Tafuta

Vatican News
2021.02.10 Katekesi ya Papa Francisko kupitia Maktaba ya kitume, Vatican 2021.02.10 Katekesi ya Papa Francisko kupitia Maktaba ya kitume, Vatican  (Vatican Media)

Papa Francisko:Mungu anakutana nasi katika kila maisha tunayoishi

Sala ya kila siku ni mada ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye Jumatano 10 Februari ameendeleza akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume.Hakuna wakati mzuri zaidi kuliko mwingine wa kufanya mazungumzo na Mungu,amesisitiza kwamba kila wakati na kila kitu kinakuwa fursa ya kuzungumza naye.Kusali,hutusaidia kuwapenda wengine.Na hatupaswi kufikiria juu ya yaliyopita au yajayo,lakini tuzingatie ya leo,mahali pazuri pa kukutana na Mungu.

Na Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko akiwa katika Maktaba ya Kitume mjini Vatican, Jumatano, tarehe 10 Februari 2021, amejikita tafakari yake ya katekesi kuhusu mwendelezo wa mada ya sala ya kila siku, ya wakati wetu wa siku na kwamba hata katika njia, ofisini na vyombo vya usafiri. Kila eneo ni muafaka kwa ajili ya kuzungumza na Mungu. Papa amethibitisha kuwa mazungumzo na Mungu yanaendelea na kila mtu anayeomba ni kama mpenzi, ambaye hubeba mpendwa wake kila wakati moyoni mwake, popote alipo. Maombi pia yapo bila maneno na kila kitu inakuwa fursa ya kuongea na Mungu. Akili ya mwanadamuni ni wazi mbele ya siri, juu ya kile kinachopita zaidi yake: Siri hii haina uso wa kusumbua au kufadhaisha, Papa anasema. Kumjua Kristo kunatufanya tujiamini kwamba mahali ambapo macho yetu na macho ya akili zetu hayawezi kuona,  kama kuna kitu, lakini kumbe ni neema isiyo na mwisho. Maombi ya Kikristo huweka tumaini lisiloshindwa katika moyo wa mwanadamu, uzoefu wowote unagusa njia yetu, upendo wa Mungu unaweza kuibadilisha kuwa nzuri.

Siyo jana wala kesho ni leo hii

Papa Francisko akiendelea amenukuu katika Katekisimu ya Kanisa katoliki mahali ambapo amesisitiza kuwa katika mambo ya kila siku ambayo tunapewa na Roho Mtakatifu ni wakati uliopo ambao tunaweza kuutegemea. “ Siyo jana wala kesho, ni leo. Leo hii ni mkutano na Mungu, daima kuna leo ya kukutana Hakuna siku nyingine nzuri zaidi kuliko leo hii tuliyoipata. Watu ambao daima wanaishi kwa kufikiria juu ya siku zijazo: Lakini, itakuwa bora...japokuwa, hawachukulii ya  leo kama ilivyokuja. Hao  ni watu wanaoishi katika hewa, hawajui jinsi ya kuchukua hali halisi ya ukweli. Na leo ni kweli, leo ni thabiti. Na sala inafanyika  leo hii. Yesu anakuja kukutana nasi leo, hii leo ambayo tunaishi. Na ni sala ambayo hubadilisha leo hii kuwa neema, au tuseme, ambayo hutubadilisha: inatuliza hasira, inadumisha upendo, huzidisha furaha, inatia nguvu ya kusamehe. Katika nyakati nyingine itaonekana kwetu kuwa hatuishi tena, lakini neema hiyo inaishi na inafanya kazi ndani mwetu kupitia maombi.

Kuomba hutusaidia kupenda, tunaombea kila mtu

Sala hutupatia ujasiri, inatusindikiza maishani. Tuombe, kwa maana hiyo, kwa kila kitu na kwa ajili ya kila mtu, Papa amehimiza, na hata kwa wale ambao hatuwajui, hata kwa wale ambao ni maadui zetu, kama Injili inavyosisitiza. Maombi uongeza upendo mwingi. Tunaomba juu ya yote kwa ajili ya watu wasio na furaha, kwa wale ambao wanalia kwa wenye upweke na kukata tamaa ili kwamba wajue kuwa bado kuna upendo unaowasukuma. Maombi hufanya miujiza; na maskini kwa maana hiyo hutambua kuwa na  busara, kwa neema ya Mungu, kwamba, hata katika hali yao za hatari, sala ya Mkristo imeonesha huruma ya Yesu:

Usihukumu, lakini angalia ulimwengu kwa huruma

Yesu hakuhukumu ulimwengu, ameendelea Papa Francisko, kwamba alikuja kuuokoa. Ni mkono unaoongezeka. Ni wale wenye maisha mabaya, watu wale ambao huwahukumu wengine kila wakati, wanawalaani kila wakati, wakihukumu… Papa ameongeza kusema kuwa hayo ni maisha mabaya, yasiyo na furaha. Wakati Yesu alikuja kutuokoa. Fungua moyo wako, usamehe, uhalalishe wengine, uelewe, kuwa karibu na wengine pia, kuwa na huruma, usiwahukumu bali uwahurumie kama Yesu. Sisi sote ni wenye dhambi, na kumbuka lakini kwamba tunapendwa kila mmoja na Mungu. Kwa kuupenda ulimwengu huu kwa njia hiyo, kuupenda kwa upole amesema tutagundua kuwa kila siku na kila kitu kinabeba kipande cha siri ya Mungu iliyofichwa ndani yake.

Kusali kila siku ni moja ya sir iza Ufalme zilizofunuliwa kwa wadogo

Papa tena amenukuu kifungu kutoka Katekisimu ya Kanisa Katoliki: Kusali katika matukio ya kila siku na kila wakati ni moja ya siri za Ufalme zilizofunuliwa kwa wadogo, kwa watumishi wa Kristo, kwa maskini wa Heri. Ni vizuri na haki kuomba kwamba ujio wa Ufalme wa haki na amani uweze kutoa chachu ya safari ya historia, lakini pia ni muhimu kwa usawa kuchanganya hali za kila siku za unyenyekevu kupitia maombi. Sisi ni viumbe dhaifu, Papa anahitimisha, lakini tukijua jinsi ya kusali ndiyo heshima yetu kuu, ni nguvu zetu. Bwana yuko karibu nasi na maombi huleta miujiza.

Siku kuu ya Bikira Maria Lourdes

Katika salamu zake kwa lugha ya  Kiitaliano, mara baada ya tafakari ya  katekesi, Baba Mtakatifu Francisko amewaalika waamini kujitoa kujenga muktadha wao wa maisha: Katika jamii inayoendelea kutawanywa na tofauti na mafarakano , Papa amehiza kuwa wao wawe ishara ya mpango  wa upatanisho na udugu ambao una mizizi yake katika Injili na katika msaada muhimu wa sala . Hatimaye amekumbuka siku ya maadhimisho ya liturujia ya Bikira Maria mbarikiwa wa Lourdes itakayoadhimishwa tarehe 11 Februari:Ni matashi yangu  kwenu kumwiga Mama yetu katika hutafutaji wa kweli wa mapenzi ya Mungu.

KATEKESI YA PAPA 10 FEBRUARI
10 February 2021, 15:21