Tafuta

Radio ni muhimu sana hasa katika mazingira magumu Radio ni muhimu sana hasa katika mazingira magumu 

Papa:Uzuri wa Radio ni kutokana na kufikia maeneo ya mbali sana

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwenye mtandao wa kijamii anasema Uzuri wa Radio unafikia hata maeneo ya bali. Ni katika muktadha wa siku ya Kimataifa ua Radio iliyonzishwa na Unesco mnamo 2011 kwa ajili ya kukumbuka ujumbe wa kwanza uliotangazwa na Radio ya Umoja wa Mataifa 1946.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ujumbe wa Papa kwa njia ya Mtandao Jumamosi, tarehe 13 Februari 2021 anasema: “uzuri wa radio ni kutokana na kwamba unafikia hata maeneo yaliyo mbali sana”. Ni katika muktadha wa siku ya Kimataifa ya Radio, iliyoanzishwa mnamo 2011 na UNESCO kwa ajili ya kuenzi ujumbe wa kwanza wa habari za umoja wa Mataifa uliotangazwa kunako mwaka 1946.  Ni Radio ambayo hadi sasa inaripoti kila siku kwa lugha nane na kwa zaidi ya vituo elfu mbili vya washirika ulimwenguni. Radio bado inasalia kuwa chombo muhimu cha kuunganisha jamii na kuchangia katika kuendeleza mbele ajenda ya maendeleo endelevu (SDG's).

Umuhimu wa Radio 

Umuhimu wa Radio ni kuwaleta watu pamoja, na zaidi  katika enzi za mageuzi ya haraka ya vyombo vya Habari, Radio inakuwa ni sehemu maalum katika kila jamii kama chanzo cha habari muhimu na taarifa. Lakini radio pia ni chanzo cha uvumbuzi ambao uliendeleza mazungumzo na wasikilizaji na taarifa zilizotokana na watumiaji wa chombo hicho kwa miongo kadhaa kabla ya kuwa maarufu. Radio inatoa taswira nzuri ya utofauti katika mundo wake, lugha zake, na miongoni mwa wataalam wenyewe wa radio. Kwa njia hiyo Radio  inatuma ujumbe muhimu kwa ulimwengu wote. Katika uwanja wa habari za uinjilishaji, Radio imekuwa mchango mkubwa na kupeleka neno la kutia moyo na matumaini kwa dhati. Katika muktadha wa kumbu kumbu ya Miaka 90 ya Radio Vatican, ambayo muundaji wake wa kwanza  Guglielmo Marconi kwa utashi wa Papa  Pio XII, katika nyakati za Vita ya II pili ya  dunia na vita baridi, RadioVatican ilifanya kazi kubwa ya kuwaunganisha familia na wafungwa na kuwatia moyo katika hali yao ngumu waliyokuwa nayo.

Toleo la 2021

Kwa mwaka huu, UNESCO imewaalika watangazaji ulimwenguni kote kuzingatia masuala kadhaa ya mada ndani ya ratiba zake. Mambo matatu msingi: Mageuzi - Ulimwengu unabadilika, radio inakua. Njia ya kudumu na endelevu. Ubunifu - Ulimwengu unabadilika, radio inazoea na inapyaisha, kati ya teknolojia za digitali na uhamaji. Uunganisho - Ulimwengu hubadilika, radio inaunganisha. Jukumu lake ni  msingi wakati wa majanga ya asili, mizozo ya kijamii na kiuchumi, magonjwa ya milipuko, kama vile tunayoishi sasa. (https://en.unesco.org/commemorations/worldradioday)

Papa:Shughuli ya utangazaji habari lazima ikue

Hata hivyo katika ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya 55 ya Mawasiliano kijamii ulimwenguni Papa anasema kwamba kazi ya kutoa habari lazima ikue kwa kukutana na watu mahali na jinsi walivyo. Kwa mujibu wa Papa Francisko, mawasiliano ni mahali pa kukutana, penye umoja unaonafanana na ule mkusanyiko wa mikutano ambao kwa miaka elfu mbili umeturuhusu kuwasiliana na uzuri wa kushangaza wa safari ya Kikristo. Kwa maoni ya Kikristo, radio, kama vyombo vingine vya habari hubadilika ikiwa vinaelekeza kwa mtu huyo, ukweli na ukweli wa maisha yake. Kinyume chake, Papa anaonya juu ya hatari za mawasiliano ambazo zinatokana na kiteknolojia, lakini labda kupoteza uhusiano na mwanadamu, hivyo kuzaa habari iliyowekwa tayari katika ofisi ya wahariri, mbele ya kompyuta, bila kuteketeza nyayo za viatu, bila kwenda nje barabarani, kuona, kukutana, kuthibitisha na kushiriki.

Kwa mujibu wa Papa  Francisko “Tovuti inabaki kuwa fursa ya muda mrefu kama inatumiwa na akili na roho ya kukosoa. Uelewa huu muhimu unasukuma kutobadilisha chombo, lakini kwa uwezo mkubwa wa  kufanya umang’amuzi, akiwa na jukumu la yaliyomo ambayo yamesambazwa na udhibiti ambao tunaweza kutumia pamoja dhidi ya  habari za uwongo, kuzifunua na vile vile, sisi sote tumeitwa kuwa mashuhuda wa ukweli”, anasisitiza Papa Francisko.

13 February 2021, 16:15