Tafuta

Papa Francisko akutana na Waziri Mkuu Saad Hariri wa Lebanon Papa Francisko akutana na Waziri Mkuu Saad Hariri wa Lebanon 

Papa akutana na waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri

Alhamisi 22 Aprili 202,Papa Francisko amekutana na kwa faragha na Waziri Mkuu wa Lebanon ambapo katika mazungumzo yao,amewatakia Lebanon kwa msaada wa Jumuiya ya kimataifa,iweze kurudi kujikita ndani ya nguvu za mwerezi,wa kuishi katika utofauti ambao udhaifu unakuwa nguvu kwa watu wakuu walipopatanishwa na kwa wito wake wa kuwa ardhi ya kukutana,kuishi na kuwa tamaduni nyingi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Akijibu maswali ya waandishi a habari, Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, Alhamisi tarehe 22 Aprili 2021, Dk. Matteo Bruni, amesema: “ninaweza kuthibitishwa kuwa asubuhi hii, Baba Mtakatifu amekutana kwa mkutano wa faragha na Waziri Mkuu wa Lebanon, Saad Hariri.  Katika mazungumzo yao, yaliyodumu karibu dakika thereathini, Papa amependa kuelezea ukaribu wake kwa watu wa Lebanon ambao wanaishi kupindi cha matatizo makubwa na kisichokuwa na uhakika, na kukumbusha uwajibikaji wa nguvu zote za kisiasa ili wafanye jitihada kwa dharura kwa ajili ya wema wa Taifa.

Aidha katika kuelezea  shauku yake ya kutaka kuitembelea nchi, ikiwa kutakuwa na hali ya kuridhisha, Papa Francisko, amewatakia  nchi ya Lebanon kwa msaada wa Jumuiya ya kimataifa, iweze kurudi ndani ya nguvu za mwerezi, wa kuishi katika utofauti ambapo udhaifu unakuwa nguvu kwa watu wakuu waliopatanishwa na kwa wito wake wa kuwa ardhi ya kukutana, kuishi na kuwa tamaduni nyingi.

22 April 2021, 15:10