Tafuta

2020.11.17 Wakimbizi wakifika Jimbo Kuu la Calabar 2020.11.17 Wakimbizi wakifika Jimbo Kuu la Calabar 

Imetolewa Kauli mbiu ya Siku Wahamiaji na wakimbizi ulimwenguni 2021

Kwa mujibu wa Ofisi ya Wanahabari Vatican imetangaza kauli mbiu iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuongoza ujumbe wake wa Siku ya 107 ya Wahamiaji na Wakimbizi Ulimwenguni 2021 isemayo"kelekea sisi zaidi".Katika taarifa hiyo inasema mada hiyo imetokana na msukumo wa Waraka wa ‘Fratelli tutti’ yaani Wote ni ndugu kuhusu Ndugu wa ulimwengu.

Sr. Angela. Rwezaula -Vatican.

Papa Francisko amechagua kauli mbiu” Kuelekea sisi” zaidi,  ili kuongoza  ujumbe wake wa kiutamaduni wa  Siku ya 107  ijayo ya Wahamiaji na wakimbizi itakayoadhimishwa mnamo Dominika tarehe 26 Septemba 2021.  Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari wanaeleza kuwa Papa Francisko katika fursa hiyo amechagua kauli mbiu ya ujumbe huo unaoangazwa na Wito wake ya kwamba wasiwe ni wengine  bali, ni sisi tu,ambayo ni maneno yanayotoka katika kifungu cha Waraka wa kitume wa (Fratelli tutti 35). Na hii  “sisi” ya ulimwengu wote lazima iwe ukweli hasa ndani ya Kanisa mahali ambamo linaitwa  kufanya muungano katika utofauti”. Ujumbe wa Papa Francisko umegawanyika katika sehemu sita ambazo zinahitaji umakini kwa namna ya pekee utunzaji wa familia ya pamoja ambayo kwa pamoja ni kutunza nyumba yetu ya pamoja, ambayo ndiyo lengo kuu la “Sisi” ambao tunaweza kugeuka daima kuwa sehemu kubwa ya ukarimu.

Ili kuweza kuandaa vema maadhimisho ya siku hii, hata kwa mwaka huu kitengo cha Wahamiaji  na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu, wametengeneza Kampeni ya mawasiliano, ambayo itaweza kufanyiwa kazi katika kufafanua vifungu hivi sita vilivyo pendekezwa na Ujumbe huo. Kila mwezi watapendekeza kupitia vyombo vya habari, zana na tafakari ya kitaalimungu kupitia wataalam ambao watasaidia kufafanua kwa kina mada na vipengele vya ujumbe huo vilivyochaguliwa na Papa Francisko.

Katika Waraka wa Fratelli tutti kipengele cha 35 kinasema kuwa “hata kama tunasahau haraka mafunzo ya historia, “mwalimu wa maisha”, mara tu itakapoisha shida ya afya, athari mbaya zaidi zitakuwa ni kuanguka hata zaidi katika homa ya hutumiaji hovyo na aina mpya za kujilinda za ubinafsi. Kitakacho hitajika ni shauku ya mbingu ambayo mwishowe hakuna “wengine”, lakini  ni “sisi” tu. Na kwamba kutambua kuwa  hilo halikuwa tukio lingine kubwa la kihistoria ambalo hatukuweza kujifunza. Na kwamba hatusahau wazee waliokufa kwa kukosa vifaa vya kupumulia, katika sehemu kubwa kama hii ni matokeo  ya mifumo ya kiafya kufutwa kila mwaka. Na kwamba uchungu huu mkubwa usiwe wa bure na kuwa haukufanya  kuchukua hatua kuelekea njia mpya ya kuishi na kugundua mara moja na kwa yote kwamba tunahitaji na tuna deni, la mmoja na mwingine ili ubinadamu uzaliwe tena na nyuso zote, mikono yote na sauti zote, zaidi ya mipaka ambayo tumeunda.”

27 February 2021, 14:06