Tafuta

Kila tarehe 22 Machi ni Siku ya Kimataifa ya Maji: Maji  safi na salama ni muhimu. Kila tarehe 22 Machi ni Siku ya Kimataifa ya Maji: Maji safi na salama ni muhimu. 

Papa Francisko:Maji safi na salama ni kwa wote!

Mara baada ya Sala ya Maika wa Bwana,Papa Francisko amekumbuka:Siku ya kimataifa ya Maji ifayikayo kila tarehe 22 Machi ambayo inaalika kutafakari zawadi hiyo msingi ya kushangaza na Siku ya Kumbukumbu na jitihada za kukumbuka waathirwa wasio na hatia waliouwa na mafia nchini Italia ifanyikayo mwezi Machi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya sala ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 21 Machi 2021, ikiwa ni Dominika ya tano ya kipindi cha Kwaresima, Papa Francisko mawazo yake yamewaendea nchini Italia ambao leo hii wanakumbuka waathiriwa wa Mafia. Papa amesema “Leo hi inchini Italia inaadhimisha Siku ya kumbu kumbu na jitihada ya kukumbuka waathiriwa wasio na hatia wa mafia, Mafia ipo katika sehemu mbali mbali za ulimwengu na kwa kutumia fursa ya janga, wanajitajirisha kwa ufisadi. Mtakatifu Paulo II alitangaza kuwa wao ni utamaduni wa kifo, na Papa Benedikto XVI akasema ni kama njia za kifo. Miundo hii ya dhambi yaani miundo ya mafia, ni kunyume na Injili ya Kristo kwani wanabadilisha imani katika muungu. Leo hii tufanye kumbu kumbu kwa ajili ya waathiriwa wote na kupyaisha jitihada zetu za kupambana dhidi ya mafia hizo.”

Ikumbukwe kuwa muundo huo wa mafie ni aina fulani ya uhalifu mkubwa na mbaya sana katika jamii nyingi za ulimwengu. Kuna aina nyingi za kimafya au kihalifu kama vile biashara haramu za silaha, ngono, madawa ya kulevya, usafirishaji wa wat una hata uhamiaji wa kupangwa, unyonyaji na uhalifu mwingine kinyume na sheria

Dada maji sio bidhaa:ni ishara ya ulimwengu na chanzo cha maisha na afya

Kesho ni Siku ya Maji Duniani, ambayo inatualika kutafakari juu ya thamani ya zawadi hii nzuri na isiyoweza kubadilishwa kutoka kwa Mungu. Kwetu sisi waamini, “dada maji” sio bidhaa: ni ishara ya ulimwengu na chanzo cha maisha na afya. Ndugu wengi, sana, kaka na dada wengi wanapata maji kidogo na labda yaliyo machafu. Papa Francisko amesema “Inahitajika kuhakikisha maji ya kunywa na usafi wa mazingira kwa wote. Nina washukuru na kuwatia moyo wale ambao, kwa ustadi na majukumu tofauti ya kitaalam, wanafanya kazi kwa kusudi hili muhimu sana. Ninafikiria, kwa mfano, wa Chuo Kikuu cha Maji, katika nchi yangu, kwa wale wanaofanya kazi ya kupeleka mbele na kuwafanya watu waelewe umuhimu wa maji. Asante sana kwa ninyi Waargentina ambao mnafanya kazi katika Chuo Kikuu hiki cha Maji”. Aidha amewasalimia wote ambao wameunganishwa kupitia vyombo vya habari kwa namna ya pekee wagonjwa na watu walio na upweke. Amewatakia Dominika njema, lakini basi wasisahau kusali kwa ajili yake.

21 March 2021, 14:49