Tafuta

Tamko la Papa Francisko: Dr. José Gregorio Hernández Cisneros atakuwa ni Msimamizi mwenza wa Masomo ya Sayansi ya Amani  Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran, Tamko la Papa Francisko: Dr. José Gregorio Hernández Cisneros atakuwa ni Msimamizi mwenza wa Masomo ya Sayansi ya Amani Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran, 

Dr. Josè Gregorio Hermàndez: Msimamizi wa Sayansi ya Amani

Baba Mtakatifu Francisko ametamka kwamba, Mtumishi wa Mungu Dr. José Gregorio Hernández Cisneros atakuwa ni Msimamizi mwenza wa Masomo ya Sayansi ya Amani yaliyoanzishwa kwa tamko lake la tarehe 12 Novemba 2018 na kuchapishwa kwenye Nyaraka za Vatican AAS, CX [2018], 17-1722, kwa kushirikiana na Mwenyeheri Giovanni della Pace. Huyu ni Msamaria mwema!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Kardinali Baltazar E. Porras Cardozo, Msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Caracas, Venezuela, Barua N. AAC/26-21, Mwezi 9 Machi 2021; na kupokelewa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran. Baba Mtakatifu anasema, Mtumishi wa Mungu Dr. José Gregorio Hernández Cisneros atakuwa ni Msimamizi mwenza wa Masomo ya Sayansi ya Amani yaliyoanzishwa kwa tamko lake la tarehe 12 Novemba 2018 na kuchapishwa kwenye Nyaraka za Vatican AAS, CX [2018], 17-1722, kwa kushirikiana na Mwenyeheri Giovanni della Pace.

Mtumishi wa Mungu Dr. José Gregorio Hernández Cisneros, Mwamini mlei, alizaliwa tarehe 26 Oktoba 1864 huko Isnotù, Venezuela na kufariki dunia tarehe 29 Juni 1919 huko Caracas nchini Venezuela. Tarehe 30 Aprili 2021 akatangazwa kuwa ni Mwenyeheri. Tamko hili la Baba Mtakatifu Francisko limetolewa mjini Vatican tarehe 26 Aprili 2021.

Papa Tamko

 

 

29 April 2021, 15:11