Tafuta

Sala ya Malaika wa Bwana  Dominia tarehe 21 Februari 2021 Sala ya Malaika wa Bwana Dominia tarehe 21 Februari 2021 

Papa Francisko:Kamwe usiongee na shetani ni kutumia Neno la Mungu!

Katika tafakari ya Papa Fracisko Dominika ya kwanza ya Kwaresima,amejikita kufafanua juu ya Fumbo la maisha ya Kristo ambaye mesisitiza kuwa tangu mwanzo ilikuwa ni kupambana na mabaya na aina zake.Ni katika Injili ya siku ambayo inaelezea Yesu alikwenda jangwani kwa siku arobaini mahali pa majaribu na vishawishi.Papa anaonya kuwa makini na shetani bila kumpa nafasi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko, akiwa katika dirisha la kiutamaduni kutoa tafakari yake, Dominika tarehe 21 Februari 2021 kwa mahujaji na waamini waliofika kusali naye sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Petro amefafanua  Injili ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresima. Akianza tafakari hili amesema “Jumatano iliyopita, kwa ibada ya toba ya majivu, tumeanza safari ya Kwaresima. Leo ni Dominika ya kwanza ya kipindi hiki cha kilirutujia, ambapo Neno la Mungu linatuelekeza njia ya kuweza kuishi ili kuwa na ufanisi kwa siku arobaini ambazo zinatufikisha katika maadhimisho ya mwaka ya Pasaka. Ni njia aliyoipitia Yesu kwa mujibu wa Injili kama anavyoelezwa Marko kwa mtindo  wake. Mtindo huo unafafanua ukisema kuwa Yeye kabla ya kuanza kuhubiri, alifanya mafungo ya siku arobaini katika jangwa, mahali ambapo pia alijaribiwa na shetani: (Mk 1,12-15)”.

Jangwani ni mahali ambamo Yesu anazungumza katika moyo wa mtu

Mwinjili anasisitiza kuwa Roho alimsukuma Yesu katika jangwa. Roho Mtakatifu alimshukia juu yake haraka baada ya ubatizo alioupokea kutoka kwa Yohane katika Mto Yordani, Roho Mtakatifu huyo huyo sasa ndiye anamsukuma kwenda jangwani ili kukabiliana na mjaribu. Kuishi kwake Yesu kulikuwa  chini ya ishara ya Roho wa Mungu ambaye alimhuisha, alimhamasisha, na kumuongoza. Papa Francisko katika tafakari hii amependa kusisitiza juu ya jangwa na ambalo anasema ni katika mazingira asili na ishara namna hii muhimu ya Biblia. Jangwa ni mahali ambamo Yesu anazungumza katika moyo wa mtu, na mahalia ambamo panabubujika jibu la sala. Lakini pia ni mahali penye majaribu na vishawishi ambavyo mlaghai  hutumia fursa ya udhaifu na mahitaji ya mwanadamu kutoa sauti yake ya kilaghai, tofauti na ile ya Mungu.

Kila mwanzo wa Kwaresima hutolewa Injili ya majaribu ya Yesu jangwani

Kiukweli mara baada ya siku arobaini alizoishi Yesu jangwani, alianza lile duru kati ya Yesu na shetani, na ambalo litahitimisha na Mateso na Msalaba. Fumbo lote la Kristo ni mapambano dhidi ya Mabaya katika mitindo mbali mbali ya kama vile: Kuponya magonjwa, kufukuza pepo kwa waliopagawa na  kusamehe dhambi. Baada ya hatua ya kwanza ambayo Yesu alionekana kuzunguka na kutenda kwa nguvu ya Mungu, utafikiri kwamba shetani  anaushindi  hasa wakati Mwana wa Mungu alivyokataliwa, akaachwa na hatimaye kukamatwa na kuhukumiwa kifo. Kiukweli ni katika kifo ambacho kilikuwa ndiyo jangwa la mwisho la kupitia na kushinda moja kwa moja nguvu za shetani na kukomboa sisi sote. Papa Francisko amesema, kila mwaka, mwanzoni mwa Kwaresima, Injili hii ya majaribu ya Yesu katika jangwa inatukumbusha kuwa maisha ya kikristo katika nyayo za Bwana, ni mapambano dhidi ya roho ya ubaya. Ni kutuonesha kwamba Yesu alikabiliana kwa kupambana na mlaghai huyo na akamshinda; na wakati huo huo tunaoneshwa wazi kuwa shetani ana uwezo wa kutenda juu yetu katika vishawishi. Lazima kuwa na utambuzi wa uwepo wa adui huyo mlaghai, mwenye kujihusisha na hukumu yetu hapa duniani, kushindwa kwetu, na  kujiandaa kujilinda dhidi yake na kupambana naye. Neema ya  Mungu katika ushindi dhidi ya adui inatuhakikisha, kwa imani, sala na toba.

Hakuna kuzungumza na shetani ni kwa Neno la Mungu tu

Hata hivyo Papa Franisko amependa kusisitiza jambo moja kuwa katika majaribu ya Yesu kamwe hakuna kufanya mazungumzo na shetani. Katika maisha yake Yesu hakufanya mazungumzo na shetani kamwe. Alikuwa akiwatoa pepo wabaya kwa waliopagawa au kuhukumu na kumwonesha ubaya wake, lakini kamwe hakuongea naye. Na katika jangwa utafikiri mazungumzo yapo kwa sababu shetani anampa mapendekezo matatu na Yesu anajibu. Lakini Yesu hakujibu kwa maneno yake. Anajibu kwa kutumia Neno la Mungu kama inavyo elekezwa katika hatua tatu za Maandiko matakatifu. Na hii kwetu sote, Papa ameshauri. “Wakati anapokaribia mdanganyifu, anaanza kutudanganya: fikiria hivi, fanya hivyo ..., ni kutaka kujaribu na  kufanya mazungumzo naye, kama alivyofanya Eva kwani alisema: “Lakini haiwezekani kwa sababu sisi ...”, na kwa maana hiyo aliingia katika mazungumzo”. “Na ikiwa sisi tunainga kwenye mazungumzo na shetani tutashindwa”. Papa Francisko ametahadharisha kuwa “Wekeni haya vichwani na moyoni mwenu: pamoja na shetani hakuna mazungumzo, hakuna majadiliano yanayowezekana. Ni kwa Neno la Mungu tu”

Adui ameinama kaa makini lakini kumbukeni  kutozungumza naye

Katika kipindi cha Kwaresima Roho Mtakatifu atusukume hata sisi kama Yesu kuingia katika jangwa. Siyo sehemu halisi (tumeona) bali eneo la maisha halisi ambayo yanatakiwa ukimya, kujiweka kwenye usikivu wa Neno la Mungu, ili uongofu wa kweli uweze kutimizwa (taz. Sala ya Dominika ya I ya Kwaresima B). “Msiogope jangwa, tafuteni wakati mwingi zaidi wa sala, wa kimya na kuingia ndani mwetu binafsi. Msiogope”. Tunaitwa kutembea katika nyayo za Mungu, kujipyaisha ahadi za Ubatizo wetu: “unamkataa shetani na mambo yake yote na ulaghahi wake wote? “Adui ameinama kuweni makini. Lakini kumbukeni kamwe kutozungumza naye. Tujikabidhi chini ya maombezi ya Bikira Maria”. Papa amehitimisha.

TAFAKARI YA PAPA DOMINIKA 21 FEBRUARI
21 February 2021, 15:32