Tafuta

Vatican News
Vita nchini Ucraine Vita nchini Ucraine   (Copyright: Serhiy Takhmazov)

Papa atoa wito wa kusitisha mapigano nchini Ukraine Mashariki

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu ametoa wito wa kusitisha vita huko Ukraine pia amekumbuka Wenyeheri wapya mashahidi ambao ni wamonaki wa Shirika la Cistercians wa Abasia ya Casamari,nchini Italia waliouawa mnamo 1799.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada sala ya Malkia wa Mbingu, Dominika ya III ya Pasaka, tarehe 18 Aprili 2021, Papa Francsko wakati wa salamu zake, amekumbuka hali halisi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea na kusema kuwa: “Na hili ni jambo la kusikitisha. Ninafuatilia kwa wasiwasi mkubwa matukio katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Ukraine, ambapo ukiukwaji na matatizo ya vita imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni, na ninaona kwa wasiwasi mkubwa kuongezeka kwa shughuli za vita. Kwa maana hiyo Papa amesema: “Tafadhali, ninatumaini sana kwamba inawezekana kuepukwa ongezeko la mivutano badala yake, ishara zenye uwezo wa kuhamasisha kuaminiana na kukuza maridhiano na amani, vinahitajika na ni vya lazima sana, na kutamaniwa. Tunapaswa pia kuzingatia hali mbaya ya kibinadamu ambayo idadi hiyo inajikuta, inakabiliana nayo, na ambayo ninaelezea ukaribu wangu na ambayo ninawaalika tuiombee. Salam Maria…

Wenyeheri wa Abasia ya Casamari

Papa Francisko aidha amekumbuka tukio la kutangazwa wenye heri, Simeone Cardon na wenzake watano, wamonaki wa Cistercians katika  tukio lililofanyika huko Abasia ya Casamari nchini Italia. Papa amesema iliku mnamo 1799, wakati wanajeshi wa Ufaransa walipokuwa wakirudi kutoka Napoli waliteka makanisa na nyumba za watawa, wanafunzi hawa wapole wa Kristo waliopinga kwa ujasiri na ushujaa, hadi kifo, kutetea Ekaristi dhidi ya kukashifiwa. Papa amesema kuwa mfano wao utuchochee kujitoa zaidi kwa uaminifu kwa Mungu, wenye uwezo wa kubadilisha jamii na kuifanya iwe ya haki na ya kidugu”. Tuwapigie makofi wenyeheri wapya…

WENYEHERI WAFIADINI WA ABASIA YA KASAMARI
WENYEHERI WAFIADINI WA ABASIA YA KASAMARI
18 April 2021, 13:54