Tafuta

Vatican News
2019.08.01 Mtakatifu Alfonsi Maria de Liguori 2019.08.01 Mtakatifu Alfonsi Maria de Liguori 

Papa Francisko:Mtakatifu Alfonsi ni mwalimu wa uinjilishaji na maadili ya huruma!

Papa ametuma ujumbe wake katika fursa ya maadhimisho ya miaka 150 tangu Mtakatifu Alfonsi Maria de’ Liguori atangaze kuwa Mwalimu wa Kanisa,kwa hati ya Papa Pio IX kunako tarehe 23 Machi 1871. Katika ujumbe huo anahimiza shirika kufuata mfano wa uongofu kuelekea uchungaji wa huruma.Alihimiza maadili ya kiroho kwani alitambua udhaifu wa watu wake katika sawa na sasa katika kipindi cha janga,akili bandia na tishio la ukosefu wa kidemokrasia.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko ametuma ujumbe wa wake kwa Padre Michael Brehl, C.Ss.R., Mkuu wa Shirika la Mwokozi Mtakatifu na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Alfonsiana kufuatia na fursa ya maadhimisho ya miaka 150 tangu Mtakatifu Alfonsi atangazawe kuwa  Mwalimu wa Kanisa. Papa anaandika kuwa tarehe 23 Machi 1871, Papa Pio IX alimtangaza Mtakatifu  Alfonsi Maria de’ Liguori kuwa Mwalimu wa Kanisa. Katika Hati ya kutangazwa kuwa Mwalimu inaoneshwa wazi juu ya pendekezo la Maadili na Kiroho kutokana na kujua kuelekeza njia dhidi ya  maoni yanayopingana ya ukali na udhaifu. Baada ya miaka hii 150 ya  fursa hii ya furaha, ujumbe wa Mtakatifu Alfonsi Maria de’ Liguori, aliyekuwa ni Askofu, Mwalimu wa Kanisa, na  msimamizi wa wataalimungu maadili na waungamishaji na mtindo wa Kanisa lote linalotoka nje la kimisionari, anaelekeza kwa mara nyingine  kwa nguvu  ile njia mwalimu kwa ajili ya kukaribia dhamiri katika uso mkarimu wa Baba na wokovu ambao Mungu anautoa na kwa kazi ya huruma yake (EG 112).

Papa Fracisko amebainisha kuwa mapendekezo ya kitaalimungu ya Mtakatifu Alfonsi, yanazaliwa kutokana na  usikivu na kupokea kutoka kwa udhaifu wa wanaume na wanawake walioachwa kiroho zaidi. Daktari Mtakatifu, aliyefundishwa katika tabia nzuri ya maadili, alibadilika katika wema kwa njia ya  kusikiliza hali halisi. Uzoefu wa kimisionari katika sehemu za pembezoni za wakati wake, kutafuta walio mbali, na kusikiliza wakati wa maungamo, kuanzisha shirika na kuliongoza Shirika la Mwokozi Mtakatifu  na bado alikuwa na uwajibikaji kama Askofu wa Kanisa Maalum ambao, ulimfikisha kuwa baba na mwalimu wa huruma, uhakika ambao mbingu ya Mungu ni moyo wa binadamu. Ilikuwa ni hatua kwa hatua za uongofu kuelekea kwa uamuzi wa uchungaji kimisionari, mwenye uwezo wa ukaribu na watu, kwa kutambua kuwasindikiza hatua  kwa hatua, kushirikisha kwa dhati maisha hata katikati ya vikwazo na changamoto, vilimsukuma Alfonsi atazame si kwa ugumu tu hata muundo wa kitaalimungu  na kisheria alivyokuwa katika miaka ya mafunzo yake. Hapo awali taalimungu maadli likuwa  kama  alama na ukali fulani, baadaye  ikabadilishwa kuwa njia ya huruma, na nguvu ya uinjilishaji inayoweza kuigwa.

Katika mizozo ya kitaalimungu akipendelea sababu ya mamlaka, hakuacha kuendelea katika uundaji wa kanuni za nadharia, lakini aliruhusu mwenyewe kupingwa na maisha yenyewe. Alikuwa ni wakili wa wachache, wadhaifu na waliokataliwa na jamii ya wakati wake, yeye lakini alitetea haki ya wote, hasa walioachwa zaidi na maskini. Njia hii ilimwongoza kwenye uchaguzi mzuri wa kujiweka katika utumishi wa dhamiri ambazo zinatafuta, licha ya shida elfu, uzuri wa kufanya, kwa sababu ni waamini kwa wito wa Mungu na kwa utakatifu. Mtakatifu Alfonsi alikuwa makini na alikuwa ni mkristo halisi kwa sababu alitambua kuwa katika moyo huo wa Injili kuna maisha ya kijumuiya na jitihada na wengine pamoja  (EG 177). Kutangazwa kwa Injili katika jamii inayobadilika haraka kunahitaji ujasiri wa kusikiliza ukweli, kuelimisha dhamiri kufikiria tofauti, bila kuacha kadiri siku zinavyopita

Papa Francisko anandika kuwa kila tendo la kichungaji lina mizizi yake katika mkutano wa wokovu na Mungu wa uzima, huzaliwa kutokana na kusikiliza maisha na hulishwa na tafakari ya kitaalimungu  ambayo inajua jinsi ya kuchukua maombi ya watu na kuoneesha njia zinazofaa. Kwa kufuatia mfano wa Alphonsi,  Papa anaalika wanataalimungu  wa maadili, wamisionari na waungamishi  kuingia katika uhusiano wa kuishi na watu wa Mungu, na kuangalia uwepo kutoka pembe zao za maisha, kuelewa shida halisi wanazokutana nazo na kusaidia kuponya vidonda, kwa sababu udugu wa kweli anajua jinsi ya kuangalia ukuu  wa mtakatifu wa jirani yako, ambaye anajua jinsi ya kugundua Mungu kwa kila mwanadamu, ambaye anajua jinsi ya kubeba unyanyasaji wa kuishi pamoja kwa kushikamana na upendo wa Mungu, na ambaye anajua kufungua moyo kwa upendo wa kimungu ili kutafuta furaha ya wengine kama Baba yao mwema alivyofanya (EG, n. 92).

Akiwa mwaminifu katika Injili na  mafundisho yake ya maadili kikristo yanaalika kutunza kwa kina na kufundisha daima jibu kwa Mungu ambaye anapenda na anaokoa na kumtambua kupitia wengine na kutoka ndani mwetu ili kutafuta wema wa wote ( EG, 39). Taalimungu Maadili haiwezi kutafakari tu juu ya misingi na sheria, lakini pia inahitaji kubeba maendeleo ya hali h halisi inayoshinda kila wazo (cf. EG, n. 231).  Ndiyo kipaumbele (cf. EG, nn. 34-39) Papa amesisitiza, kwa sababau dhamiri moja ya msingi wa kinadharia, kama anavyokumbusha Mtakatifu Alfonsi, haitoshi kusindikiza na kusaidia dhamiri karika kufanya mang’amuzi ya wema wa kutumiza. Inahitajika kwamba ujuzi uwe wa vitendo kwa kusikiliza na kukaribisha wachache, wadhaifu na wale ambao wanachukuliwa kuwa taka za jamii.

Yote haya ni kwa sababu wengi wa maskini wana uwazi maalum wa imani; wanamhitaji Mungu na hatuwezi kukosa kuwapa urafiki wake, baraka zake, Papa anaongeza kuwa, Neno lake, maadhimisho ya Sakramenti na pendekezo la safari ya ukuaji na kukomaa kwa imani. Chaguo la upendeleo kwa maskini lazima litafsiri sana katika upendeleo na kipaumbele cha kidini” (EG 200). Papa Francisko anasema ni dhamiri iliyokomaa kwa Kanisa moja lililokomaa. Kwani mfano wake, mpyaishaji wa Taalimungi Maadili ulifanya kuwa ulazima wa kisindikiza  na kusaidia kiroho katika safari kuelekea wokovu. Mzizi wa Kiini unakwenda kinyume na udhaifu wa mtu, Ni lzaima kutafatu daima njia ambazo hazipeleki mbali bali  zinazokaribia mioyo kwa Mungu na kwa maana hiyo alifanya hivyo Alfonsi kwa njia ya mafundisho yake ya Kiroho na Maadili.

Papa Francisko amesema kama Alfonsi wote tunaalikwa kwenda kukutana na watu kama jumuiya ya kitume ambayo inamfuata Mwokozi kati ya walioachwa. Hii ya kwenda kukutana ni kwa yule hasiye na msaada wa kiroho ili asaidiwe kushinda maadili ya kibinafsi na kuhamasisha ukomavu wa maadili yenye uwezo wa kuchagua wema wa kweli. Kuunda dhamiri zinazowajibika na huruma ndipo tutakuwa na Kanisa komavu lenye uwezo wa kujibu kwa kujenga udhaifu wa kijamii katika matazamio ya ufalme wa Mbingu. Kuna haja ya kwenda kinyume na udhaifu huo ili kupambana na mizizi za ushindani na sheria za wenye nguvu ambao wanafikiri kuwa binadamu ni kama wema wa kutumia yaani kutumia na baadaye kutupa kwa kuanzisha utamaduni wa kibaguzi (Eg 53). Ole wetu ikiwa jitihada za uinjilishaji zinatenganishwa na kilio cha maskini kutoka kilio cha dunia. Papa aidha anasema katika kipindi hiki cha mwisho changamoto ambazo jamii inaendelea kukabiliana nazo ni nyingi, kuanzia na janga la corona, na kazi katika ulimwengu baada ya covid, uhakikisho wa tiba kwa wote ulinzi wa maisha, njia mpya za kiteknolojia kama vile akili bandia, utunzaji wa kazi ya uumbaji, vitisho vya kidemokrasia na dharura ya udugu.

Mtaatifu Alfonsi de’ Liguori, mwalimu na msimamizi wa waungamishi na wanamaadili alitoa majibu ya kujenga katika changamoto za kijamii za wakati wake, kwa njia ya uinjishaji wa watu akielekeza mtindo wa taalimungu maadili yenye uwezo wa kuweka pamoja dharura za Injili na za udhaifu wa kibinadamu. Papa Francisko anawalika kwa maana hiyo kuwa na mfano wa Mtakatifu Daktari katika kukabiliana kwa ngazi ya taalimungu maadili kilio cha Mungu ambacho kinauliza swali wote yuko wapi ndugu yako? (Mw 4, 9). Yuko wapi ndugu yako mtumwa?  Yuko wapi ambaye unamuua kila siku katika kiwanda cha watu wasio na vibali, katika mtandao  wa ukahaba, katika watoto ambao wanatumiwa kwenye vita, na yule ambaye anatakiwa afanye kazi amejicha kwa kuwa hana uhalali (EG, n. 211).  Mbele ya  hatua za kizamani kama za sasa, inaonesha wazi kuwa kuna tishio na hatari za kusuluhisha za hali ya nguvu kwa kusahau walio na mahitaji zaidi Papa Francisko anawaalika kwenda kukutana na ndugu kaka na dada wadhaifu wa jamii zetu, kama alivyo fanya Mtakatifu Alfonsi. Hii ndiyo inapelekea maendele ya tafakari ya taalimungu maadili na matendo ya kichungaji, yenye uwezo wa kufanya jitihada kwa ajili ya wema wa pamoja ambao ndiyo mzizi wa tangazo la Kergma na ambalo ni neno la uamuzi katika kulinda maisha kuelekea uumbaji na udugu.

23 March 2021, 14:48