Tafuta

Vatican News
Papa Francisko katika mahojiano Papa Francisko katika mahojiano 

Mzungumzo ya Papa kuhusu afya yake

Katika mahojiano na Papa 2019 katika kitabu cha mwandishi Nelson Castro,zimetolewa ndondoo katika gazeti La Nación nchini Argentina.Yaliyomo ni kama vile:Operesheni ya mapafu,wasiwasi katika kipindi cha udikteta alipoficha walionyanyaswa,mazungumzo na daktari wa magonjwa ya akili na ambaye alimsaidia kusoma matokeo ya manovisi.Na kuhusu kifo kwamba hakimtishi anafikiri kitamkuta Roma akiwa ofisini au mstaafu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Sina hofu ya kifo na ninakifikiri nitakuwa Roma ndivyo anathibitisha Papa Francisko katika Mahojihano yaliyotolewa ndondoo zake kwenye utangulizi na Gazeti la kila siku la Argentina liitwalo La Nación. Haya ni mazungumzo yaliyotokea miaka miwili iliyopita mnamo tarehe 16 Februari 2019 na mwandishi wa habari na daktari Nelson Castro kwa ajili ya kitabu chake juu ya “afya ya Papa”. Papa Francisko anathibitisha kujihisi vizuri na amejaa nguvu, akitoa shukrani kwa Mungu. Anakumbuka wakati mgumu mnamo 1957, akiwa na umri wa miaka 21, wakati alipotolewa tundu la juu ya pafu lake la kulia kwa sababu ya tezi tatu.  Papa anasema: “Nilipozinduka kutoka katika anesthesia, maumivu niliyohisi yalikuwa makali sana. Lakini si kwamba nilikuwa na wasiwasi, kwa sababu  siku zote nilikuwa na imani kwamba nitapona.”

Papa amesema  kuwa urejesho wa afya yake ulikuwa kamili: “Sijawahi kuhisi mapungufu katika shughuli zangu.” Hata katika safari mbali mbali za kimataifa anaeleza kuwa “Sikuwahi kuwa na ulazima ya kukwama au kughairi” shughuli zozote zilizopangwa: “Sijawahi kupata uchovu au ukosefu wa pumzi (dyspnea). Kama madaktari walivyonielezea, pafu la kulia limepanuka na kufunika hemithorax nzima ya pande zote”. Mwandishi wa habari alimwuliza Papa ikiwa amewahi kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kwa kujibu alisema: “Nitakwambia jinsi mambo yalivyokwenda. Sijawahi kujichambua kisaikolojia. Wakati nilikuwa kiongozi wa kanda ya Wajesuiti, wakati wa siku mbaya za udikteta, mahali ambapo nililazimika kuficha watu chini ya ardhi ili kuwaondoa nchini na kuokoa maisha yao, ilibidi nisimamie hali ambazo sikujua jinsi ya kushughulika nazo.

Nilikwenda kumtembelea mwanamke mmoja ambaye alikuwa amenisaidia kusoma vipimo vya kisaikolojia kwa ajili ya manovisi.  Kwa namna hiyo, katika miezi sita, nilikwenda kuomba ushauri mara moja kwa wiki”.  Alikuwa mtaalamu wa akili: “Katika miezi hiyo sita, alinisaidia kujielekeza jinsi ya kukabiliana na hofu ya wakati huo. Fikiria jinsi ilivyokuwa katika kubeba mtu aliyefichwa kwenye gari, amefunikwa na  blanketi moja tu na kupitia vizuizi vitatu vya kijeshi katika eneo la “Campo de Mayo. Mvutano uliokuwa ndani mwangu ulikuwa mkubwa sana”.

Papa aidha anasema, mahojiano na mtaalam wa magonjwa ya akili pia yalimsaidia kujifunza kudhibiti wasiwasi na kuepuka kufanya maamuzi ya haraka. Anazungumzia juu ya umuhimu wa utafiti wa kisaikolojia kwa kuhani: “Nina amini  kwamba kila kuhani lazima ajue saikolojia ya wanadamu”. Kwa maana hiyo anazungumza kuchanganyikiwa: “wakati wa kuchanganyikiwa lazima kujindaalia (mate) aina fulani ya utamaduni wa kinywaji nchini Argentina. Sio hivyo tu, lazima pia kuibembeleza. Ni rafiki wa mtu huyo katika maisha yake yote”. Papa Francisko, kama alivyokwisha sema mara kadhaa, anakumbuka alivyosoma kitabu ambacho kilimpendeza sana na kumfanya acheke kwa moyo wote: “Rejoice in Being Neurotic” yaani (Furahi ya kuwa umechanganyikiwa) cha daktari mmoja Mmarekani wa magonjwa ya akili, Louis E. Bisch: “ ni muhimu sana kuweza kujua mahali mifupa inaingilia. Yako wapi na mabaya yetu ya kiroho ni yapi. Baada ya muda, mtu hujifunza juu ya kuchanganyikiwa kwake mwenyewe (neuroses)”.

Papa Francisko katika mahujiano hayo anazungumza juu ya wasiwasi wa kutaka kufanya kila kitu mara moja. Ananukuu methali maarufu inayohusishwa na Napoleon Bonaparte:(alikuwa kiongozi wa kijeshi na wa kisiasa nchini Ufaransa baada ya mapinduzi ya Kifaransa: 1769-1821): “Nivalisheni polepole, nina haraka”. Amezungumzia juu ya hitaji la kwenda polepole.  Na mojawapo ya mitindo yake ni kumsikiliza Bach (huyu alikuwa mtunzi maarufu  wa Ujerumani na mwanamuziki 1685-1750): “Ananituliza na kunisaidia kuchambua matatizo vizuri”. Mwisho wa mahojiano, hayo mwandishi wa habari anauliza ikiwa anafikiria juu ya kifo: “Ndio”, anajibu Papa.  Ikiwa anaogopa, anajibu: “Hapana, hata kidogo”. Na jinsi gani anavyofikiria kifo chake: “Kama Papa, akiwa katika majukumu au mstaafu. Sitarudi Argentina”.

27 February 2021, 15:20