Tafuta

Vatican News

Wito wa Papa kwa ajili ya kutafuta suluhisho la amani nchini Yemen!

Papa Francisko anasikitishwa na majanga ya ukosefu wa amani yanayoendelea ulimwenguni kama vile nchini Yemen pia wazo lake na wito ni kwa ajili ya nchi ya Nigeria kutokana na wengi walio mikononi mwa wateka nyara.Ni matarajio yake kuwa inawezekana kupata suluhisho na melewano.Anawashukuru wote wanaojikita katika kuhamasisha amani na waliomtakia heri ya mwaka mpya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana akiwa katika Maktaba ya Jumba la kitume, tarehe Mosi Januari 2021, siku mpya ya kufungua mwaka na sherehe za Maria Mama wa Mungu ametoa wito katika ulimwengu kutokana na ukosefu wa amani. Katika muktadha huo, Papa Francisko ameonesha uchungu wake na wasiwasi kuhusiana na kuongezeka kwa vurugu nchni  Yemen, ambayo yamesaabaisha idadi kubwa ya waathirika na hivyo amesali ili waweze kupata suluhisho ambalo linawezesha kurudisha amani kwa ajili ya watu hao waliopata pigo. “ Kaka na dada, tufikiria watoto wa Yemen…bila elimu, bila madawa, na wenye njaa. Tume pamoja kwa ajili ya Yemen”, (kimya kwa sala )…

Kuungana na Jimbo Kuu katoliki la Owerri, Nigeria

Baada ya sala hiyo, Papa amependa kuungana na maombi na Jimbo Kuu katoliki la Owerri, Nigeria, kwa ajili ya askofu Moses Chikwe, na dreva wake ambao wametekwa nyara siku zililizopita. Amesema tuwaombee kwa Bwana na wale wote waathirika kama wao wa vitindo hivyo nchini Nigeria, waweze kurudi na kuwa na uhuru na kwamba nchi hiyo pendwa iweze kuwa na usalama, maelewano na amani.

Shukrani na matashi mema na wahamasishaji wa amani na mshikamano

Papa Francisko amesema: “Kwa wote ambao wameunganishwa kwa vyombo vya habari, ninawatakia heri ya amani na utulivu wa Mwaka Mpya. Ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Italia, Mheshimiwa  Sergio Mattarella, kwa mawazo mazuri aliyoniambia jana usiku katika ujumbe wake wa mwisho wa mwaka, na kwa moyo wote ninaurudisha heri hizo. Ninawashukuru wale wote katika kila sehemu ya ulimwengu, hata katika  kuheshimu vizuizi vilivyowekwa na janga, wamehamasisha wakati wa sala na tafakari juu ya tukio la  Siku ya Amani Ulimwenguni ya leo.” Aidha amesema kwa mawazo kwa namna ya pekee amekumbuka maandamano kwa njia ya mandao yaliypfanyika usiku a kuamkia tarehe Mosi , ambayo yameandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Chama cha Matendo ya kitume Katoliki, kama ilivyo pia mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio wa Amani duniani kwa njia ya mtandao tarehe 1 Januari. Kwa wote anawashukuru kuanzisisha shughuli hizo kwa ajili ya mapatano na maelewano kati ya watu. 

Kwaya ya watoto na vijana ya Sternsinger

Ameoa salam maalum kwa waimbaji wa Sternsinger, “i Cantori della Stella” ambao ni watoto na vijana nchini Ujerumani na Austria, ambapo licha ya kutokutembelea familia zao katika nyumba zao, wamepana namna ya kuwatangazia habari njema ya Noeli na kukukusanya zawadi kwa ajili ya wenzao wenye shida. Papa amehitimisha ujumbe huo kwa kuwatakia mema ya amani ya Bwana na mwaka wa tumaini na kwa ulinzi wa Maria Mtakatifu Mama wa Mungu. Wasiwahau kusali kwa ajili yake.

01 January 2021, 16:42