Tafuta

2021.02.08 Papa Francisko amehutubia viongozi wa kidiplomasia na wawakilishi mjini Vatican 2021.02.08 Papa Francisko amehutubia viongozi wa kidiplomasia na wawakilishi mjini Vatican 

Papa Francisko:udugu ndiyo njia muafaka katika migogoro na migawanyiko leo hii!

Papa Francisko amekutana na Mabalozi na wawakilishi wa Vatican katika fursa ya kutakiana heri na baraka za Mwaka Mpya ambapo baada ya kueleza yale yaliyotendeka mwaka jana kama vile mikataba ya Vatican na nchi kadhaa, sehemu kubwa ya hotuba hiyo imejikita katika mgogoro mitano inayokumbwa ulimwengu:kiafya,mazingira,uchumi kijamii,kisiasa na uhusiano kibinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko tarehe 8 februari 2021 kwa kukutana kama utamaduni na Mabalozi na wawakilishi wa Vatican katika fursa ya kutakiana heri na baraka ya Mwaka Mpya japo kwa kuchelewa ametoa hotuba yake ndefu  na zaidi kufafanua mambo muhimu yaliyokumba ulimwengu  mwaka jana na kuendelea. Papa Francisko katika hotuba hiyo amejikita kutafanua zaidi migogoro mitano uliyopo ulimwenguni leo hii: mgogoro wa kiafya, wa mazingira, uchumi, kisiasa na husiano wa kibinadamu.  Hata hivyo Papa amebanisha  juu ya yote shauku yake ya kuanza ziara za kitume kuanza na ile ya Iraq ambayo tayari imepangwa. Udugu na tumani ni kama dawa ambazo leo hii Dunia inahitaji sana na chanjo amesema Papa Francisko.

Migogoro ulimwenguni 

Katika kutazama hali halisi ya mgogoro ulimwenguni ambayo kuanzia nchini Siria, Lebanoni, Nchi Takatifu naugaidi kimataifa amegusia kwa njia hiyo hata bara la Amerika, Afrika hadi Ulaya; vile vile hata kugusia nchini Myanmar, katika mgogoro wa siku hizi ambapo Papa amerudia kuomba utayari wa kuweka huru viongozi wa kisasa waliofungwa. Papa Fracisko ameelezea hata kuhusu mkataba wa Vatican na nchi ya China kuhusu kuchaguliwa kwa maaskofu, mkataba ambao hadi sasa ni wa kichungaji na ambao umepyaishwa kwa miaka mingine miwili hivi karibuni. Hakukosa kuelezwa juu ya janga ambalo limeweka wazi migogoro mingi ulimwenguni.  Papa amelezea kuhusu ulimwengu kwamba umegugua lakini si virusi tu bali hata janga limeonesha wazi matokeo ya hatari zaidi ya kuishi kwa kutawaliwa na ubinafsi, utamaduni wa kibaguzi na ambapo amesema kuna pendekezo mbadala au kuendelea na  njia hiyo au kubadili njia nyingine mpya.

 Kulinda maisha kila hatua

Papa amechunguza kila hali ya shida kuanzia ya afya, huku akithibitisha thamani ya kila maisha tangu kutungwa  mimba hadi kifo cha asili, lakini pia akibainisha kuwa, kuna kisingizio cha kuhakikisha haki za madai, idadi kubwa ya sheria ulimwenguni ambazo zinaonekana kuondolea mbali na jukumu muhimu la kulinda maisha ya binadamu katika kila hatua. Fransisko anathibitisha haki ya utunzaji, jukumu la kusaidia maskini, waliotengwa, na juu ya yote ameomba kwamba sio mantiki ya faida inayoongoza uwanja dhaifu kama ule wa huduma ya afya na matibabu. Kwa maana hiyo wito mpya kwa uwajibikaji wa kibinafsi katika vita dhidi ya Covid-19 na kwa serikali ili chanjo ya Covid-19 iwe ya kila mtu: “Ninahimiza Mataifa yote kuchangia kikamilifu katika mipango ya kimataifa inayolenga kuhakikisha usambazaji sawa wa chanjo, sio kulingana na vigezo vya kiuchumi tu, lakini kwa kuzingatia mahitaji ya wote, hasa wale wa watu wanaohitaji sana”.

Mgogoro wa mazingira

Huu ni wakati wa kutenda, kwani tunaweza tayari kugusa kwa mikono yetu athari za kutochukua hatua za muda mrefu. Maneno ya Papa yanatazama mgogoro wa mazingira, kwa ardhi ambayo, wakati wa janga, imeoneesha jinsi udhaifu na inavyohitaji utunzaji. Mgogoro wa mazingira unahitaji suluhisho la muda mrefu na ushirikiano wa kimataifa, ndiyo sababu kuna tarajio la Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP26), uliopangwa kufanyika Novemba ijayo huko Glasgow. Papa Francisko ana wasiwasi juu ya uwezekano wa kutoweka kwa visiwa kadhaa katika Bahari la Pasifiki na uwezekano wa kwamba vijiji na tamaduni zote zinaweza kutoweka. Lakini pia kwa Vietnam na Ufilipino waliokumbwa na mafuriko mazito na moto huko Australia na California kwa sababu ya ongezeko la joto duniani.

Mazungumzo nchini Sudan Kusini

Papa hakusahau bara la Afrika, katika mawazo yake, yanawaendea nchini Burkina Faso, Mali na Niger, na mamilioni ya watu wanaoteseka kwa  njaa, walio katika hatari ya baa la njaa huko Sudan Kusini ambapo zaidi ya watoto milioni wanauhaba wa chakula, wakati mikondo ya  kibinadamu mara nyingi zinakwamishwa na uwepo wa mashirika ya kibinadamu katika eneo hilo kuwa mdogo. Ili kukabiliana na hali hiyo, ni jambo la dharura, kwamba mamlaka ya Sudan Kusini imalize haraka  migogoro ya  kutokuelewana na kuendelea katika mazungumzo ya kisiasa kwa upatanisho kamili kitaifa.

Mapinduzi mapya ya Copernican ya uchumi

Tafakari ya Papa Francisko pia imegusa mantiki mbali mbali ya shida ya kiuchumi na kijamii kwa kuchambua athari za mgogoro kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, upotezaji wa ajira, na shida za familia. Anakumbuka kuwa mgogoro huo umeangazia mfumo unaotegemea unyonyaji na ubadhirifu wa watu na maliasili, ambao umepoteza mtazamo wa mshikamano. Kwa maana hiyo ni kuzindua tena ujumbe wa Uchumi wa Francesco. “Tunahitaji aina ya mapinduzi mapya kama vile ya  Copernican ambayo yaweke uchumi kwa huduma ya mwanadamu na sio kinyume chake, kwa kuanza kusoma na kufanya uchumi tofauti, ambao hunafanya maisha na siyo kuua, unajumuisha na na siyo kutojumuisha kibinadamu na  kumfanya mwanadamu ajidhatiti ubinadamu wake, kutunza  kazi ya uumbaji na siyo kuipora”. Ni wito wa usijifanyie mwenyewe bali kwa, kushirikiana na ushiriki kwa sababu hiyo Papa anaamini kuwa ni muhumu kuwekwa mgao uliopendekezwa na mpango wa kizazi kijacho cha Umoja wa Ulaya (EU) kwa mfano wa kukusanya rasilimali kwa roho ya mshikamano. Na kwamba ni lengo linaloweza kufikiwa kweli.

Mgogoro wa kiuchumi katika jamii na matokeo yake

Upande wa pili wa sarafu ya mgogoro wa uchumi ni ulimwengu wa kukata tamaa ambao unafungua milango kwa kazi isiyo halali au ya kulazimishwa, ukahaba na vitendo vya uhalifu, pamoja na biashara mbaya ya binadamu. Ni matokeo ya ukosefu wa utulivu wa kiuchumi unaosababisha riba na ufisadi na dhuluma nyingine nyingi zinazotumiwa kila siku mbele ya macho ya uchovu na yanayo danganywa na jamii yetu ya kisasa, Papa amebainisha. Hatari nyingine ni uhalifu wa mtandao ambao unalenga watu walio katika mazingira magumu zaidi, ambao pia ni mawindo rahisi ya picha zilizo mbaya kwa watoto.

Dharura za kibinadamu

Jambo jingine ambalo Papa Fracisko amekazia  linahusu kuzorota kwa dharura za kibinadamu pia zinazosababaisha hata na kutengwa na kwa njia hiyo kufungwa kwa mipaka. Papa amefikiria kwa namna ya pekee Sudan ambapo maelfu ya watu wanaokimbia mkoa wa Tigray wamepata hifadhi, pia nchi zingine za Kusini mwa Jangwa la Sahara, au mkoa wa Cabo Delgado nchini Msumbiji, ambapo wengi wamelazimika kuacha eneo lao na sasa wako katika hali mbaya sana. Katika moyo wa Papa Francisko pia amekumbuka Yemen na Siria, ambapo, pamoja na dharura nyingine kubwa, kuna ukosefu wa chakula unaokumba sehemu kubwa ya idadi ya watu na watoto ambap tayari wamechoka na utapiamlo. Papa amerudia kusisitiza juu ya hitaji la kusamehe deni  la nchi maskini, pia  amefafanua kuwa mizozo ya kibinadamu mara nyingi huchochewa na vikwazo vya kiuchumi. Kwa njia hiyo, pamoja na kutambua mantiki ya vikwazo, lakini  Vatican bado haioni ufanisi hata kwa ajili ya kuhamasisha mtiririko wa misaada ya kibinadamu, juu ya dawa na zana za afya, ambazo ni muhimu sana wakati huu wa janga.

08 February 2021, 15:36