Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu amemteua  Askofu mkuu Alain Paul Charles Lebeaupin kuwa Mshauri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu amemteua Askofu mkuu Alain Paul Charles Lebeaupin kuwa Mshauri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican.  (ANSA)

Askofu mkuu Alain P. C. Lebeaupin, Mshauri Mambo ya Nje Vatican

Askofu mkuu Alain Lebeaupin alizaliwa tarehe 2 Machi 1945. Baada masomo yake tarehe 28 Juni 1975 alipewa daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 7 Desemba 1998, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Ecuador na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu. Tarehe 6 Januari 1999 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu: Ecuador, Kenya na Umoja wa Ulaya

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Alain Paul Charles Lebeaupin kuwa mtaalam mshauri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Alain Paul Charles Lebeaupin alizaliwa tarehe 2 Machi 1945 huko Paris, nchini Ufaransa. Baada masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 28 Juni 1975 alipewa daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki la Nice, nchini Ufaransa. Tarehe 7 Desemba 1998, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Ecuador na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu.

Tarehe 6 Januari 1999 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe 14 Januari 2005 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Kenya na Mwakilishi wa Vatican kwenye Makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi,  UN-Habitat pamoja na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP). Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe tarehe 23 Januari 2012 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican kwenye Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, EU. Tarehe 16 Novemba 2020 akang’atuka rasmi kutoka madarakani. Ilipogota tarehe 27 Machi 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa mtaalam mshauri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican.

Mshauri

 

29 March 2021, 14:35