Tafuta

Papa Francisko aombea amani Iraq,Mashariki ya Kati na ulimwengu

Ni picha na maneno yanayohusu Hija ya Kitume ya Papa Francisko ambayo yameongoza tafakari ya Katekesi akiombea amani nchini Iraq,Mashariki ya Kati na ulimwengu mzima.Hata hivyo katika katekesi yake amesema“Nimehisi maana ya toba katika hija hiyo na wakati huo huo kuona furaha iliyonizunguka ya mapokezi ya mjumbe wa Kristo”.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Katika maneno yake kwenye video fupi wakati wa katekesi Jumatano tarehe 10 Machi 2021, Papa amesema “Ndugu kaka na dada, tusifu Mungu kwa ajili ya historia ya ziara hii na kuendelea kusali kwa ajili ya Nchi ile na kwa ajili ya Mashariki ya Kati. Nchini Iraq, licha ya kishindo cha uharibifu na silaha, mitende, ishara ya nchi na matumaini yake, imeendelea kukua na kuzaa matunda. Ndivyo ilivyo kwa udugu: kama matunda ya mitende, haitoi kelele, lakini mtende unazaa na hutukuza. Mungu, ambaye ni amani, aipe  wakati ujao wa udugu nchi ya Iraq, Mashariki ya Kati na ulimwengu wote”

Salamu za Papa

Papa Francisko mara baada ya katkesi yake, amesalimia waamini wote kwa lugha mbali mbali, akiwa katika maktaba ya kitume jijini Vatican. Katika lugha ya kiitaliano amewaomba kunedelea na njia ya Kwaresima kwa kuacha waongozwe na matendo ya Roho Mtakatifu ambaye anawongoza katika nyayo za Kristo kuelekea Yerusalemu, mahli ambapo Yeye atatimiza utume wake wa wokovu.

Uongofu na toba

Wazo kama kawaida limewaendea hatima ye kwa wazee. vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Kwa kila mmoja anamwombea neema ya Mungu ili katika ujana, iwe katika uzee, wagonjwa, wanaweza kufikia furaha ya Pasaka kwa kujihusisha katika safari ya uongofu na ya toba ambayo tunaishi katika kupindi hiki. Kwa wote amewapa Baraka yake.

10 March 2021, 13:25