Tafuta

Vatican News
2021.02.12 Papa akutana na wawakilishi wa Taasisi ya kwa ajili ya Mafunzo Ulaya. 2021.02.12 Papa akutana na wawakilishi wa Taasisi ya kwa ajili ya Mafunzo Ulaya.  (© Vatican Media)

Papa Francisko kwa wasomi wa ulaya:kuzeni utamaduni wa kukutana

Francisko akihutubia ujumbe kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Ulaya, amesisitiza juu ya jitihada ya kujibu changamoto na kukuza mazungumzo na umoja, amewaachipa pemenekezo la akuelekeza akili na moyo wao kwa jili ya faida ya wote na maendeleo fungamani ya kila mtu,bila upendeleo au ubaguzi usio wa haki.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko Ijumaa tarehe 12 Februari 2021, amekutana na uwakilishi wa Taasisi ya Ulaya ya Mafunzo ya Kimataifa ulioongozwa na Kardinali A. Arborelius, askofu Mkuu wa Stockholm nchini Sweden. Akianza hotuba yake amewasalimu wote wanaoongoza Taasisi hiyo na kuwapongeza kwa ajili ya kuwakilisha Utamaduni wa makutano, uhusiano kimataifa, mazungumzo ya kidini  na amani na ambao wanawakilisha tunda la Mkutano uliofanyika huko Stockholm nchini Sweden mnamo 2019. Anawapongeza kuanzisha masuala mbali mbali kwa ajili ya kuhamasisha mazungumzo ya kidini na huduma ya umoja wa familia ya binadamu.

Papa Francisko akitazama hali halisi ya sasa, anasema kudumu kwa mgogoro wa kiafya ulimwenguni umesababisha uchungu na kuonesha dharura ya lazima katika kuhamasisha utumaduni wa kukutana kwa ajili ya ubinadamu wote ili kuweza kukuza kati ya wanaume na wanawake wa wakati wetu shauku ya kukutana na wengine na kutafuta jambo jumuishi, kujenga madaraja, kushirikishana mipango ambayo inajumuisha wote (Ft 216). Katika muktadha huo, Papa Francisko anatumia fursa kwa namna hiyo kuunga mkono utafiti wa majibu ya fursa na katika changamoto kwa  matazamio yanayoikabili dini ulimwenguni

Kama wasomi na wanadiplomasia kutoka nchi mbali mbali, wao na wenzao wanajikita katika nafasi muhimu kuhamasisha utamaduni huo. Kwa asili yake, Papa amebainisha kwamba mchango wao unahitaji hasa kuzingatia msingi wa uchambuzi na mwelekeo wa matumizi ya matokeo ya vitendo na uhusiano kwa kuzingatia hasa haki za watu maskini na waliotengwa zaidi. Kwa maneno mengine, akili na mioyo lazima vielewane katika kufuata wema wa pamoja ulimwenguni na kwa mujibu wa kuboresha tamaduni za Shule yaSalamanka, ili kufikia  maendeleo fungamani ya kila mtu bila upendeleo na ubaguzi.

Kwa sasa , kuhusiana na  ufungamanishawaji wa kulinda na kuhamasisha haki za wote, Papa Francisko ambainisha kwamba zinawatazama viongozi wa kisiasa na kidini na ili kweli utmaduni wa kukutaba uweze kuwapo kwa misingi ambayo dunia inaungana zaidi na kupatana. Ni kwa njia ya utamaduni tu ambao unaweza kupelekea hali endelevu na amani kwa wote na kama unyeti wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja. Papa Francisko aidha ameongeza kusema kuwa wakati ubinadamu unaendelea kukabiliana na ukosefu haki,na changamoto zilizopo, anawatia moyo wa kuendelea na jitihada za utafiti kwa njia mpya na bunifu, ambazo zilepeke ukuaji wa utamaduni wa makutano kwa faida ya maendeleo na ustawi wa kizazi kijacho. Anawashukuru kwa ujio wao na kuwaomba wamkumbuke katika sala zao.

12 February 2021, 16:10