Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza kwa sala na sadaka zao wakati wa hija yake ya kitume nchini Iraq. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza kwa sala na sadaka zao wakati wa hija yake ya kitume nchini Iraq. 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Iraq: Msaada wa Sala!

Baba Mtakatifu ametumia fursa hii, kuwaomba waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza kwa sala na sadaka zao katika hija hii ya Kitume ili iweze kuzaa matunda yanayokusudiwa. Watu wa Mungu nchini Iraq wanawasubiri viongozi wa Kanisa kwa hamu kuu. Walimsubiri Mtakatifu Yohane Paulo II, hija hiyo ikagonga mwamba na kushindikana. Sasa Hapana!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Iraq, kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021 inanogeshwa na kauli mbiu “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu” Mt. 23:8. Ni hija inayofumbata mambo makuu matatu: Ukaribu wa Baba Mtakatifu kwa Wakristo nchini Iraq, uhamasishaji wa ujenzi wa Iraq mpya katika haki na usawa na kuendeleza mchakato wa majadiliano ya kidini ili kudumisha udugu wa kibinadamu kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Baba Mtakatifu wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 3 Machi 2021 amewaambia waamini kwamba, Ijumaa tarehe 5 Machi 2021 anaanza hija yake ya kitume, ili kukutana na watu wa Mungu nchini Iraq. Hawa ni watu ambao wameteseka sana. Anataka kukutana na waamini wa Kanisa la Mashuhuda wa imani katika Nchi ya Ibrahimu Baba wa Imani. Kwa kuungana na viongozi wengine wa kidini, anapania kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini na kiekumene kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa umoja, upendo, mshikamano na udugu wa kibinadamu miongoni mwa waamini wa dini mbalimbali.

Baba Mtakatifu ametumia fursa hii, kuwaomba waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza kwa sala na sadaka zao katika hija hii ya Kitume ili iweze kuzaa matunda yanayokusudiwa. Watu wa Mungu nchini Iraq wanawasubiri viongozi wa Kanisa kwa hamu kuu. Walimsubiri Mtakatifu Yohane Paulo II, hija hiyo ikagonga mwamba na kushindikana. Haiwezekani hata kidogo kuendelea “kupukutisha" matumaini ya watu wa Mungu nchini Iraq sanjari na kuwakatisha tamaa kwa mara ya pili! Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusali kwa bidii ili safari hii iweze kupata mafanikio makubwa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini humo.

Papa Sala Iraq
03 March 2021, 16:32