Tafuta

Mbele ya Bunge la Washington DC Mbele ya Bunge la Washington DC 

Papa Francisko:siyo wakati wa vurugu ni wakati wa kutafuta muafaka!

Kwa utangulizi,Papa Francisko amezungumzia juu ya shambulio la Bunge la Marekani katika mahojiano ,yatakayo rushwa na Chanel 5,tarehe 10 Januari jioni.Ili kuelewa na sio kurudia,anasema,lazima mtu ajifunze kutokana na historia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ili kuelewa na sio kurudia, lazima mtu ajifunze kutokana na historia. Ni katika mahojiano ya Papa Francisko na kituo cha Luninga cha matangazo 'Chanel 5' nchini  Italia ambayo yatarushwa tarehe 10 Januari 2021 jioni. Katika utuangulizi mfupi wa mahojiano hayo ni katika muktadha wa shambulio la Bunge la Marekani lililotokea tarehe 6 Januari, wakati waandamanaji wanaomuunga mkono Trump walipo shambulia Bunge la Marekani. Papa anazungumzia pia juu ya chaguo la maadili ya kupata chanjo akitumaini kwamba kila mtu atafanya hivyo.

Kwa mujibu wa Papa anasema, matukio ya kilimani yalikuwa mshangao kwake pia hata ikiwa  kwamba,  hakuna jamii yoyote  inayoweza kujiona kuwa iko nje na vikosi vya uasi wa ndani kama huo. “Nilishangaa kwa sababu ni watu wenye nidhamu katika demokrasia”. Walakini, Papa Francisko anabainisha, hata “katika ukweli uliokomaa kila wakati kuna jambo ambalo haliendi”, kuna watu “ambao huchukua njia dhidi ya jamuiya, dhidi ya demokrasia, na dhidi ya faida ya wote”.

Vurugu kwa hakika zinapaswa kulaaniwa, Papa anaendelea kusema: “harakati hizi lazima zilaaniwe kwa maana ya kuanzia kwa watu”. Hakuna watu, wanaoweza kujivunia kutokuwa na siku, ya kesi ya vurugu” na kwa nji hiyo ni suala la “kuelewa vizuri ili pasirudiwe na kujifunza kutokana na historia”, amesisitiza. Kwa hali yoyote, Papa Francisko amefafanua kuwa ili kuelewa ni jambo msingi kwa sababu ndiyo jinsi unaweza kupata suluhisho”.

Wakati wa mahojiano, Papa Francesko pia amezungumzia juu ya chaguo la maadili ya chanjo dhidi ya virusi vya corona ambayo imesababisha janga kuu, huku akitumainia kwamba kila mtu atafanya hivyo pia kwa kuheshimu maisha na afya ya wengine. Papa hata hivyo amebainisha kuwa amejiandikisha mwenyewe ili na yeye kuweza kupata chanjo ambazo zitataanza kutolewa  katika wiki zijazo jijini Vatican.

10 January 2021, 15:42