Tafuta

Vatican News
2021-03-13 Miaka 8 tangu kuchaguliwa Papa Francisko 2021-03-13 Miaka 8 tangu kuchaguliwa Papa Francisko  

Miaka 8 na Papa Francisko:Furaha ya Injili kwa ulimwengu wote

Tarehe 13 Machi 2013 Jorge Mario Bergoglio alichaguliwa kuwa Kharifa wa Mtume Petro;Papa wa kwanza Mjesuit,Mmarekani na wa kwanza kuitwa jina la Francisko.Katika miaka hii nane ya Upapa, umejionesha mambo mengi na mageuzi yanayowahusu wakristo wote katika uzinduzi mpya wa kimisionari kwa lengo la kupeleka upendo wa Yesu kwa ubindamu wote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ukaribu, umoja na uzinduzi wa kimisionari, ndizo ncha muhimu za Upapa  wa Francisko, aliyechaguliwa miaka 8 iliyopita katika kiti cha Petro.  Matazamio ya Upapa wake yanaanzia chini kabisa,  kwa umakini wa sehemu za pembezoni mwa maisha ya binadamu na kijiografia ambazo zimeonesha bayana msimamo wake. Kwa hili amekuwa akiwaalika kurudia asili ya Injili ya Yesu, amewaomba waamini wawe na mwamko mpya, ari mpya kwa sababu ya upendo wa Yesu uweze kuwafikia kweli watu wote. Shauku ya Papa ni Kanisa linalotoka nje, lenye milango iliyo wazi, hospitali iliyo wazi katika kambi na ambalo haliogopi mapinduzi ya huruma na wala miujiza ya ukarimu.

Ni Papa wa kwanza kuitwa jina la Francisko, mjesuit wa kwanza na Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini! Kama hiyo haitoshi ni upapa wa kwanza katika nyakati za kisasa kuchaguliwa baada ya mtangulizi wake kung’atuka katika shughuli za uchungaji. Tulimwona jinsi alivyo anza upapa wake katika hali halisi ya mambo mapya. Jambo linalokumbusha zaidi ni Misa za kila siku katika nyumba ya Mtakatifu Marta, Vatican, mahali alipoamua hata kuishi; na hili ni jambo jipya kabisa katika mapapa wengine waliomtangulia.

Katika misa zake za kila siku alionekana akitoa mahubiri yake mafupi bila kusoma, ambao unakuwa mtindo wa kiparoko, hivyo Papa alizindua mazungumzo ya moja kwa moja na waamini akiwashauri kukabiliana moja kwa moja na Neno la Mungu. Mara kwa mara ameomba pia hata kutoa zawadi ya Biblia ndogo huku akiwakumbusha kubeba Neno la Mungu kila mahali zaidi ya kubeba simu ya mkononi.

Mwaka 2013 alipochaguliwa, unakumbushwa kuchapishwa kwa Wosia wake wa kitume wa “Evangelii gaudium”, ambao tunaweza kusema ndiyo mpango mzima au mwelekeo wa Upapa mpya. Papa Francisko anawaalika kuwa na uinjilishaji mpya wenye tabia ya furaha, ikiwa ni pamoja na mageuzi ya muundo wa kikanisa na uongofu wa kipapa ili wote waweze kuwa wamisionari kwa sababu ya kumpendeza Yesu kama alivyozindua utume wake! Kwa kufanya hivyo mwaka huo huo 2013 , Papa alianzisha Baraza la Makardinali washauri wenye shughuli ya kuchunguza mpango wa kusasisha Katiba ya Kitume “Pastor bonus” ya mwaka 1988. Makardinali hao wanamsaidia Papa katika Ushauri na ambapo mikutano yao inafanyika kila mara. Ni mambo mengi sana kwa miaka 8 ya Upapa ambayo yameonekana na yanendelea kufanywa licha ya kipindi kigumu cha majaribu ya janga la ulimwengu.

Hadi sasa Papa Francisko amefanya ziara 25 nchini Italia na nje ya nchi  33. Lakini katika Upapa wake, amefanya mikutano yake zaidi ya 340, Sala ya Malaika wa Bwana, Malaika wa mbingu 450; mahubiri karibu 790 katika nyumba ya Mtakatifu Marta na kuidhinisha hati ya watakatifu wapya 900, wakiwemo wafiadni 800 wa  Otranto.  Papa Francisko amefanya mikutano 7 ya makardinali , kwa kuwachagua makardinali wapya 101 na kutangaza miaka maalum kama vile: “Mwaka wa kitawa  (2015-2016), wa sasa wa Mtakatifu Yosefu (2020–2021) wa Familia-Amoris Laetitia (2021-2022). Papa Francisko ameanzisha Siku ya Kimataifa mbali mbali, kwa kutaja ya  mwisho:“ Siku ya Babu/bibi na wazee, itakayo adhimishwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai 2021, katika sikukuu ya Mtakatifu Joakimu na Anna babu na bibi wa Yesu. 

13 March 2021, 09:09