Tafuta

Papa atoa wito wa kulinda Maisha na ulinzi wa watoto wahamiaji

Makumi ya vijana na watoto peke yao kwenye njia za uhamiaji wanahitaji utunzaji na ulinzi,kama inavyotakiwa kila hatua ya maisha.Ni katika maneno ya Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana siku ambayo Baraza la Maaskofu nchini Italia wameitoa kwa ajili ya Maisha,inayoongozwa na kaulimbiu “Uhuru ni maisha”.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Utunzaji na njia za upendeleo za kibinadamu, ndivyo mtazamo na ombi la Papa Franciako kwa wale wote ambao wanalazimika kuhama katika mazingira magumu na yasiyo na usalama, hasa watoto wengi, wasio na msindikizaji. Hawa wako rohoni mwa Papa katika meneno yake baada ya sala ya Malaika wa Bwana Februari 7. Mtazamo wa Papa umewaendea kwa naama ya pekee njia,  kati ya nchi ya  Serbia na Kroatia, ambapo kwa siku kadhaa, makumi ya maelfu ya watu wamezuiliwa wakijaribu kuvuka mipaka ya Ulaya huku wakilazimika kukaa katika  hali isiyo ya kibinadamu katika kambi za muda mfupi:

Ninapenda kutoa wito kwa  ajili  ya watoto wahamiaji wasiosindikizwa. Ni wengi! Kwa bahati mbaya, kati ya wale ambao kwa sababu tofauti wanalazimika kuondoka nchi yao, na  daima kuna watoto kadhaa na vijana peke yao, bila familia zao na wako katika hatari nyingi. Katika siku za hivi karibuni, niliarifiwa juu ya hali mbaya ya wale ambao walijikuta kwenye kile kinachoitwa “Njia ya Balkani”. Lakini ni katika njia zote. Basi tufanye namna ya kwamba viumbe hivi dhaifu na wasio na kinga hawakosi utunzaji mzuri na njia za upendeleo za kibinadamu.

Maisha, zawadi ya kulindwa kutokana na  mashambulizi

Umakini na ulinzi wa maisha katika hatua  zake zote bado umerudi kusikika katika maneno ya Papa Francisko katika fursa ya “Siku ya kitaifa ya  43 ya Maisha” ambayo imeadhimishwa nchini Italia, Jumapili tarehe 7 Februari. Siku hii ilipendekezwa na Baraza la Maaskofu Italia  tangu 1978, ikiwa na kusudi la kuhamasisha na kukuza makaribisho ya maisha, hasa maisha ya kuzaliwa. Sherehe hii hufanyika kila mwaka, katika Jumapili ya kwanza ya mwezi Februari na mwaka huu imeongozwa na kaulimbiu “Uhuru ni maisha”: Ninaungana  na maaskofu wa Italia kukumbusha kuwa uhuru ni zawadi kubwa ambayo Mungu ametupatia kutafuta na kufikia wema wetu na wa wengine, kuanzia na wema  mkuu wa maisha. Jamii yetu lazima isaidiwe ili kupona kutokana na mashambulio yote ya maisha, na ili iweze kulindwa katika  kila hatua.

Kupungua kwa idadi ya watu, ni hatari kwa siku zijazo

Papa Francisko kabla ya kuwaaga waamini waliokusanyika katika uwaja wa Mtakatifu Petro, amelezea hata wasiwasi mwingine ambao bado unahusu nchi ya  Italia na kusema: Na niruhusu niongeze moja ya wasiwasi wangu: kuhusu kipindi cha kupungua  kwa  idadi ya watu wa Italia. Nchini Italia, kuzaliwa kumepungua na siku zijazo ziko hatarini. Hivyo tuwe na  wasiwasi huu na tujaribu kuhakikisha kuwa kipindi hiki  cha kupungua kwa idadi ya watu kinaisha na kipindi kipya cha watoto wa kike na kiume kinachanua.

Siku ya maombi na tafakari kwa ajili ya kukomesha biashara ya utumwa

Papa Francisko, kati ya miito mbalimbali aliyotoa kwa siku amekumbusha Siku kuu ya Mtakatifu Josephine Bakhita ambaye ni mwathirika wa utumwa sambamba na siku ya 7 ya Siku ya tafakari na maombi kwa ajili ya kukomesha utumwa. Papa amesema: Kesho ni kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Josephine Bakhita, mtawa wa Sudan ambaye alijua fedheha na mateso ya utumwa, na inaadhimishwa Siku ya Maombi na Tafakari dhidi ya biashara Haramu ya Watu. Ka mwaka huu lengo ni kufanya kazi kwa jili ya uchumi ambao haupendelei, hata kwa njia isiyo ya moja kwa moja, biashara hii ya unyonge, yaani uchumi ambao haufanyi wanaume na wanawake kuwa bidhaa, au kitu, badala yake uwe ndiyo mwisho. Na kwa maana hiyo iwe kwa ajili ya huduma ya mwanaume na mwanawake, lakini siyo kuwatumia kama bidhaa. Tamuombe Mtakatifu Josephine Bakhita atusaidie katika hili.

Shukrani kufika waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Papa Francisko hatimaye amewasalimia wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, waroma na mahujaji wote: Nina furaha kuwaona mmekusanyika uwanjani tena, hata wale wa kawaida, watawa wa Uhispania hapo, ambao wanaiìjitahidi, kila wakati, na mvua na jua wapo! Hata watoto wa Parokia Bikira Maria hasiye na doa. Kwa wote Papa amefurahi kuwaona na kuwatakia Jumapili njema. Wasiwasahau kusali kwa ajili yake na amewatakia mlo mwema.

 

07 February 2021, 19:06