko akiwasalimia waliokuwapo amewafafanua kama ndiyo hali halisi ya huduma ambayo inafanyika kwa dhati,wanakaribia,wanatoa huduma na umakini kwa watu wenye shida.Kwa maana hiyo amewatakia matashi mema ya kuhisi daima waliohurimiwa na ili nao pia waweze kuwa na huruma kwa wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko mara baada ya Misa Takatifu katika Dominika ya Huruma ya Mungu tarehe 11 Aprili 2021 amesema kuwa kabla ya kuhitimisha maadhimisho amependa kuwashukuru wale wote walioshirikiana kuandaa na kuitangaza moja kwa moja. Na amewasalimia wale wote ambao wameunganika kwa njia ya vyombo vya habari. Salamu kwa namna ya pekee wale wote ambao walikuwawapo katika Kanisa la Roho Mtakatifu Sassia, ambayo ni Madhabahu ya Huruma ya Mungu. Waamini Walei, wauguzi, wafungwa, walemavu, wakimbizi na wahamiaji, watawa wa Hospitali wa Huruma ya Mungu, watu wa kujitolea na viongzoi wa   Ulinzi wa raia. Wote hawa  amesema walikuwa wanawakilisha baadhi ya hali halisi mahali ambamo huruama inakuwa ya dhati, inakuwa ya ukaribu, ya huduma, ya umakini kwa watu walio katika matatizo. Papa Francisko  amewatakia wahisi daima huruma hiyo ili nao waweze kuitoa huruma hiyo. Bikira Maria, Mama wa Huruma awajalia neema hiyo kwa wote.

SALAMU ZA PAPA
SALAMU ZA PAPA

Ikumbukwe hata hivyo kwa mujibu wa Maelezo kutoka kwa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya, kuwa maadhimishao hayo, miongoni mwao walioudhuria pia ni wakimbizi vijana kutoka Siria, Nigeria na Misri, wakiwemo watu wawili wa Misri wa Kanisa la kikopti  na mtu wa kujitolea wa Siria wa Caritas wa Kanisa Katoliki la Kisiria. Kikundi cha wafungwa kutoka gereza la Regina Coeli, Rebibbia wa kike na Casal ya Marmo, Roma, vile vile watakuwapo baadhi ya watawa Huruma wanaofanya kazi katika Hospitali, uwakilishi wa wauguzi kutoka Hospitali ya Roho Mtakatifu, Sassia karibu na madhabahu hiyo. Pamoja na Papa kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Wamisionari mbali mbali wa Huruma wataungana, wakiwakilisha makuhani zaidi ya elfu moja, wa taasisi zilizoanzishwa wakati wa Jubilei ya Maalum, ambayo Papa aliwakabidhi utume unao unganishwa na maadhimisho ya sakramenti ya Upatanisho na mahubiri ya fumvo la huruma ya kimungu.

BAADHI YA WAAMINI
BAADHI YA WAAMINI

Usomaji wa masomo walikuwa ni waseminari, wakati huduma ya liturujia ya kuhudmia altareni imehudumiwa na vijana kutoka parokia nje kidogo ya Roma. Kwa kufuata sheria za kuzuia maambukizi ya Covid, mahudhurio ya waamini walikuwa 80. Papa Francisko amepata kuwasalimia.

UZURI WA KANISA HILI
UZURI WA KANISA HILI
11 April 2021, 16:40