Tafuta

2017.12.02 Papa Francisko akisalimia mgojwa katika hospitali nchini Bangladesh, wakati wa ziara yake ya kitume . 2017.12.02 Papa Francisko akisalimia mgojwa katika hospitali nchini Bangladesh, wakati wa ziara yake ya kitume . 

Ujumbe wa Papa kwa Siku ya XXIX ya Wagonjwa duniani 2021

Katika Ujumbe wa Siku ya 29 ya Wagonjwa duniani,uliotolewa leo,Papa Francisko anahimiza kuwekeza katika utunzaji,kwa kumbusha kuwa afya ni wema msingi wa pamoja.Janga la sasa limeonesha mapungufu katika mifumo ya kiafya na wazee na walio katika mazingira magumu kila wakati hawahakikishiwi kupata matibabu kwa usawa."Mwalimu wenu ni mmoja,nanyi nyote ni ndugu",(Mt 23,8) ndiyo kauli mbiu inayoongoza ujumbe huo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko katika barua yake ya siku ya XXIX ya  wagonjwa duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 11 Februari katika siku kuu ya Bikira Maria wa Lourdes, Papa anasema ni kipindi muafaka kwa ajili ya kuwa na umakini kwa watu wagonwa na wale ambao wanawasaidia, iwe katika majengo ya  utunzaji au katika familia na jumuiya. Mawazo ya Papa kwa namna ya pekee yamekwenda kwa wale wote ulimwenguni ambao wanateseka na matokeo ya janga la virusi vya corona. Na wote hasa maskini, waliobaguliwa, anaonesha  ukaribu wa kiroho akiwakikishia sala  na upendo wa Kanisa. Kauli mbiu inayoongozwa ujumbe wa mwaka huu ni “ Mwalimu  wenu ni mmoja na ninyu nyote ni ndugu” (Mt 23,8).Uhusiano wa imani msingi wa kutunza wagonjwa. Kwa maan hiyo katika neno la Kiinjili Yesu anapinga vikali unafiki kwa wale ambao wanasema lakini hawatendi (Mt 23, 1-12).  Imani inapopunguzwa na kuishia kwenye maneno yasiyo zaa matunda, bila kuhusisha hisia na katika mahitaji ya mwingine, uthibiti unapunguza  imani ya kukaribia na kuishi kwa dhati. Ni hatari mbaya, kwa maana hiyo Yesu anatumia kilelezo kugumu ili kuweka umakini wa hatari ya kuangukia kwanye kuabudu miungu na kusema, “mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Papa Francisko amebainisha kuwa ndiyo hiyo daima imekuwa ikitendekea kwa wote, kwa sababu hakuna aliye nje ya ugonjwa huo wa unafiki, ugongwa mbaya sana ambao unazaa matokeo mabaya ya kuzuia maua yasichanue kwa wana wa Baba mmoja,nwanaoitwa kuishi kama ndugu wa ulimwengu. Mbele ya hali za mahitaji ya dada na kaka, Yesu anaelekeza kukutana  nao jambo  ambalo ni tofauti kabisa na unafiki. Anapendekeza kusimama, kusikiliza, kudumisha uhusiano wa moja kwa moja na watu na wengine, kuhusu uelewano na hisia kwa ajili yao na kuacha uingie ndani na mtindo hadi kufikia kubeba mzigo huo wakati wa kutoa huduma ( Lk 10,30-35).

Uzoefu wa ugonjwa unatufanya tuhisi udhaifu wetu

Papa Francisko katika ujumbe huo amesema,  uzoefu wa ugonjwa hutufanya tuhisi udhaifu wetu na,wakati huo huo, kuona hitaji la asili la mwingine. Hali ya kuwa viumbe inakuwa wazi zaidi na tunaona wazi kabisa utegemezi wetu kwa Mungu,  tunajikuta katika hali ya kukosa nguvu, kwa sababu afya yetu haitegemei uwezo wetu au kujitahidi kwetu (taz Mt 6:27). Ugonjwa unauliza swali la maana, ambalo kwa imani linaelekezwa kwa Mungu: swali ambalo linatafuta maana mpya na mwelekeo mpya wa kuishi, na ambalo wakati mwingine haliwezi kupata jibu mara moja. Marafiki na jamaa maranyingi  hawawezi kutusaidia kila wakati katika utafutaji huu mgumu. Katika suala hili, sura ya kibiblia ya Ayubu ni ishara, Papa Francisko amebainisha. Mke wake na marafiki hakuwawezi kumsindikiza katika mkasa wake, badala yake, walimshutumu, wakiongeza upweke na kufadhaika ndani yake. Ayubu aliangukia katika hali ya kutelekezwa na kutokuelewana. Lakini hasa kupitia udhaifu huo uliokithiri, kwa kukataa unafiki wote na kuchagua njia ya uaminifu kwa Mungu na kwa wengine, likafanya kilio chake cha kusisitiza kimfikie Mungu, ambaye mwishowe alijibu, akamfungulia upeo mpya.  Alimthibitishia kwamba mateso yake sio adhabu au kuachwa, na wala sio hali ya umbali kutoka kwa Mungu au ishara ya kutokujali kwake. Kwa maana hiyo kutoka moyo uliojeruhiwa na kuponywa kwa Ayubu, inapitia tangazo hilo lenye nguvu na linalogusa Bwana: “Nilikujua tu kwa kusikia, lakini sasa macho yangu yamekuona” (Ayubu 42,5).

Zipo sura nyingi za ugonjwa na wagonjwa

Ugonjwa daima una uso, na sio mmoja tu: una sura ya kila mgonjwa na  hata wale ambao wanahisi kupuuzwa, kutengwa, wahanga wa dhuluma za kijamii ambazo zinawanyima haki msingi (taz. Waraka  Wote ni Ndugu22). Janga la sasa limeleta upungufu wa mifumo ya afya na upungufu katika kusaidia watu wagonjwa. Ufikiaji wa matunzo hauhakikishiwi kila wakati kwa wazee, walio dhaifu na walio hatarini zaidi, na sio haki kila wakati,  Papa Francisko amebainisha. Hii inategemea na uchaguzi za sera za kisiasa, jinsi rasilimali zinavyosimamiwa na kujitoa kwa wale wanaoshikilia nafasi za uwajibikaji. Kuwekeza rasilimali katika utunzaji na usaidizi wa watu wagonjwa ni kipaumbele kilichounganishwa na kanuni kwamba afya ni wema wa kawaida wa pamoja, Papa amesisitiza. Wakati huo huo, janga hilo pia limeangazia kujitoa na ukarimu wa wahudumu wa afya, watu wakujitolea, wahudumu, mapadre, wanaume na wanawake watawa, ambao kwa weledi, kujinyima, hali ya uwajibikaji na upendo kwa jirani wamesaidia, kutunza, kufariji na kuhudumia wagonjwa wengi na familia zao. Kikundi kukubwa cha kimya cha wanaume na wanawake ambao wamechagua kutazama nyuso hizo, wakibeba majareha ya wagonjwa na ambao walihisi kuwa karibu kwa sababu ya kawaida yao ya familia ya wanadamu.

Huduma daima siyo ya kiitikadi  na wala hitaji la maoni, bali ni watu

Kiukweli, ukaribu ni manukato ya thamani, ambayo hutoa msaada na faraja kwa wale wanaateseka kwa ugonjwa. Kama Wakristo, Papa Francisko amesema tunaishi ukaribu kama mfano wa upendo wa Yesu Kristo, wa Msamaria mwema, ambaye kwa huruma alijifanya kuwa karibu na kila mwanadamu, aliyejeruhiwa na dhambi. Tukiungana naye kupitia matendo ya Roho Mtakatifu, tumeitwa kuwa wenye huruma kama Baba na kupenda, hasa, ndugu zetu wagonjwa, wadhaifu na wanaoteseka (taz. Yoh 13: 34-35). Na tunaishi ukaribu huu, zaidi ya kibinafsi, hata katika mtindo wa kijumiya, ambao kwa dhati upendo wa kidugu katika Kristo ufanya jamuiya inayoweza kuponya, ambayo haimwachi mtu yeyote, na ambayo ni kwa pamoja inakaribisha juu ya yote walio wadhaifu zaidi. Katika suala hili, Papa Francisko amependa kukumbuka umuhimu wa mshikamano wa kidugu, ambao umeoneshwa kwa usawa katika huduma na inaweza kuchukua mitindo tofauti, zote zikiwa zimeelekezwa kusaidia wengine. “Kuhudumia inamaanisha kuwajali wale ambao ni dhaifu katika familia zetu, katika jamii yetu, na watu wetu” (Mahubiri  huko Havana, 20 Septemba 2015). Katika ahadi hii, kila mtu anaweza “kuweka kando mahitaji yake na matarajio, tamaa zake za kuwa na nguvu zote mbele ya macho halisi ya wadhaifu zaidi. […] Huduma daima  inaangalia sura ya ndugu, hugusa mwili wake, huhisi ukaribu wake kwa kiwango cha kuteseka, wakati mwingine, na inataka uhamasishaji  wa ndugu. Kwa sababu hiyo, huduma kamwe siyo ya kiitikadi, kwani haitaji maoni, bali watu”.

Tiba bora ni kuwa na mantiki ya uhusiano:wagonjwa,wahudumu na familia za wagonjwa

Ili kuwe na tiba nzuri, hali ya uhusiano ni muhimu, na ambayo inaweza kuwa na njia kamili kwa mtu mgonjwa. Papa anabainisha. Katika kuimarisha mantiki hii pia inaweza kusaidia madaktari, wauguzi, wataalamu na watu wa kujitolea kuchukua jukumu kwa wale wanaoteseka kwa kuwasindikiza kwenye njia ya kupona, shukrani kwa uhusiano binafsi wa uaminifu (taz. Mkataba mpya wa Wafanyakazi wa Huduma ya Afya [2016], 4). Kwa  maana hiyo ni suala la kuanzisha mapatano kati ya wale wanaohitaji huduma na wale wanaowajali; mkataba unaotegemeana, kuaminiana na kuheshimiana, juu ya ukweli, upatikanaji, na  ili kushinda kizuizi chochote cha kujihami, kuweka hadhi ya mgonjwa katikati, kulinda taaluma ya wafanyakazi wa afya na kudumisha uhusiano mzuri na familia za wagonjwa. Ni katika uhusiano hasa  huu na mtu mgonjwa ambapo hupata chanzo kisichoisha cha motisha na nguvu katika upendo wa Kristo, kama inavyothibitishwa na ushuhuda wa milenia wa wanaume na wanawake ambao wamejitakasa kwa kuwahudumia wagonjwa, anabainisha Papa Francisko. Kwa dhati  kutoka katika fumbo la kifo na ufufuo wa Kristo ndipo unaibukwa ule upendo ambao unaweza kutoa maana kamili kwa hali halisi ya mgonjwa na ile ya wale wanaomjali. Injili inashuhudia hili mara nyingi, ikionesha kwamba uponyaji uliofanywa na Yesu kamwe siyo ishara za mazingaombwe, lakini kila wakati yalikuwa ni  matunda ya kukutana, ya uhusiano kati ya watu, na ambayo imani ya wale wanaoipa ilifanana na zawadi ya Mungu, iliyotolewa na Yesu na ambayo  inakaribisha, kwa ufupi  neno ambalo Yesu anarudia mara nyingi kusema: “Imani yako imekuokoa”.

Amri ya upendo iliyoachwa na Yesu inapata utimilifu katika uhusiano

Katika kipengele cha tano na cha mwisho, Papa Francisko amebainisha kwamba amri ya upendo, ambayo Yesu aliwaachia wanafunzi wake, inapata utimilifu halisi pia katika uhusiano na wagonjwa. Jamii ni ya kibinadamu zaidi na inajua zaidi jinsi ya kuwatunza wajumbe wake dhaifu na wanaoteseka, na inajua jinsi ya kuifanya kuwa na ufanisi uliohuishwa na upendo wa kindugu. Papa Francisko anaomba kujikita katika lengo hilo na kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayesalia peke yake, na kwamba hakuna mtu anayehisi kutengwa na kutelekezwa. Papa Francisko amewakabidhi wagonjwa wote, wahudumu wa afya na wale ambao wanajitahidi sana kusaidia wanaoteseka, kwa Maria Mama wa huruma na Afya ya wagonjwa. Kuanzia katika Grotto ya Lourdes na maeneo yake mengi ulimwenguni, Yeye adumishe imani na matumaini yetu, na atusaidie kusaidiana kwa upendo wa kidugu. Na kwa kila mmoja Papa amempatia Baraka yake kwa moyo mkunjufu.

UJUMBE WA PAPA WA SIKU YA WAGONJWA 2021
12 January 2021, 16:58