Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko kuanzia Jumapili tarehe 7 Februari 2021 anaanza tena kutoa tafakari na kusali pamoja na waamini na mahujaji kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko kuanzia Jumapili tarehe 7 Februari 2021 anaanza tena kutoa tafakari na kusali pamoja na waamini na mahujaji kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.  (ANSA)

Papa Francisko: Sala ya Malaika wa Bwana: St. Peter's Square!

Ili kuendelea kuwaimarisha ndugu zake katika imani, matumaini na mapendo hasa katika kipindi hiki cha maambukizi makubwa ya UVIKO-19, Baba Mtakatifu Francisko kuanzia Jumapili tarehe 7 Februari 2021 ataanza tena kusali na waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema Sala ya Malaika wa Bwana, kutoka kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanasema, ili Kristo Yesu, Bwana na Mwalimu aweze kulichunga na kuzidi kuliongeza Taifa la Mungu aliweka katika Kanisa lake huduma mbalimbali, zinazolenga wema wa Fumbo la Mwili wake, yaani Kanisa. Wahudumu hawa waliopewa uwezo mtakatifu wanawatumikia ndugu zao, ili watu wote wa Mungu waweze kuufikia wokovu. Kristo Yesu aliwachagua Mitume na ili kusudi Uaskofu wenyewe uwe mmoja na usiogawanyika, akamweka Mtakatifu Petro juu ya Mitume wengine wote na katkka yeye akatia chanzo na msingi udumuo na unaoonekana wa umoja wa imani na wa ushirika. Baba Mtakatifu anatekeleza dhama na utume wake wa kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kwa njia ya nyaraka, barua binafsi, mahubiri, katekesi na tafakari; mambo yanayonafsishwa katika maisha na utume wa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Tangu kuzuka kwa janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19, (COVID-19), shughuli nyingi za Baba Mtakatifu zilizisitishwa ili kutekeleza itifaki inayopania kuzuia maambukizi ya UVIKO-19. Badala yake, Baba Mtakatifu ameendelea kutoa katekesi na tafakari ya Sala ya Malaika wa Bwana kutoka kwenye Maktaba yake binafsi iliyoko kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha, mjini Vatican. Mara ya mwisho kwa Baba Mtakatifu Francisko kuonekana kwenye dirisha la Uwanja wa Kanisa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, ilikuwa ni tarehe 20 Desemba 2021. Ili kuendelea kuwaimarisha ndugu zake katika imani, matumaini na mapendo hasa katika kipindi hiki cha maambukizi makubwa ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19, (COVID-19), Baba Mtakatifu Francisko ameamua kwamba, kuanzia Jumapili tarehe 7 Februari 2021 ataanza tena kusali na kutafakari na waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema Sala ya Malaika wa Bwana, kutoka kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. 

Angelus

 

 

06 February 2021, 07:30