Tafuta

2021.03.25  Mtunzi maarufu na mshairi Dante Alighieri  anajulikana na kazi yake iitwayo 'Divina Commedia'. 2021.03.25 Mtunzi maarufu na mshairi Dante Alighieri anajulikana na kazi yake iitwayo 'Divina Commedia'. 

Papa Francisko:Dante ni nabii wa matumaini na nabii wa huruma!

Katika barua ya kitume “Candor lucis aeternae”iliyochapishwa leo,Papa Francisko anakumbusha miaka 700 tangu kifo cha mshairi Dante Alighieri akizingatia hali halisi ya sasa,umilele na imani ya kina iliyomo kwenye utunzi wa “Divina Commedia”.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Baada ya miaka 700 tangu kifo kilichotokea mnamo mwaka 1321 huko Ravenna Italia akiwa uhamishoni na uchungu kutoka katika mji wake Firenze alioupenda, Dante bado anazungumza nasi. Anazungumza na sisi wanaume na wanawake wa leo hii na kutuomba kwamba si kuwa tumesoma na kujifunza, lakini hata zaidi kusikiliza na kuiga katika mchakato wake wa safari ya  kuelekea furaha yaani upendo usio na mwisho na wa umilele wa Mungu.  Hivyo ndivyo fursa ya siku kuu ya Kupashwa Habari Bikira Maria kuwa atakuwa mama wa Bwana. Tarehe ya kuchapishwa kwake siyo kwa bahati mbaya, kwa maana katika fumbo la Mungu kufanyika Mwili, kutokana na kiitikio cha: “Tazama mimi hapa” ya Maria ndiyo hasa Papa anaeleza kiini cha kuandika na msingi cha Mtunzi wa Kitabu cha “Divina Commedia” ambacho kinaonesha na kuthibitisha umungu au maajabu ya kubadilishana kati ya Mungu ambaye anaingia katika historia yetu kwa kujifanya mtu na ubinadamu unapata kutoka kwake Mungu furaha ya kweli.

Barua ya kitume ya Papa Francisko imegawanyika katika sura 9, ambapo inafunguliwa kwa mhutasari ambao Papa Francisko anatoa mawazo tofauti ya Mapapa kuhusu Dante Alghieri ambaye ni mtunzi huyo wa kitabu. Kwa maana hiyo Papa anazingatia sana kuhusu maisha ya Alighieri, akimfafananisha na hali ya binadamu na kusisitiza hali halisi ya sasa na umilele wa kazi yake. Katika yeye ni sehemu fungamani ya utamaduni wetu, anaandika Papa, na kwamba anaturudisha kuona mizizi ya kikristo ya Ulaya na Mashariki.  Anawakilisha urithi wa mawazo na thamani zinazopendekezwa hata leo hii, ya Kanisa na jamii ya raia kama msingi wa kuishi kibinadamu ili tuweze na lazima kujitambua kuwa sisi sote ni ndugu.

Misingi miwili muhimu ya kitabu cha “Divina Commedia” au tuseme shauku iliyowekwa katika roho ya mwanadamu na furaha, ambayo ni maono ya upendo ambao ni Mungu. Kwa maana hiyo Papa anaeleza kwamba, Dante ni nabii wa matumaini kwa sabahu katika kazi yake inasukuma kwenye ubinadamu wa kujikomboa kutoka katika utumwa mweusi wa dhambi ili kupata njia stahiki na kuweza kwa namna hiyo kufika katika maisha ya historia na heri ya milele kwa Mungu. Mchakato wa safari iliyoelekezwa na Dante, ambayo ni  hija ya kweli na hakika anabainisha Papa kuwa ni halisi na iwezekanayo kwa wote kwa sababu huruma ya Mungu imetolewa daima na uwezekano wa kubadilika na kuongoka.

Barua ya kitume zaidi inabainisha  mambo mengine matatu ya sura ya Kike katika Kitabu hicho cha “Divina Commedia”. Kwanza  Maria,  Mama wa Mungu ni mfano wa upendo. Beatrice katika kitabu ni ishara ya Tumani na Mtakatifu Lucia anawakilisha imani. Wanwake hawa watatu ambao wanaturudisha katika fadhila tatu za kitaalimungu Papa anaandika  wanamsindikiza Dante katika hatua tofauti za hija yake zilizojionesha kutokana na kwamba haiwezekani kujikomboa peke yetu, lakini ni lazima  na kwa msaada wa yule anayeweza kutusaidia, na kutuongoza kwa hekima na busara. Kilichomfanya kuwatumia María, Beatrice na Lucia kwa hakika ni upendo wa kimungu daima ambao ndiyo kisima pekee ambacho kinaweza kutupatia wokovu. Kwa kupyaishwa maisha na furaha, Papa Francisko anabainisha.

Katika kipengele kingine Papa anajikita katika sura ya Mtakatifu Francis wa Assisi, ambaye katika kazi ya mtunzi huyo Dante amemfananisha katika Mwanga wa wenyeheri”. Kati ya Maskini wa Assisi na Mtunzi mkuu, Papa anatambua maelewano ya kina yaliyopo ambayo katika hao wawili wanawaelekeza watu. Kwanza kwenda katikati ya watu, pili, kuchagua kutumia lugha asili ya watu inayotumia na wote na siyo kilatino. Wote wawili zaidi Papa anaandika wanafungulia uzoefu na wa thamani ya Uumbaji, kioo cha Muumbaji wake. Msanii ni gwiji, ambaye ubinadamu wake bado ni wenye thamani ya sasa, ambapo huyo Alghieri pia ni mfuasi wa utamaduni wetu  wa vyombo vya habari zetu, kwa sababu katika kazi yake kuna mchanganyiko wa maneno na picha, ishara na milio ambayo inaunda ujumbe mmoja.

Papa Francisko katika Barua ya kitume kwa kuwapongeza walimu ambao wanaweza kuwasilisha kwa shauku kubwa ujumbe wa Dante, na tunu ya utamaduni, dini na maadili ya kazi yake, anaomba lakini kwamba urithi huo usibaki umefungwa katika madarasa ya shule na vyuo vikuu, badala yake uweze kujulikana na kusambazwa shukrani kwa jitihada za jumuiya ya kikristo na vyama vya kiutamaduni.

Hata kwa wasanii ambao wanaalikwa kujikita ndani mwake, Papa Francisko anawatia moyo ili kutoa muundo katika ushairi wa Dante kwa  njia ndefu ya uzoefu, kwa namna ya kusambaza ujumbe wa amani, uhuru na udugu. Ni kazi ambayo kamwe kama wakati wote wa hija  haujawahi  kutokea katika wakati wa kihistoria  wa sasa ambao umezingirwa na vivuli, uharibifu, na ukosefu wa imani ya wakati ujao, mesisitiza Papa. Katika kuhitimisha, Barua ya Kitume, Papa anasema Mshairi huyo kwa maana hiyo anaweza kutusaidia kutusukuma mbele kwa utulivu na ujasiri katika hija ya maisha na imani ili moyo wetu uweze kupata amani na furaha ya kweli, upendo ambao unatingisha  jua na nyota.

25 March 2021, 16:05