Tafuta

2021.03.14. Uharibifu wa mji wa Siria katika vita ambavyo vimedumu sasa miaka kumi. 2021.03.14. Uharibifu wa mji wa Siria katika vita ambavyo vimedumu sasa miaka kumi.  

Wito wa Papa kwa Siria:Ulimwengu usaidie kwa maamuzi kusuluhisha mgogoro!

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,Papa Francisko amezindua kwa upya ombi kwa Jumuiya ya Kimataifa kwa ajili ya nchi ya Siria ambayo inateseka,ikiwa ni mwaka wa kumi tangu kuanza kwa mgogoro,na ili waweze kutoa tumaini kwa watu hao.Jitihada ziwe kwa sahemu zote mbili ili kuweza kujenga na mshikamano;silaha ziweze kusitishwa na kusuka kiungo cha kijamii kwa kuanza ujenzi mpya na uchumi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Wito wa dhati kwa wahusika kwenye mzozo huko Siria, ndiyo uliotolewa na Papa Francisko Jumapili tarehe 14 Machi 2021 ili kuonesha dalili za ishara ya mapenzi mema, kwa namna ya kuweza kufunguliwa mwanga wa matumaini kwa watu waliochoka. Lakini hata matashi ya maamuzi na upyaisho wa jitihada za kijenga na mshikamano wa jumuiya ya kimataifa ili kuweka silaha chini na kwamba kiungo cha kijamii kiweze kurekebishwa na ujenzi mpya vile vile kwa ajili ya urejesho wa uchumi.  Papa ametoa wito huo juu ya Nchi za Mashariki ya kati, katika mkesha wa kumbu kumbu ya mwaka wa kumi tangu mwanzo wa mzozo wa umwagaji damu huko Siria uanze, ambao umekuwa moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu ya wakati wetu. Papa anakumbuka mateso ya nchi pendwa ya  Siria kwani kuna idadi isiyo julikana ya waliokufa na waliojeruhiwa, mamilioni ya wakimbizi, maelfu ya watu, waliopotea, uharibifu, vurugu za kila aina na mateso makubwa kwa watu wote, hasa kwa walio hatarini zaidi, kama vile watoto, wanawake na wazee.

Papa Francisko  kwa ajili ya nchi ya Mashariki ya Kati, hasa Siria  amewaomba wote ili kusali kwa  Bwana kutokana na mateso mengi, katika Siria inayopendwa na inayoteswa, isisahaulike, na ili mshikamano wa wote ufufue matumaini. Kwa kufanya hivyo amewaalika waamini mara moja waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro na kusali sala ya “Salamu Maria….

Nchi ya Siria, ambayo inajiandaa kufanya kumbu kumbu ya miaka kumi ya mzozo, ambao ulizuka mnamo tarehe 15 Machi 2011, inalalamikia juu ya idadi kubwa ya waathiriwa: zaidi ya wahanga 400,000, wakimbizi milioni 12 na watu milioni 12.4, sawa na asilimia 60 ya idadi ya watu wote walioathiriwa na uhaba wa chakula. Hata hivyo zaidi ya wiki moja iliyopita, Papa Francisko mnamo tarehe 6 Machi, huko Iraq, katika mkutano wa kidini kwenye Uwanda wa Uru, aliwaalika wawakilishi wote wa dini kuomba kwa ajili ya Mashariki ya Kati, hasa ya karibu sana Siria  inayoteseka ili migororo ya kivita iishe na kushikamana na njia za amani, kushirikishana na kukarimu.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya mateso ya watu wa Siria kwenye ndege ya kurudi Roma, Papa Francisko alikuwa amezishukuru nchi zenye ukarimu, pamoja na Lebanon, ambazo hupokea wahamiaji; na kurudia kukumbusha sala katika mkesha wa maombi kwa ajili ya Siria mnamo tarehe  7 Septemba 2013. Yeye alikuwa amekumbuka “mchana huo wa sala katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kulikuwa na ibada ya kuabudu Sakramenti, wakiwa wanasali rozari ... Lakini ni Waislamu wangapi, ni Waislamu wangapi walio kwenye zulia wakiomba pamoja nasi kwa ajili ya amani huko Siria, kuzuia mabomu, kwani wakati huo walikuwa wakisema kuwa bomu kali lingelipuliwa.

14 March 2021, 17:32