Tafuta

Vatican News
Papa: Papa wakati akiungamisha baadhi ya mapadre Papa: Papa wakati akiungamisha baadhi ya mapadre  (ANSA)

Papa:Muungamishi siyo hakimu awe mfariji,baba na kaka!

Kila mmoja ni mwenye dhamb.Muungamishi amewekwa kuhudumia wengine ili kwa sakramenti ya Upatanisho,aweze kukutana na upendo unaovutia na kubadilisha maisha.Tunatambua kuwa siyo sheria ambazo zinaokoa.Mtu hawezi kubadilika kwa sababu ya safu za sheria ngumu bali mvuto wa upendo na zawadi ya bure kwa mungu.

Na Sr Angela Rwezaula- Vatican.

Kuanzia Jumatatu tarehe 8-12 Machi imefanyika Kozi ya XXXI, ya Toba ya Ndani iliyoandaliwa na Idara ya Toba ya Kitume, Vatican  kwa njia ya mtandao kutokana na virusi vya corona. Mwaka jana haikuwezekana kufanya kozi hiyo. Ni karibu makuhani  900 na waseminari wamefuatilia kwa njia hiyo ya umbali kozi hiyo ulimwenguni kote. Katika hitimisho la Kozi hiyo, Alhamisia 12 Machi Papa Francisko amekutana katika Ukumbi wa Paulo VI, na uwakilishi huo ambapo Papa amesema kwamba kozi hiyo kwa kawaida uangukia kwa kipindi cha neema ya Mungu  cha Kwaresima, kipindi cha jangwa, cha uongofu na kukaribisha huruma ya Mungu. Kwa namna ya pekee amemsalimia Kardinali Mauro Piacenza, Mhudumu Mkuu wa Toba ya Kitume na kumshukuru kwa hotuba yake, kwa niaba ya viongozi wengine. Hotuba ya Papa imejikita kuzungumzia mambo matatu ambayo amesema yanafafanua vizuri maana ya Sakramenti ya Upatanisho. Ya kwanza kijikabidhi  kabisa katika upendo, pili kujikabidhi ili ubadilishwe na upendo na tatu kuwajibika katika upendo.

Kujikabidhi kwenye upendo maana yake kutimiza tendo la kweli la imani. Imani haiwezi kamwe kupunguzwa katika orodha ya mantiki au safu za uthibitisho wa kuamini. Imani inajieleza na kueleweka ndani ya uhusiano. Uhusiano kati ya Mungu na mtu, na kati ya Mtu na Mungu kwa muktadha wa wito na jibu. Mungu anaita na mtu anaitikia. Imani ni mkutano na iImani ni kukutana na Huruma , na Mungu mwenyewe ambaye ni Huruma, na ni kujikabidhi katikati ya mikono ya upendo huo, fumbo na ukarimu ambao tunauhitaji sana lakini ambao wakati mwingine kuna hofu ya kujikabidhi. Papa Francisko amesema uzoefu unafundisha kuwa asiye jikabidhi katika upendo wa Mungu mapema au baadaye ataishie kujikadhi kwa mwingine na kuishia katika mikono ya hisia na akili za kiulimwengu, na mwishowe zinampelekea katika uchungu, huzuni na upweke. Kwa maana hiyo hatua ya kwanza kwa muungamishialiye  mwema, ndiyo hiyo ya tendo la imani,  kujikabidhi ambapo anayetubu anakaribia huruma.  Kila muungamishi lazima awe na uwezo wa kushangaza daima kwa ndugu ambao kwa imani wanaomba msamaha wa Mungu na bado kwa imani  wanajikabidhi kwake, hasa wanapojikabidhi wenyewe kwa Muungamishi. Uchungu wa dhambi binafsi ni ishara hiyo ya kujikabidhi kwa imani katika upendo, Papa amebainisha

Kuishi namna hiyo kwa kutubu maana yake ni kuacha ubadilishwe na upendo ambao ndiyo kelelezo cha pili ambacho Papa Francisko amependelea kufafanua. “Tunatambua kuwa siyo sheria ambazo zinaokoa. Mtu hawezi kubadilika kwa sababu ya safu za sheria ngumu bali kwa mvuto wa upendo na zawadi itolewayo bure. Ni upendo mbao ulijionesha na ambao ni Mungu mwenyewe ambaye alijionesha kwa watu kwa namna ambayo ndiyo ya kwanza na lazima, mpya kwa ujumla, hivyo  yenye uwezo wa kupyaisha mambo yote. Mwenye kutubu ambaye anakutana katika mazungumzo ya kisakramenti, mwanga wa upendo huo wa ukarimu, ambao unaacha abadilishwe na upendo, neema na kuanza kuhisi mabadiliko ya moyo wa jiwe na kuwa wa nyama. Hata katika maisha ya urafiki ni namna hiyo. Mtu anabadilika kutokana na kukutana na upendo mkubwa. Muungamishi mwema daima anaalikwa kugundua miujiza ya abadiliko na kugundua kazi ya neema katika mioyo ya mtubu huku akisaidia uwezekano wa tendo la mabadiliko hayo. Ufungamanishwaji hatia ni ishara ya mabadiliko ambayo upendo unafanya kazi, kwani yote yamekabidhiwa, kwa sababu yote yanasamehewa.

Kielelezo chatatu ambapo Papa Francisko amejikita nacho  ni kuwajibika na kujibu upendo. Kujikabidhi na kujiachia kubadilishwa na upendo ni kama ulazima na matokeo ya kuwajibika katika upendo ambao umetolewa. Mkristo daima analo neno lile la Mtakatifu Yakobo :“Nionesha imani yake bila matendo na mimi  nitakuonesha matendo yangu na imani yangu (Yak 2,8). Mapenzi ya kweli ya uongofu yanagu  na dhati  katika kujibu upendo wa Mungu ulitolewa na kupokelewa. Hii ni sawa sawa na kuonesha mabadiliko ya maisha na matendo ya huruma ambayo yanafuata. Aliyekaribishwa kwa upendo hawezi kutomkaribisha ndugu yake. Aliyejikabidhi katika upendo hawezi kuwacha kuwafariji wenye kuteseka. Aliye samehewa na Mungu hawezi kuacha kuwasamehe kwa moyo ndugu. Ikiwa ni kweli kwamba hatutaweza kuendana kikamilifu na Upendo wa kimungu, kwa sababu ya tofauti isiyoweza kufutwa kati ya Muumba na viumbe, ni kweli kwamba Mungu anatuonesha upendo unaowezekana, ambao kuishi upendo huo ni lazima yaani: Upendo kwa ndugu. Kwa kuwapenda ndugu tunajionesha sisi wenyewe, katika ulimwengu na Mungu kwamba tunampenda kweli na tunaendana kila wakati kwa njia inayofaa, hasa kwa huruma yake.

Papa Francisko pia kwa kusisitiza amewashauri wakumbuke daima kuwa kila mmoja wetu ni mdhambi aliyesamehewa, nafasi katika huduma ya wengine, kwa sababu hata wao kwa njia ya kukutana na sakramenti wanaweza kukutana na upendo ule ambao unavutia, na kubadilisha maisha yetu. Kwa uambuzi huo, Papa Francisko amewatia moyo ili waundwe kwa imani katika huduma hiyo yenye thamani ambayo wanatekeleza au ambayo wabatarajiwa kukabidhiwa. Ni huduma muhimu kwa ajili ya kutakatifua watu watakatifu wa Mungu.  Wakabidhi huduma yao ya upatanisho kwa nguvu ya ulinzi wa Mtakatifu Yosefu mtu wa haki na mwanifu. Papa Francisko wakati akiwaachia tafakari hizo, ametakia ufanisi mwema wa uongofu katika maungamo ya kwaresima na kuwabariki wote, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

12 March 2021, 16:58