Tafuta

Vatican News
2021.03.27 Uzinduzi wa Mwaka wa Makakama ya Serikali ya Vatican 2021.03.27 Uzinduzi wa Mwaka wa Makakama ya Serikali ya Vatican   (Vatican Media)

Papa:Kanisa liwe mfano wa uwazi katika muktadha wa uchumi na fedha

Papa Francisko kwa miaka miwili mfululizo ameshiriki uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama wa Serikali ya Vatican.Ushauri wa Papa ni kwamba mipango iliyozinduliwa iwe na uwazi kabisa wa shughuli za kitaasisi ya serikali ya Vatican,hasa katika uwanja wa uchumi na kifedha,kwa kuzingatia vigezo na katika kiwango cha kimataifa.Kabla ya Mkutano Kardinali Parolin ameongoza Misa katika Kikanisa cha Kipapa Sistina.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 27 Machi 2021, Papa Francisko amezindua Mwaka wa Mahakama ya Vatican. Hii ni kutokana na kwamba licha ya mji wa Vatian kuwa makao makuu ya Kanisa katoliki ulimwenguni, ni nchi ndogo ambayo inajitegemea na kiongozi wake mkuu ni Papa. Kama nchi nyingine zozote, katika uendeleshaji, hufuata kanuni na taratibu za kisheria ambazo ni sawa sawa na Vatican katika mfumo wake wa kulinda, kuhifadhi na kutetea haki zote za raia wake, japokuwa tofauti na nchi nyingine kwenye mahusiano ya kimahakama na Jumuiya ya Kimataifa. Katika hotuba yake, Papa Francisko ameonesha furaha ya uzinduzi wa mwaka wa 92 wa mahakama hiyo ya serikali ya mji wa Vatican. Amewasalimia na kuwashukuru Dk. Pignatone  na  Profesa  Milano na kupongeza mshauri ambaye ni waziri Mkuu mpya wa Serikali ya Italia Bwana Mario Draghi kwa uwepo wake. Papa hata hivyo hakusahau kutaja makujumu aliyokuwa nayo Profesa Giuseppe Dalla Torre, ambaye aliaga dunia mwaka jana. 

Sababu za kufanyika mkutano katika ukumbi wa baraka

Papa  Francisko akiendelea amesema kuwa kuzuka kwa janga la virusi umepelekea kufanya mkutano huo katika Ukumbi wa Baraka uliomo  kati ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na uwanja wake. Eneo hilo Mapapa wamekuwa wakitoa Baraka kwa waamini katika Siku Kuu Muhimu na baraka za Urbi et Orb  kwa Roma na Ulimwenguni.  Upande mwingine wa Chumba unatazamana na Uwanja mkubwa wa Kanisa Kuu, katika matarajio ya utukufu wa Roho Mtakatifu ambaye anaangazia  kutoka juu. Mtazamo wa kimwili na kiroho ni kiini kati ya  nafasi iliyo wazi na wakati huo huo inaeonesha umuhimu wa muhimili wa Bernin ambao ni imani kwa maana kukikiri na kusheherekea karibu na kaburi la Petro. Papa amekumbuka jambo moja na kusema:  “Na ninakumbushwa ujasiri wa Pio XI wa kutaka kurudi kwenye ubaraza  huu kutoa baraka, kwa sababu kati ya mapazia na ubaraza kulikuwa na ghala na alipoomba kutoa baraka hiyo, ilibidi wasubiri kusafisha ghala hilo baada ya zaidi ya miaka sabini, Papa aliweze kutazama tena kwenye uwanja”.

Shukrani kwa jitihada zao za kazi ngumu

Mtazamo huo wote unaweza kutambulishwa kwa maana na zoezi ambalo Kanisa limeundwa na kutumwa na Kristo Bwana ili kutimiza utume usio badilishwa wa ukweli na kama Mtaguso II wa Vatican unavyofundisha “kueneza mfano wake wa utii na kujikana mwenyewe (Lumen gentium, 8), na mtindo wake wa Mungu wa ukaribu, upendo upeo na huruma. Kwa kazi hiyo ya Kanisa inaingia katika historia ambayo inakuwa mahali pa kukutana kati ya watu na mapatano kati ya watu ili kuwaelekeza Neno na Sakramenti kwa neema na mifano ya maisha, imani, katika uhuru na amani ya Kristo (Ad gentes, 9). “Huu ni mwaka wa pili mfululizo ambao ninashiriki katika ufunguzi wa mwaka wa mahakama. Ninachangamka na hisia ya shukrani na utambuzi, kwa sababu najua jinsi shughuli yenu inavyohitaji, wakati mwingine na ni ngumu, ambayo mnafanya kila siku kukuza utaratibu wa uhusiano wa kibinafsi na wa kijamii, ambao hupata usawa katika kazi ya haki”, Papa Francisko amebainisha.

Papa Francisko amewasihi kila mtu, ili mipango iliyozinduliwa hivi karibuni na ya sasa iwe na  uwazi kabisa wa shughuli za kitaasisi za serikali ya  Vatican, hasa katika uwanja wa uchumi na kifedha, ambazo zinahimizwa kila wakati na kanuni msingi za maisha ya Kanisa na  wakati huo huo, kwa kuzingatia vigezo na "mazoea mazuri" ya sasa katika kiwango cha kimataifa, na uonekane mfano, kama inavyotakiwa  na  ukweli wa Kanisa Katoliki. Wahudumu wote katika sekta hii, na wote wanaoshikilia ofisi za taasisi, kwa hivyo wawe na mienendo ambayo  inaashiria toba inayofaa, inapobidi kupita ya  kizamani, na lazima iwe ni mfano kwa wakati huu na wa baadaye. Hatua hii, katika matarajio itakuwa muhimu kuzingatia mahitaji ya kipaumbele ambayo pia  kwa kupitia mabadiliko muafaka ya sheria katika mfumo wa sasa wa kiutaratibu, kuibua usawa kati ya washiriki wote wa Kanisa na hadhi yao sawa na msimamo, bila upendeleo  wa kizamani na sio na  majukumu  bali  iwe kwa  kila mmoja kujenga Kanisa. Hii inahitaji uthabiiti  wa imani na mshikamano na tabia na matendo.

Tafakari juu ya mchangongo wao ili Vatican na Kanisa iwe na mfano mzuri

Kwa mtazamo huo na kwa madhumuni haya, ukweli wa kuwa pembeni katika mienendo ya uhusiano wa kiuchumi  haiwezi kuleta sisi kuwa jumuiya ya waamini na kama watu binafsi, kutoka katika jukumu fulani la ushuhuda. Badala yake tumeitwa kushuhudia, kwa usadikisho na kwa njia ya kuaminika, katika majukumu na, dhamana kubwa ya maadili ambayo inabainisha utume wa Kanisa, ikiwa ni “chumvi na mwanga" katika jamii na katika jumuiya ya kimataifa, hasa wakati wa shida kama ya sasa. Papa Francisko anawashauri kutafakari juu ya kile ambacho wanajikita nacho kila siku katika kazi yao iliyofichika na uvumilivu ambayo wanajitoa kama tunu msingi wa mchango wao ili Kanisa katika Serikali hiyo ndogo ya Vatican, iweze kuwa mfano mzuri wa mafundisho yake kwa jamii.

Mwito wa kufanya kazi kwa haki na wasiogope kusali

Papa anawaalika kwa maana hiyo wale walioitwa kufanya kazi kwa sababu ya haki, wasiogope kutumia muda mwingi wakati ambao wanajitoa wenyewe katika sala. Katika sala ndiyo njia  pekee ya kuweza kuchota kutoka kwa Mungu Neno lake ambalo ni utulivu wa ndani unaoruhusu kutimiza kazi zetu kwa  muda mrefu, usawa na wa kudumu. Lugha ya uchoraji na uchongaji mara nyingi inawakilisha dhamira ya Haki, katika mkono mmoja, kupima maslahi yanayopingana au hali na mizani, na tayari, kwa upande mwingine, kutetea haki kwa upanga. Picha ya Kikristo baadaye inaongeza ile ya utamaduni  wa sanaa ya hapo awali katika maelezo ya  umuhimu ambao siyo madogo hasa kwa  macho ya Haki hayajafunikwa macho, badala yake yameelekezwa juu, na hutazama Mbinguni, kwa sababu haki ya kweli ipo Mbinguni tu. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amewatakia mema na anawasindikiza kwa sala na baraka yake ili waendelea katika kutenda huduma yao ya haki.

Shukrani kutoka kwa Pignatone kwa Papa kuhusu maneno a msamaha na haki

Wakati wa mkutano huo, ametoa hotuba fupi Mwenyekiti wa Mahakama hiyo Giuseppe Pignatone, ambaye amemshukuru Papa Francisko kwa uwepo wake na kwa namna ya pekee alich kiandika katika Waraka wa ‘Fratelli Tutti’,  yaani ‘Wote ni ndugu’ kuhusiana na pendekezo la haki na msaada na  ripoti yake kuhusu msamaha. Ni maneno na maandiko ambayo yamekuwa na uwazi kabisa katika mada muhimu sana kwa wote ambao wanatoa huduma katika kitengo hicho na ambacho ni muhimu sana kwa haki.

Kardinali Parolin ameadhimisha Misa katika Kikanisa cha Kipapa

Kabla ya Mkutano huo, Kardinali Pietro Parolin, katibu wa Vatican, ameongoza Ibada ya Misa katika Kikanisa cha Kipapa kwa ajili ya kuzinduliwa Mwaka wa Mahakama ambamo pia ameshiriki Waziri Mkuu wa Italia,  Bwana Mario Draghi ambaye mara baada ya misa amebaki kwa kutafakari kidogo. Wakati wa mahubiri yake Kardinali Parolin, akitafakari Injili ya Siku kutoka Yohane 11, 45-56, iliyokuwa inahusu uamuzi wa Mahakama kutaka kumuua Yesu, ameufafanua kama mchakato haramu dhahiri wa vurugu na kitendo cha upinzani, kilichoidhinishwa baadaye na woga wa Pilato. Kardinali Parolin amesisitiza kwamba kesi ya Yesu inawakilisha kukataliwa kabisa kwa kile  kitwacho ustaarabu wa kisheria wa leo  hii na  ambamo unaoneesha kama kesi ya haki na mahitaji yake yasiyoweza kuondolewa, na ambayo kila mtu ameitwa katika  haki ya kulinda mali kuu za mtu kama vile  heshima yake, uhuru wake, na maisha yake. Kuanzia hapa ndipo linaibuka  jukumu kubwa la maadili, pia sheria, ambayo wamekabidhiwa katika mchakato, na ambao ni waendeshaji wake, lile jukumu ambalo linapatikana katika kanuni ya uhalali  kwa  kuzingatia  vifaa vyote na matokeo misingi iliyomo na ambayo haiwezi kushindwa.

27 March 2021, 15:11