Tafuta

Vatican News
VOLKANO KATIKA KISIWA CHA CARIBBEAN VOLKANO KATIKA KISIWA CHA CARIBBEAN  ((C)2020)

Papa Francisko aombea watu waliokimbia hatari ya Volkano

Katika maneno ya Papa yaliyomo kwenye telegram iliyosainiwa na Kardinali Parolin anawaombea watu wa selikali ya Mtakatifu Vincent na Grenadines,katika Antilles Ndogo,ambapo wamehamishwa maelfu ya watu ili kuepuka janga la kibinadamu lililosabishwa na Volkano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko tarehe 23 Aprili 2021 ametuma telegram yake iliyosainiwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kwa wahanga wa mlipuko wa volkano “La Soufrière” katika visiwa vya Mtakatifu Vincent na Grenadines, huko Karibiani ulitokea hivi karibuni. Papa Francisko anawahakikishia ukaribu wake wa kiroho kwa wale wote ambao wameathiriwa hivi karibuni na volkeno hiyo na anaelezea mshikamano wake kwa watu waliotawanyika na kuacha nyumba zao huku wakitafuta mahali pa kukaa kutokana na janga hili. Anasali kwa namna ya peke kwa wanahusika na janga hili la kibinadamu kwa watu wa kujitolea ambao wanaendelea kusaidia kwa matumaini kwa Mungu mpaji. Volkano hiyo ilianza kulipuka mnamo tarehe 9 Aprili baada ya zaidi ya miaka 40 ya kulala. Mlipuko huo ambao ulifanyika mnamo 1902 ulisababisha vifo 1,680, wakati wa mwisho, mnamo 1979, haukusababisha waathiriwa wowote, shukrani kwa kengele iliyopiga mapema. Mamlaka ya serikali imeamuru kuhamishwa kwa watu katika sehemu ya kisiwa cha Mtakatifu Vincent kutokana na uwezekano wa mlipuko huo kuwa mbaya sana.

Waziri wa Kilimo Saboto Kaisari mezindua wito kuhusu ukosefu wa chakula: “Tunakabiliwa na janga katika kilimo na uvuvi  na shida zinazohusu usalama wa chakula na uhuru kwa sababu upatikanaji wa chakula sasa huko mashakani”. Vijiji vyote vilifunikwa na majivu na majengo yaliyoathiriwa, shule na biashara kufungwa, mazao na mifugo kuharibiwa, na wakazi walio na upatikanaji mdogo wa maji safi. Safu ya majivu ilifikia kilomita elfu chache kwa urefu. Hata hivyo Umoja wa Mataifa ulizindua nao  ombi la haraka kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia suala hili la kisiwa hicho ambalo lina zaidi ya wakazi 100,000. Volkano ya “La Soufrière” ina urefu wa mita 1,220 na ya chini inayojumuisha mwingiliano wa matabaka ya lava iliyozidishwa na majivu ya volkano: kwa maana linafanya umbo lenye mteremko mkali. Milipuko ya mara kwa mara ni ya kulipuka.

23 April 2021, 16:27