Tafuta

2021.01.09 Askofu Mkuu Oscar RizzatoMsimamizi wa Sadaka ya Kiume ya Papa tangu  1989 hadi 2007 2021.01.09 Askofu Mkuu Oscar RizzatoMsimamizi wa Sadaka ya Kiume ya Papa tangu 1989 hadi 2007 

Papa Francisko:Mons Rizzato alikuwa mtumishi mnyenyekevu wa Kanisa!

Katika siku ya mazishi ya Askofu Oscar Rizzato huko Arsego,Padua Papa Francisko ameeleza masikitiko yake kupitia salam za rambi rambi kwa wanafamilia na jumuiya nzima ya jimbo akikumbuka kwa shukrani kubwa jitihada zake alizotoa kwa unyenyekevu wa Kanisa huku akitunza maisha ya undani na umakini kwa walio wadhaifu zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, kwa niaba ya Papa Francisko, ametuma telegram kwa Askofu Claudio Cipolla  wa Padua ambaye  Jumamosi, tarehe 16 Januari 2020 saa 4.00 asubuhi, majira ya Ulaya ameongoza misa ya mazishi ya Askofu Mkuu Oscar Rizzato, aliyeaga dunia tarehe 11 Januari 2021. Ibada ya mazishi imefanyikia katika Parokia ya Arsego, Wilayani Padua, mahali alipozaliwa Askofu mkuu huyo ambaye alitumiaka Vatican kwanza katika ofisi ya ukatibu na baadaye kuwa Msimamizi wa Sdaka ya Kipapa kuanzia 1989 hadi 2007.  Katika telegram hiyo Kardinali anaandika kuwa “Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuelezea ukaribu wake kwa jumuiya nzima ya jimbo, akikumbuka kwa moyo wa shukrani mtumishi wa Kanisa ambaye alikuza maisha ya undani na umakini kwa walio wadhaifu zaidi na kujikita katika huduma yake ya kikuhani  kwa unyenyekevu, kwa namna ya pekee katika  Ofisi ya Katibu wa Vatican na Sadaka ya kitume

Katibu wa Vatican amekumbuka utendaji wake wa kazi Askofu Mkuu  Rizzato kwa jitihada kubwa za kushirikiana kichungaji hasa katika kuongoza na kusimamia sakramenti za ukristo hasa kipaimara. Aidha Kardinali Parolin ameeleza kuwa Papa Francisko wakati anasali kwa ajili ya marehemu na amependa sala hizi ziwafikia Jumuiya nzima ya jimbo, wanafamilia na wale wote wanao omboleza  kwa sababu ya kuondokewa naye na kuwatia moyo kwa baraka ya kitume. Kwa kuihitimisha anaunganisha salam zake  huku akiomba maombezi ya Bikira Maria Mama Mungu na wale wote ambao duniani walikuwa maskini na sasa ni matajiri mbinguni,na waliweza kunufaika kwa msaada wa Kaka ambaye wameoboliza.

Katika mahubiri ya Askofu Mattiazzo: kumbu kumbu ya namna yake ya kusali

Naye Askofu wa jimbo la Padua  wakati wa mahubiri yake amesema kuwa Askofu Mkuu alikuwa mtoto wa Arsego, mahali alipozaliwa katika familia yenye mizizi wa kina wa kikristo na kwa utayari wa kuitikia wito wake hasa wa kuwekwa wakfu moja kwa moja katika huduma kwa Bwana na kwa Kanisa. Askofu wa Padua ameelezea kumbu kumbu yake na Askofu Mkuu Oscar ambayo imemfanya akumbuke enzi wakati katika Taasisi ya Kiaskofu ya  imemepelekea Thiene, mahali ambapo yeye  mwenyewe alikuwa ni makamu Gombera wa seminari ndogo. Askofu amesema : “Nilimwona akiwa mdogo mbele ya tabernakulo” na  “ ikiwa ninahifadahi picha hiyo ni kwa sababu alishangaza sana. Mtu ambaye anasali akiwa amepiga magoti na katika hali ya kuabudu kwa kimya, ndiyo jambo ambalo lilinishangaza juu yake”. Baadaye kabisa, katika huduma ya Kanisa la ulimwengu , alijielezea zaidi roho yake kwa upendo mkubwa sana, katika hali halisi na matatizo ya ulimwengu na Kanisa, na zaidi akiwa karibu na mapapa wakuu, ambapo aliweza kutoa huduma yake kwa uaminifu.

Alichangia uongozi wake katika huduma ya mapapa

Askofu wa Jimbo la Padua aidha amesema, ni kuthibitisha kwamba Askofu Mkuu Oscar Rizzato alichangia, katika uongozi wake mwema tunu msingi ya huduma ambayo hawezi kuondolewa kwa mapapa katika wakati huo, katika moja ya nyakati muhimu na tukufu, lakini pia kati ya watu wenye shida sana katika Kanisa na jamii. Katika jukumu lake kama mtoaji wa huduma ya misaada ambayo ni zoezi la upendo wa kiinjili inayofanywa kwa niaba ya Papa, amesema askofu, na kwamba "linabaki limechapishwa kwenye karatasi nyingi na baraka za Papa ambazo alituma katika Kanisa lote na ambazo zinaibua huduma ya umoja wa imani na muungano wa Papa ambaye hutoa baraka na ulinzi wa Bwana". Askofu wa jimbo la Padua katika mahubiri hayo amewataka waamini waungane katika maadhimisho hayo kama jamuiya ya Kikristo kumkabidhi Ndugu yao Askofu mkuu huyo kwa Bwana Yesu, na hisia za shukrani za dhati kwa mema yote aliyotenda na kwa mfano mzuri wa maisha, aliyejitoa kabisa kwa huduma ya Ufalme wa Mungu ambaye sasa amewaacha.

Mshumaa wa Pasaka ni ishara ya ufufuko 

Na zaidi ni kujiuliza je! Askofu Mkuu Rizzato alipata wapi chanzo hai cha maisha yake na kufanya kazi kama kuhani na Askofu, ardhi ya kina ambalo alitoa nguvu za imani, matumaini na mapendo? Kwa kujibu swali hili amekumbusha kwamba ni katika maombi yake kama alivyokuwa ameanza kusema mwanzoni. Katikati ya maisha yake ya kiroho kulikuwa na Ekaristi, muungano wa karibu na Bwana Yesu, Mkate ulio hai na wa kweli wa uzima wa milele. Kwa kuongozwa na Injili iliyosomawa ta Mtakatifu Yohane 6: 51-58,  amesema kwamba ni maneno ya ajabu ya Yesu asemaye “Mimi ndimi mkate ulio hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote anayekula mkate huu ataishi milele”. Bwana, kwa upendo wake mkubwa kwetu, ametupatia Mwili wake na Damu yake, ili kila mtu anayekula asiangamie, lakini awe na uzima wa milele. Kuwa na uzima wa milele, sio maisha marefu tu, hii ni zaidi ya  yote tunayopaswa kutamani na kupokea kutoka kwa Bwana. Mshumaa wa Pasaka ambao ulikuwa umewekwa mbele ya jeneza ambalo lilikua na  mwili wa Askofu Mkuu Oscar ni uthibitisho mzito wa Kristo unaotukumbusha kwamba “Mimi ndiye ufufuo na uzima; kila mtu aniaminiye, hata akifa, ataishi” (Yoh 11:25).

Yesu katika sadaka yake alitupatia Ekaristi tusife

Ni muhimu tutafakari juu ya thamani isiyo na kifani ya Ekaristi, ambayo ni kituo kikuu cha maisha ya Kikristo, na juu ya uharibifu ambao janga la corona limeweza kusababisha kwa kuzuia au kupunguza kushiriki katika Ekaristi. Maisha ya Kikristo ni maisha ya kweli isiyo ya kawaida, na kama kila maisha inahitaji kulishwa, vinginevyo huangamia. Kwa kujitoa  maisha yake, Yesu katika sadaka yake  alitupatia Ekaristi ili tusife, lakini tuwe na uzima wa milele, yaani maisha ya watoto wa Mungu ambayo tayari yameanza hapa duniani na ambayo yatatimizwa kikamilifu katika heri ya Mbinguni, amesisitiza Askofu. Ni jambo la  kuogopwa hasa kushindwa kushiriki katika muungano wa Ekaristi abayo inaweza kusababisha kudhoofisha zaidi maisha ya Kikristo na Kanisa. Kwa hili amesisitiza Askofu “ni muhimu  tutoe kila ahadi na hata kujitoa kwa ushiriki mzuri katika Ekaristi katika Siku ya Bwana”. Askofu Mkuu Oscar Rizzato alitembea maishani mwake akiungwa mkono na kusaidiwa na Mkate wa Ekaristi na kwa nguvu hii alifikia karamu ya harusi ya Mwanakondoo. “Ametuacha kimwili kwa kuonekana, lakini kiroho yuko karibu zaidi na sisi. Na sisi, kwa moyo wa shukrani kwa mema yote aliyotaka na kutimiza, tunamwomba Bwana amkaribishe kwa uso wenye furaha katika Ufalme wake wa heri na amani, akimwambia: “Njoo, mtumishi mwema na mwaminifu, ingia kwenye furaha ya Bwana wako”, amehitimisha.

16 January 2021, 19:00