Tafuta

Vatican News
Muonekano wa mji Mtakatifu Muonekano wa mji Mtakatifu  

Papa kwa Kamishna ya Nchi Takatifu:muwe mbegu ya udugu!

Tarehe 14 na 15 Februari 2021,Kamishna ya nchi Takatifu inaadhimisha miaka 600 tangu kuundwa kwake,kwa utashi wa Papa Martino V na hati ya utambulisho “His quae pro ecclesiasticarum”.Katika fursa hiyo Papa Francisko amemwandikia barua Padre Patton,(OFM)msimamizi wa nchi Takatifu akimshukuru kwa kazi ambazo watawa hao wanajikita nazo kusaidia Kanisa mahali ambapo Kristo aliishi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika fursa kuadhimisha miaka 600 ya Kamishna ya Nchi Takatifu yenye Hati ya utambulisho “His quae pro ecclesiasticarum” ya Papa Martino V ya tarehe 14 Februari 1421, Papa Francisko amemtumia barua Padre Francesco Patton, OFM, msimamizi wa Nchi Takatifu kwamba tarehe 14 ni siku ya kumbu kumbu ya kuanzishwa utume huo. Baada ya karne hizi 6 za utume wa Kamishna, daima unaendelea kuhitajika hadi sasa katika, kusaidia, kuhamasisha, kuthamanisha utume wa Usimamizi wa Nchi Takatifu  na  kuwezesha kuwa na mtandao wa mahusiano ya Kikanisa, kiroho na upendo kama kitovu cha nchi ambayo Yesu aliishi. Papa Francisko anathibitisha kuunga mkono na kubariki huduma hiyo yeye thamani na kuwatakia kwamba wawe daima mbegu ya udugu. Na kwa wote anawabariki kwa moyo na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

Hata hivyo, naye Padre Francesco Patton, Msimamizi wa Nchi Takatifu, baada ya kupata barua hiyo  amemtumia barua ya shukrani.  Miaka 600 ya Kamishna ya Nchi Takatifu ni Chombo kiliochoundwa ili kusaidia utume katika maeneo ya Yesu. Mwanzoni walipewa dhamana wanashirika wa Mtakatifu  Fransisko wa Assisi na walei. Jukumu lao lilikuwa ni kutafuta misaada ya kiuchumi kwa ajili ya  Nchi  Takatifu. Hivyo ndivyo ilizaliwa sura ya utawala na baadaye ile ya kamishna, kwa mujibu wa maelezo ya Usimamizi wa Nchi  Takatifu. Ni makamishna 67 wanaofanya kazi leo  hii ambao wataadhimisha karne 6 za historia , Jumatatu tarehe 14  na 15 kwa kufanya sherehe za Ekaristi ili kutoa shukrani kwa Mungu na kwa wafadhili wa Nchi Takatifu.

Kwa mujibu wa maelezo yao wanasema,Historia ya kamishna hiyo ilianzia wakati mgumu wa maisha ya usimamizi, mahali ambapo kulikuwa na uhitaji wa msada wa nguvu katika utume wa Nchi Takatifu. Amesema hayo  Padre Marcelo Ariel Cichinelli, mjumbe na msimamizi wa Kamishna ya Nchi Takatifu. Mlei wa kwanza aliyepewa majukumu ya kusimamia alianzia kwenye miaka ya 1392 na ndiye mfanya biashara Ruggero Contarini. Kwa karne nyingi, walei walibadilishwa na wanashirika wa Kifransikani, hadi kufikia kwambaleo hii Kamishina ya nchi Takatifu ni watawa wanaoteuliwa na wakuu wao wa eneo, kwa makubaliano na Msimamizi wa Nchi Takatifu

12 February 2021, 16:18