Tafuta

2021.02.20 Edith Bruck na Papa Francisko 2021.02.20 Edith Bruck na Papa Francisko 

Papa amtembelea Edith Bruck,aliyeokoka huko Auschwitz

Mwandishi wa Hungaria,anakaribia miaka 90,anaishi Roma kwa muda mrefu ambapo Papa Francesco,Jumamosi 20 Februari kwa kumshangaza amemtembele nyumbani kwake katikati jiji.Ni katika kutaka kumshukuru kwa ushuhuda wake alioulezea wa vitisho alivyopata yeye na familia yake wakati wa mateso ya Kinazi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Alisoma mahojiano yake, ambayo yanaelezea vitisho alivyopata yeye na familia yake wakati wa mateso ya Kinazi na yalimshangaza sana. Kwa  njia hiyo aliomba kuweza kukutana naye na kwenda kumtembelea nyumbani kwake. Papa  Francisko aliondoka jijini Vatican Jumamosi  alasiri tarehe 20 Februari 2021 na kuelekea katikati ya jiji la  Roma kwa ziara yake  binafsi nyumbani kwa Bi. Edith Bruck, mwandishi Myahudi mwenye asili ya Hungaria ambaye ametumia theluthi mbili ya maisha yake nchini Italia. Wakati wa mazungumzo yao, Papa amemwaambia Bi Edith Bruck maneno haya: “Nimekuja hapa kukushukuru kwa ushuhuda wako na kutoa heshima kwa watu waliouawa shahidi na wazimu wa kinazi na kiukweli ninarudia kwako maneno niliyosema kutoka moyoni mwangu wakati wa  tukio la Yad Vashem na ambayo ninarudia mbele ya kila mtu kama wewe, aliyeteswa sana kwa sababu ya hiyo: Msamaha wa  Bwana kwa jina la ubinadamu”.

MSHANGAO WA BI EDITH NYUMBANI KWAKE
MSHANGAO WA BI EDITH NYUMBANI KWAKE

Na kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican kuhuzia na ziara hiyo fupi amesema  kwamba “mazungumzo na Papa yamerudisha nyuma kumbu kumbu kwa zile nyakati hizo za nuru ambazo zilionesha uzoefu kama kuzimu katika kambi za mateso na kuibua hofu na matumaini kwa wakati tunaoishi, wakisisitiza thamani ya kumbukumbu na jukumu la wazee katika kukuza na kurithisha vijana. Baada ya saa moja, Papa Francisko na Bi. Bruck wameagana na Papa akarudi jijini Vatican. Mkutano huo ulihudhuriwa na mkurugenzi wa Osservatore Romano, Andrea Monda, ambaye mnamo tarehe 26 Januari 2021 alikuwa ameweka mahojiano yake katika ukurasa wao yenye kugusa moyo na mwandishi huyo, yaliyoandaliwa na Francesca Romana de 'Angelis. Papa ametoa zawadi ya Mshumaa wa matawi saba ya dini ya Kiyahudi (menorah), kitabu, na Talmud ya Babeli. Hata hivyo Papa Francisko amejikuta katikati ya mshangao na joto la wapita njia wakati wa kuondoka nyumbani kwa Edith Bruck akirudia jijini Vatican.

PAPA AKIZUNGUMZA NA BI EDITH
PAPA AKIZUNGUMZA NA BI EDITH

Ushuhuda wa Edith:kidokezo cha ubinadamu kuruhudu kuishi tumaini

Walikuwa wageni wawili, ambao uvumi wao wa mwisho katika kambi ya mateso ya Bergen-Belsen, walimwuuliza afanye hivyo: Tusimulie, hawatakuamini, lakini ikiwa utaokoka, simulia na kueleza kwa ajili yetu”. Bi Edith Bruck alijitolea maisha yake yote kushuhudia kile alichokiona. Na alitimiza ahadi yake. Kinachoshangaza, katika kusoma vipindi vilivyoelezewa kwenye mahojiano, ni muonekano wa matumaini ambao Edith anaweza kuwasilisha. Hata wakati anasimulia juu ya nyakati zenye giza zaidi, za kuzimu kwa hofu ambayo yeye, kama mtoto, alizamishwa, akipoteza sehemu kubwa ya familia yake, na ambayo anasema huwa anashindwa kutazama kwa macho yake kuiweka katika maelezo mazuri, kidokezo cha ubinadamu ambacho kilimruhusu kuendelea kuishi na kutumaini.

 

21 February 2021, 11:28