Tafuta

2021.03.11  Polycarpos, Kiongozi wa Kanisa la Kirothodox nchini Italia 2021.03.11 Polycarpos, Kiongozi wa Kanisa la Kirothodox nchini Italia  

Papa kwa Polycarpos: wakatoliki na waorthodox kwa pamoja kusaidia wadhaifu

Amesimikwa Kiongozi mpya wa kiorthodox nchini Italia na eneo la Ulaya Kusini.Katika sherehe zilizofanyika huko Venezia,Italia.Katika fursa hiyo Papa Francisko ametuma ujumbe wake wa matashi mema kuwa kipindi cha janga,muungano unawaunganisha wakatoliki na waorthodox ugeuke kuwa umoja thabiti na ambao unaonekana zaidi kwa walio wadhaifu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko ametuma telegram yake kwa kiongozi mkuu mpya Polycarpos Stavropoulos, wa kiorthodox  nchini Italia na eneo la Ulaya Kisini  katika fursa ya kusimikwa rasimi. Katika ujumbe huo Papa anaungana na Yeye, Makleri, na waamini waliokuwapo, kumwomba Baba  Mungu, kisima cha kila wema, baraka nyingi za mbinguni ziwashukie na katika huduma yake. Katika ujumbe huo uliosainiwa kwa mkono wake Papa anaadika: “Ninaamini kwamba pamoja na wakatoliki na waordhox, tunaweza kufanya juhudi kwa ukarimu katika huduma ya walio wadhaifu zaidi hasa katika kipindi hiki cha janga, kwa kubadilisha kwa msaada wa Mungu, muungano ambao tayari unatuunanhisha katika umoja mkamilifu na unaoonekana”.

Tukio la kusimikwa rasmi kwa kiongozu huyo zimefanyika Alhamis tarehe 11 Machi 2021 asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Giorgio wa Kigiriki huko Venezia Italia. Baada ya kusimikwa a rasim, imefuata hotuba ya Mkuu huyo Polycarpos, ambaye amewasalimia na kushukuru hotuba zote, na zaidi kupitia hatua zote za mchakato wa safari yake ktika Bwana kwa ajili ya huduma ya Kanisa la Kristo. Mchakato ambao anasema umemfikisha hapo, baada ya kupewa daraja la ushemasi, ukuhani kwa mikononi mwa aluìiyekuwa awe Patriaki  wa sasa Bartholomeo, na pia uzoefu wa muda mrefu nchini Italia akiwa kama Makamu hata kumkumbuka kwa masikitiko mtangulizi, Zervos Gennadios, ambaye alifariki mnamo Oktoba 2020, kwa maana hiyo , Yeye anashika nafai hiyo, alichaguliwa kunako tarehe 14 Januari 2021

Hatimaye kiongozi huyo ameelezea hatua hizi za kina za kicungaji anazotarajia kufanya kwa ajili ya huduma ya Kanisa la Kiorthodox Italia. Katika sheria ya Kanisa la Upatriaki wa Kiekumene wa Costantinopoli, makao yake makuu yako Venezia Italia. Katika sherehe hizo, pia Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja a Kikristo  ametuma ujumbe wake. Kardinali anakumbusha umuhimu wa kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kutangaza Neno la Mungu, katika kuelimisha kizazi kipya na katika huduma kwa wenye kuhitaji zaidi ili kutoa mchango halisi wa safari ya pamoja kulelekea katika msimamo wa muungano kamili kati ya makanisa yote.

12 March 2021, 15:51