Tafuta

2018.06.26 Ziara ya Rais wa Ufaransa Bwana Emmanuel Macron mjini Vatican 2018.06.26 Ziara ya Rais wa Ufaransa Bwana Emmanuel Macron mjini Vatican 

Papa na Rais wa Ufaransa wazungumzia safari ya Iraq

Wakati wa mazungumzo ya simu na rais wa Ufaransa, Jumapili tarehe 21 Machi Papa amerudi kutazama matunda ya safari yake ya kitume ya hivi karibuni nchini Iraq na wameweza kujadili mada nyingine kama vile changamoto zinazosababishwa na ubinadamu na janga la Covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ziara ya kitume ya  Papa Francisko hivi karibuni nchini Iraq ilikuwa ni kiini cha mazungumzo ya simu kati ya Papa na Bwana Emmanuel Macron, Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, siku ya Jumapili tarehe  21  Machi 2021. Na hiyo ni kutokana fursa ya ujumbe wake kutoka kwa Mkuu wa Nchi ya Ufaransa wakati wa maadhimisho ya hivi karibuni ya miaka nane ya upapa wa Fransisko. Na katika mazungumzo yao yamejikita juu ya migogoro kadhaa zinazoathiri kanda tofauti za ulimwengu lakini pia changamoto zinazosababishwa na ubinadamu na janga la Covid-19.

Ikumbukwe tangu kuanza kwa janga hilo mwaka mmoja uliopita, Papa Francisko mara kadhaa amewaalika watu kutafakari juu ya ulimwengu baada ya janga hili na  alianzisha,mara moja  mnamo tarehe 20  Machi 2020, Tume Maalum ya Vatican chini ya mamlaka Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu ili kufikiria juu ya changamoto za janga la baada ya corona hii.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Baba Mtakatifu Francisko na Rais wa Ufaransa kuzungumza kwa njia ya simu. Vingozi hao wawili walikutana katika mazungmzo hasa mnamo tarehe 30 Oktoba mara baada ya shambulio la kigaidi ambalo lililenga Kanisa kuu la ‘Notre-Dame de l'Assomption’yaani Mama Yetu Mpalizwa huko Nice. Rais wa Ufaransa pia alipokelewa jijini Vatican mnamo tarehe 26 Juni 2018 na Papa Francisko, katika mkutano wa zaidi ya saa moja.

22 March 2021, 16:00