Tafuta

Vatican News
2021.02.07 Sala ya Malaika wa Bwana 2021.02.07 Sala ya Malaika wa Bwana   (Vatican Media)

Papa Francisko:Utume wa Kanisa ni ukaribu na kuinamia anayeteseka!

Kuinamia wale wanaoteseka na kuwafanya wasimame,kuwatunza kwa upole na huruma ndiyo mtindo na chaguo la upendeleo kutoka kwa Mwana wa Mungu ambao lazima uendelezwe na Kanisa lake.Lakini huruma haiwezi kutekelezwa bila kupata nguvu kutokana na uhusiano wa karibu na Baba.Ndiyo tafakari ya Papa katika Dominika ya V ya Mwaka B,kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Sr. Angela. Rwezaula-Vatican

Kwa mara nyingine katika Uwanja! Injili ya leo (Mk:1,29-39) inawakilisha uponyaji kwa upande wa Yesu akiwa ukweni kwa Petro na baadaye kwa wagonjwa wengi na watu ambao walikuwa wamemzunguka. Kule kwa mkwe wa Petro ulikuwa ni uponywaji wa kwanza kwa mujibu wa kimwili kama anavyoeleza Mwinjili Marko “mwanamke alikuwa kitandani akiwa na homa; mbele yake, tabia na ishara ya Yesu ni zile za kuwa na umakini kwani “ alimkaribia na kumwamsha huku akimshika mikono”. Kuna upole mwingi katika tendo hilo rahisi ambalo utafikiri karibu ni la kawaida.  “Homa ilimwacha na anakaanza kuwahudumia”. Uwezo wa Yesu wa kuponya ahukukumbana na kizingiti chochote; na mtu aliyeponywa alianza mara moja shughuli zake za maisha kama kawaida, kwa kuwafikia wengine haraka na wala si yeye binafsi, hii ina maana kubwa, ni ishara ya kweli ya afya!  Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko, Jumapili tarehe 7 Februari 2021, ikiwa  ni Dominika ya V ya kipindi cha kawaida cha mwaka B. Kwa mara nyingine tena Papa Francisko ametoa tafakari yake akiwa katika dirisha la Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican. Akiendelea na tafakari hiyo amebainisha kwamba siku hiyo  ilikuwa ya sabato. Watu katika kijiji walikuwa wanasubiri jioni na baada  kumalizika ulazima wa kupumzika walikuwa wanatoka  na kumpelekea Yesu wagojwa wote na wenye kupagawa. Na yeye aliwaponya, lakini huku akikataza pepo hao  wasionesha kuwa yeye ni Kristo (Mk 1, 32-34).

Yesu anawakaibia daima wanaoteseka kiroho na kimwili

Tangu mwanzo Yesu alionesha upendeleo wake kwa watu wanaoteseka katika mwili na kiroho; ndiyo upendeleo wa Yesu ambao unakaribia watu ambao wanateseka katika mwili na kiroho. Ni upendeleo wa Baba na ambao yeye anajifanya mwili na kuonesha kwa matendo na maneno.  Wafuasi wake ni mashuhuda wa kweli, waliona hayo na baadaye wakashuhudia. Lakini Yesu hakutaka  mitume wake wawe watazamaji tu, bali aliwahusisha, aliwatuma, aliwapa hata uwezo wa kuponesha wagonjwa na kuondoa pepo wabaya(Mt 10,1;Mk 6,7). Na hiyo iliendelea bila kukatika katika maisha ya Kanisa hadi leo hii. Papa ameongeza kusema kwamba hiyo ni muhimu. Kutunza wagonjwa wa kila aina kwa upande wa Kanisa sio shughuli mbadala, hapana! Siyo jambo la kijuu juu, hapana. Kutunza wagonjwa wa kila aina ni sehemu fungamani ya utume wa Kanisa lake kama ulivyokuwa ule ya Yesu. Na utume huu ni kupeleka huruma ya Mungu kwa ubinadamu unaoteseka. Papa Francisko kwa kufafanua hilo vema amesema “hii itatukumbusha siku siyo nyingi tarehe 11 Februari, ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Wagonjwa duniani.

Hali hasi ya janga tunaloishi linatuelewesha ujumbe huu

Hali halisi ambayo tunaishi ulimwenguni kote kutokana na janga inatufanya kwa namna ya pekee kuelewa ujumbe huu, yaani utume huu msingi wa Kanisa. Sauti ya Ayubu inarudia kusikika tena katika Liturujia ya siku, kwa mara nyingine tena inatafsiriwa katika hali halisi ya maisha yetu ya kibinadamu; na kwa  namna hiyo hali ya  juu katika hadhi ya hali yetu, na ya udhaifu. Mbele ya hali halisi hii daima inachanua katika moyo swali la kwanini? Na katika swali hilo, Yesu ambaye ni  Neno aliyefanyika mwili anajibu si katika mtazamo mmoja, kwa sababu sisi walio na hadhi kuu na hali ya udhaifu, elekeo lake ni  uwepo wa upendo ambao unainama na ambao unanyosha  mkono na kuinua, kama alivyo fanya kwa mkwe wa Petro (Mk 1,31).  Ni kuinama kwa ajili ya  kumwinua mwingine. Papa Francisko ameomba kwa mara nyingine kutosahau kuwa inaruhusiwa kutazama kutoka juu kuangalia chini ikiwa wewe unatoa mkono wako kumnyanyua mwingine. Na ndiyo njia pekee. Ndiyo utume ambao Yesu alikabidhi Kanisa lake. Mwana wa Mungu anajionesha katika ukuu wake, akitazama kutoka juu  kuangalia chini na siyo katika umbali, bali  kwa kuinama, kunyosha mkono; kuonesha ukuu katika ukaribu, upole na huruma.

Ukaribu, upole, uhuruma ni mtindo wa Mungu.

Mungu anajifanya kuwa karibu kwa upole na uhuruma. Ni mara ngapi tunasoma katika Injili, mbele ya tatizo la afya au tatizo lolote: “ alishikwa huruma. Huruma yake Yesi, ukaribu wa Mungu katika Yesu ndiyo mtindo wa Mungu”, amesisitiza Yesu. Injili ya siku inatukumbusha haya kwamba huruma inajikita mizizi yake katika ukina wa uhusiano na Baba. Kabla ya asubuhi na baada ya machweo, Yesu alikuwa anajitenga kando na kubaki pekee akisali( Mk 1,35. Kutoka hapo alikuwa akichota nguvu kwa ajili ya kutimiza huduma yake  akihubiri na kuponya. Bikira Mtakatifu atusaidie kuacha tuponeshwe na Yesu, kwa maana tunahitaji daima na wote kuweza kwa  mara nyingine kuwa mashuhuda wa huruma inayoponesha ya Mungu.

07 February 2021, 15:00