Tafuta

Vatican News
2020.03.27  Sala ya Papa Francisko na Baraka ya Urbi et Orbi 2020.03.27 Sala ya Papa Francisko na Baraka ya Urbi et Orbi  (Vatican Media)

Mwaka mmoja uliopita Papa alisali kwa mungu kwa ajili ya ubinadamu wote

Ilikuwa ni tarehe 27 Machi 2020,Papa Francisko alisali akiwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro bila kuwa na mtu.Ilikuwa kama jangwa na wakati huo huo kubainisha kuwa ubinadamu umekumbwa na dhoruba.Alihitimisha kwa Baraka ya Urbi et Orbi.Baada ya miezi 12 tangu siku hiyo,bado kuna umuhimu wa kuendeleza maombi zaidi kutokana na janga ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Haitasahulika siku ile maalum ambayo Papa Francisko mnamo tarehe 27 Machi 2020 alitumia wakati wake kwa ajili ya maombi maalum katika uwanja uliokuwa ni mtupu wa Mtakatifu Petro, mvua ikinyesha na kutangazwa moja kwa moja kwa njia ya luninga. Siku hiyo ulimwengu mzima ulikuwa unachungulia katika madhirisha tu kutokana na janga la kihistoria katika karne hii na ambalo halitasahulika kamwe. Hata hilivyo ilikuwa ni tarehe 22 Machi 2020, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa alitoa taarifa kuhusu wakati maalum wa sala na kusema:

“Ijumaa tarehe 27 Machi saa 12.00,  jioni masaa ya Ulaya nitafanya maombi katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Tangu sasa ninawaalikeni nyote kushiriki kiroho kwa njia ya vyombo vya mawasiliano. Tutasikiliza Neno la Mungu, tutainua maombi yetu, tutaabudu Ekaristi Takatifu, na hatimaye ninatoa Baraka ya Urbi et Orbi na kutakuwapo na uwezekano wa kupokea msamaha wa dhambi ( Undulgenzia plenaria)”.

Waamini wote kusali na kujandalia ushindi wa Kristo Mfufuka

Vile vile Papa alisema:  “Ili kuweza kuunganisha sauti juu mbinguni kwa wakristo wote ninawaalika viongozi wote wa Makanisa na viongozi wa jumuiya zote za kikristo kwa pamoja na wakristo wa madhehebu  mbalimbali kumwomba Mwenyezi Mungu aliye juu, kwa kusali wakati mmoja kwa sala ambayo Bwana wetu Yesu alitufundisha. Ninawaalika kusali sala ya ‘Baba Yetu’ siku ya Jumatano tarehe 25 Machi saa 6.00 mchana. Ni siku ambayo wakristo wengi wanakumbuka upashanaji wa habari kwake Bikira Maria kwa Neno aliyefanyika Mwili, ili aweze kusikiliza maombi ya pamoja na wafuasi wake wote ambao wanajiandaa kuadhimisha ushindi wa Kristo Mfufuka.

Papa alisali ili janga liishe:Bwana usituache kwenye dhoruba

Katika siku hiyo ya maombi ,  mara baada ya somo la Injili ya Marko, Papa alitoa mahubiri marefu  ambayo yalikuwa yanaelezea hali halisi ya waamini kwa wakati ule: wakiwa na upweke, wanaogopa , wamejikunja na uchungu: “ Katika kifungu cha Injili iliyochaguliwa kwa siku hiyo, Yesu anawaambia wanafunzi wake kuvuka kwenda pwani nyingine. Baada ya dhoruba kubwa, Kristo anaamshwa na wanafunzi ambao wanaogopa kupotea. Licha ya msukosuko na zogo, Yesu analala kwa amani, akiwa na imani na Baba. Baadaye upepo unasimama na maji yanatulia. Yesu anawaambia wanafunzi wake maneno haya:

“Kwa nini mnaogopa? Bado hamna imani? ”. Hata leo, Papa anasema, tunaishi katika wakati uliiosongwa na dhoruba: Kwa wiki sasa inaonekana kuwa jioni imeshuka. Giza nene limetanda juu ya viwanja vyetu, barabara na miji; na kutawala na kuchukua  maisha yetu, kwa kujazwa kila kitu ukimya wa kutuliza na utupu wa ukiwa, ambao unapooza kila kitu katika njia yake; inahisiwa katika ishara, na mitazamo inaonesha

Tumejikuta tukiogopa na kupoteza. Kama wanafunzi wa Injili, tulinyakuliwa na dhoruba isiyotarajiwa na kali. Tuligundua kuwa tulikuwa kwenye mtumbwi mmoja, wote tikuwa dhaifu na wenye kuchanganyikiwa, lakini wakati huo huo ni muhimu na lazima, wote tumeitwa kusonga mbele pamoja, na tukihitaji kufarijiana. Kwenye mtumbwi huu kwa maana sisi sote tupo ndani mwake.” Na itakumbukwa siku ile wakati wa maombi  Papa akitazama msalaba na akiwa anapanda ngazi taratibu kuelekea Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mahali ambapo aliweza kusali mbele ya Ekaristi Takatifu na kuiombea Roma, Italia na ulimwengu wote.

27 March 2021, 14:34